tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,861
- 18,285
mkuu, umeichunguza hiyo mikanda yenye bendera ya taifa pamoja na hiyo ya filimbi umekuta ni ORIGINAL au FAKE? kwa hiyo mmeishawakamata au bado mnawahoji? labda tuanzie hapa ili unifafanulie vizuri.
Kosa lao kubwa ni kutumia mkanda wenye bendera ya taifa ambao itabidi waeleze wametoa wapi.
Halafu mmoja wao (kati) amejipa cheo cha usajini yaani V tatu! , na pia wana mikanda ya filimbi inayopita kwenye mifuko ya mashati.
Lakini kama wangevaa hizo nguo tu na kutafuta mkanda wa aina nyingine, isingekuwa tabu.
Hata kofia walizotumia si za kipolisi kabisa.
Ila ukiangalia sana hutaweza kutofautisha sare za hao Ze Comedy na zile za polisi ukiondoa viatu vyenye rangi tofauti.
Mimi niliwahi kupitia mafunzo ya JKT miaka ya mwanzo ya 90s.
Kuna siku nilikuwa nyumbani kwa rafiki yangu kwa mapumziko ya mwisho wa wiki, nikiwa nimevalia magwanda ya JKT, nikatoka kidogo na rafiki yangu ambae alikuwa akiishi maneno ya mitaa ya Magole Upanga ambao upo karibu kabisa na makao makuu ya JKT.
Lakini nilijisahau na kuchomoa koti langu la juu kwa kuwa nilitaka kuwa "relaxed", na mkanda nilitoa basi nikakatiza kwenye geti la jamaa, ambao bila mimi kufahamu walikuwa wakinitamani kwa sana ili wanitie adabu kwa utovu wa nidhamu na kwamba nilikuwa nalidhalilisha vazi rasmi la kijeshi.
Yaliyonikuta hapo ndipo nikagundua kuwa haya mavazi yana thamani sana kwa ama jeshi la JWTZ au polisi na yalindwa na sheria.
Hivyo nazungumza kutokana na uzoefu wangu na haya mambo ya hizi sheria za haya mavazi.