Jeshi la Polisi lamkamata mchapisha maudhui Tiktok kwa tuhuma za kutukana viongozi

Kaka yake shetani

JF-Expert Member
Feb 1, 2023
3,611
8,746
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limemkamata na linamuhoji kwa kina Selemani Agai Gaya (18) Mkazi wa Kigamboni, kwa tuhuma za kutoa lugha ya matusi mtandaoni dhidi ya Viongozi Wakuu wa Serikali Tanzania kwa kutumia mtandao wa kijamii wa Tiktok.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro amesema “Mtuhumiwa huyu amekamatwa Julai 29, 2023, yeye na wenzake wamekuwa wakitengeneza maudhui ya mtandaoni (video) na kuzisambasa video hizo kwenye mitandao ya kijamii zenye kuwatukana na kuwafedhehesha Viongozi Wakuu wa Serikali katika akaunti zao za Tiktok, Mtuhumiwa huyu atafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo”

“Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kwa Mtu/ Watu wanaotoa lugha za matusi na fedheha kwa Viongozi wa Serikali kwa njia ya mtandao na njia nyingine yoyote, kuwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za kisheria limejipanga kuwafuatilia na kuwakamata, kuwahoji kwa kina kuhakikisha wanafikishwa haraka kwenye nyombo vya sheria
 
Kutokana na umri wake wa miaka 18, huyo kijana atakuwa ni miongoni mwa vijana wachache majasiri na wanaofuatilia masuala ya nchi kwa sababu vijana wenzake wapo bize na muziki. Kosa lake ni kutukana tu kwa sababu matusi ni kinyume cha sheria si kwa viongozi tu bali hata kwa watu wa kawaida.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Sasa wewe unataka tufanyaje? Whyyyyy???
 
Modification ya hii engine imefikia mwisho? What happened? 😳😳😳

Screenshot_20230719_114900_Chrome.jpg
 
Back
Top Bottom