figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,484
Barabara imefungwa (Indira Gandhi kutoka AKs hadi Morogoro Rd) kutokana na kuendelea na uvunjwaji wa Jengo la Ghorofa 16
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alitoa siku 18 kwa uongozi wa Manispaa ya Ilala kuvunja jengo la ghorofa 16 lililopo katika Mtaa wa Indira Gandhi kabla halijaleta maafa, kazi ambayo imeanza leo
Wafanyakazi wa Kampuni ya Patty Interplan iliyopewa kazi hiyo kwa gharama ya Sh1 bilioni, Waameanza utaratibu wa kubomoa. Mngulumi alisema gharama za ubomoaji zitalipwa na mmiliki wa jengo hilo ambaye ni Ali Raza Investment.
“Mtaa wa Indira Gandhi na Morogoro una watu wengi hivyo ghorofa likiwa limejengwa chini ya kiwango linaleta wasiwasi kwa wapitanjia,” alisema Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omar Kumbilamoto .
“Unajua wakati wa kubomoa hatari yoyote inaweza kutokea hivyo familia nyingi zimehama kwa ajili kujiepusha na maafa ambayo yanaweza kutokea,” alisema mmoja wa wafanyabiashara katika eneo hilo.