Dar express bus mnatia aibu

Dar express bus mnatia aibu

connections

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2013
Posts
2,840
Reaction score
3,908
Nimepanda basi la DAR EXPRESS toka DAR kwenda ARUSHA kwanza kauli za wakatisha tiketi pale UBUNGO ni za ajabu hasa (Mr. Mamkwe) kuingia garini abiria tunatukanwa ovyo ovyo kisa kuuliza kwa nini Dereva anaenda mwendo kasi ulipititiliza (Dereva Mr. Robert), kufika hotelini kwao chakula kibovu/kiporo na bei ya juu kuuliza nimeambulia kuambiwa kama hutaki ACHA, chooni nako uchafu umejaa mpaka juuu. Hakika zama za DAR EXPRESS zimekwisha
 
Kitambo sana hawa Dar express wameshapoteza network huwa sipandagi tena!
Pole sana!
 
Kwa kweli nahama rasmi Dar Express bora KILIMANJARO EXPRESS au IBRA LINE/BUFFALO/KIRUMO CHARO/MACHAME SAFARI
 
shukuru wewe ulifika salama.....mimi juzi nimemkatia tiket mama yangu kwa heshima nikaona nikate Dar express...nimempeleka jana saa moja asubuh nimeambulia kumakiza kwenye gar saa 5 kamili asubuh,.....amesafiri kwa shida amefika moshi saa 5 usiku...yaani kwa kweli ndio mwisho wangu huo kwa bwana Mremi.
 
Nimepanda basi la DAR EXPRESS toka DAR kwenda ARUSHA kwanza kauli za wakatisha tiketi pale UBUNGO ni za ajabu hasa (Mr. Mamkwe) kuingia garini abiria tunatukanwa ovyo ovyo kisa kuuliza kwa nini Dereva anaenda mwendo kasi ulipititiliza (Dereva Mr. Robert), kufika hotelini kwao chakula kibovu/kiporo na bei ya juu kuuliza nimeambulia kuambiwa kama hutaki ACHA, chooni nako ma.vi yamejaa mpaka juuu. Hakika zama za DAR EXPRESS zimekwisha

Wakati wa kurudi panda KIMOTCO
 
Ndani ya mabasi yao huwa kuna vijana wahudumu kama 4 hv wanaongea kama kasuku njia nzima kelele. Niliapa hii gari sitapanda kamwe.
 
mwacheni mzee mremi upumzike bana, ashaihudumia sana hii nchi katika kiwango cha juu kabisa kwa usafir wa basi. lisilo na mwisho ,mwanzo wake haukuwepo.
 
sisi abiria wa wifi nae mambo safi......chakula nangulukulu.......samaki wakumwaga
 
Achana na magari ya kizee panda FASTJET au kama nauli imepelea panda KILIMANJARO EXPRESS
 
kuna CHAKITO mzee Moshi Dar masaa 6 tu

ha ha ha umenikumbusha mbali sana...Chakito kama una presha lazima ufe huo mwendo sijapata kuona duh!!!

Dar express siku nyingi chaliiii. Kilimanjaro express ni zuri
 
Mremi kabaki jina tu ila hali mbaya , Nashangaa Klm express hana gari mpya lakin anauza kinyama kuliko huyu mzee Mremi
 
mwacheni mzee mremi upumzike bana, ashaihudumia sana hii nchi katika kiwango cha juu kabisa kwa usafir wa basi. lisilo na mwisho ,mwanzo wake haukuwepo.

Kale kabinti kanashindwa hata kumpatia ushauri huyu mzeee manake nasikia ako na ndogondogo
 
Voice of mtwara nadhani unazungumzia wale samaki wa buku, mpaka mia tano, haha, nangurukuru
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom