Dar bana...
Kila siku mambo na matukio humu yanaongezeka..
Maskini wanazidi kuwa wengi zaidi ya matajiri..
Matukio ni kibao!
Leo kuna matukio mengi niliyoyaona..ila kuna haya 2 yaliyonifanya niandike hapa..
1. Pale ubungo nimemwona mtu ambaye hana lips kabisaa (meno yapo nje) afu chini kuna kitambaa chenye maandishi Nimeona kichwa cha habari "SOMA UBARIKIWE"..na maandishi mengine ambayo yenyewe yanaherufi ndogo..sikuweza kuyasoma!
Baadhi wakimaliza wanarusha sarafu juu ya kile kitambaa..bila shaka ni sadaka
Na nahisi yule jamaa asiyekua na mdomo ndiyo anaomba msaada kwa style hyo.. *mungu amsaidie
2. Mbele kidogo kwenye mlango wakuingilia stand nikasikia kipaza sauti..
Jamaa anafundisha watu juu ya freemason..sijajua ana objectives zipi..
Watu wa dar es salaam hizi mambo za freemason kwenu zinafaida gani?
Kwa kujua ama kutokujua kuna faida gan?
Kama maisha ya hapa town yamewashinda nini kung'ang'ania hapa?
Hamwon gap ya umaskin inavyozidi kuwa kubwa?
Wale wa Lumumba! nyie mwanze tu kusepa..hali ngumu