Lapton2005
Member
- Dec 20, 2010
- 76
- 0
Lakini ipo siku tu dsm itabadirika katika maamuzi ya kuajiri hao wanao tuongoza.
oh, ndo maana ilala na temeke mbunge lazime awe born hiahia die hiahia siyo!..Poleni bandugu
wewe unaishi wapi???? Dar au nje????wana jf
kwa mtazamo wangu naona watu wa mikoani wamejitambua muda mrefu na hata kuchagua wabunge kutoka vyama vya upinzani tokea mabunge yaliyopita(ukiacha kawe na ubungo 2010),ukiangalia msukumo uliopo arusha,mara,mbeya ,kigoma,songea,kagera,mwanza nk utaliona hilo.je ni kwanini wana dar hawana mwamko sana wa kimapinduzi na ukizingatia wajanja wengi wapo hapo?
nawasilisha ukumbini
Watz wa dsm wako chini ya vigezo vingi mno. Kubwa lao ni maisha. Wengi wao ni wajasilia mali. Hawa ni wale, bila chapaa basi kila kitu hakiendi, wafanyakazi nao mshahara hautoshi. Omba omba ni wengi mno, mateja ni kabisa. Hapa asilimia kubwa ni wale waliokata tamaa na kuridhika na matatizo yao ukizingatia kwamba wengi ni wakuja. Inashangaza sana utakuta kwamba hata mambo ya jamii inakua ni mtu mmoja mmoja. Je mambo ya uchaguzi siitakuwa zaidi ya hapo?. Wapenda mabadiriko tupo wengi lakini tumezingirwa na roho ya kukata tamaa. Fikiria temeke, watu wake ni wale wa hali ya chini mno. Ilala pia wale wale tu. Tofauti na kinondoni imejazwa na watu wa kutoka AR,MS,MZ,TARIME n.k. Watu hawa ni wale wasiopenda ujinga katika mstakabari mzima wa haki na maisha.
Dar es Salaam hawajalal kama unvyofikiria. Hawana sababu ya kuwachaguwa wakuja. Utakuta hata hao wabunge wawili ni wakuja tu na wamechaguliwa na wakuja. Na madhara yake yataonekana baada ya muda si mrefu.
Dsm wanajua haki zao hawawezi kuingizwa mkenge wa kijinga kama wengine wa huko mikoani. Jimbo kama la Ilala linachangia 80% ya mapato ya serikali ya kila mwezi, sasa unafikiri wa kuja anaweza kulishika hilo jimbo? Hata CHADEMA japokuwa makao makuu yao yapo hapa dar waliogopa kuliingia hilo jimbo
Baada ya kufikiri kodogo, naona huyu jamaa aliosema Dar Es Salaam wamelala ana point.
Nyerere, alikaribishwa na vijana wa Dar. Hata suruali alikuwa hajawahi kuvaa, kwani alikuja hapa na kaptura. Akawazidi ujanja akaukwaa uRais halafu akawageuka vibaya sana.
Katika siku hizo Nyerere alikuwa akivaa kaptura na soksi ndefu, mavazi yaliyopendwa na walimu wa shule na hasa kivazi kilichopendwa na wale waliojiona wameelimika, hususan watu wenye asili ya bara. Nyerere amenukuliwa akisema kuwa ilikuwa Dossa Aziz ndiye aliyemtahadharisha kuwa maadam sasa anachanganyika na wazee haitakuwa vyema kwake kuonekana amevaa kaptura.
soma zaidi: An-nuur Na. 291
Wajanja wengi au wezi wengi ndio wapo dar.
Dar wizi mtupu kuanzia kwenye ngazi ya umachinga hadi mainvestors wakubwa.
Watu wa dar wanaangalia nafsi zao na mapinduzi ya kweli unatakiwa uangalie nafsi za wengine.
Wewe ulitaka avae kanzu na nusu koti? Waswahili wa Dar walikuwa waoga kupambana na Mkoloni, maneno mengi ya kwenye kahawa lakini hawawezi kujieleza mbele ya mkoloni. Wakaona wamtangulize JK wa Ukweli kwa vile ana asili ya ujasiri toka Mara. Lakini baada ya kupewa nchi na wakoloni si alimkabidhi nchi Kawawa yeye akaenda kuimarisha chama? Mwacheni Baba wa Taifa apumzike kwa amani huko aliko.
wallah naapa kumsikia (System at w0rk) (ZOMBA)anasapot thread japo with -ve perceptionBaada ya kufikiri kodogo, naona huyu jamaa aliosema Dar Es Salaam wamelala ana point.
Nyerere, alikaribishwa na vijana wa Dar. Hata suruali alikuwa hajawahi kuvaa, kwani alikuja hapa na kaptura. Akawazidi ujanja akaukwaa uRais halafu akawageuka vibaya sana.
Katika siku hizo Nyerere alikuwa akivaa kaptura na soksi ndefu, mavazi yaliyopendwa na walimu wa shule na hasa kivazi kilichopendwa na wale waliojiona wameelimika, hususan watu wenye asili ya bara. Nyerere amenukuliwa akisema kuwa ilikuwa Dossa Aziz ndiye aliyemtahadharisha kuwa maadam sasa anachanganyika na wazee haitakuwa vyema kwake kuonekana amevaa kaptura.
soma zaidi: An-nuur Na. 291
mkuu hiyo gazeti uliyoiquote inasomwa na na nyinyi walengwa tu,haiwezi kuuza hata kopi 1000 kwa wiki hapa dar kwenye population ya watu 5,000,000 lakini kwa kuwa mnajua kuongea sana vijiweni na kwenye daladala wapo wanaowasikiliza..humu JF ni community iliyoelimika japo sauti yao haisikiki mbali kwani ni watanzania wachache wenye uwezo wa kumiliki pc na mtandao au kufanya kazi ofisi zenye kuwa na uwezo huo.pia ni wachache wenye kumiliki simu zenye uwezo wa kubrowse na pia wenye uthubutu wa kunena kilichopo mioyoni mwao.wallah naapa kumsikia (System at w0rk) (ZOMBA)anasapot thread japo with -ve perception
Apart from Ubungo and Kawe the rest of Dar es salaam = Uswahili + fanaticism + Ignorance