Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,940
- 831,459
(Tusameheane kwa post za mfululizo)
Nimekutana na mabango makubwa ya kampuni ya matangazo ikiwa na mapicha makubwa kubwa ya viongozi wa kisiasa wakipanda miti na nyingine ya barabara iliyojaa mnazi ile ya mapambo
Nikajiuliza hii ndio Dar tunayoitaka kweli? Mnazi kwenye barabara chache za lami! Vipi miundombinu yote kwa ujumla?
Pale jangwani ndio kama kuingia kwenye moyo wa nchi au jiji vipi vile vibanda? Njia zote kuu za kuingia Dar zimesongwa na shughuli za biashara zilizo shaghala baghala, hakuna mpangilio kabisa mikaa chips mafundi washi mafundi magari machinga vitoroli nk nk
Kilichoonekana kwenye mabango ni upuuzi mwingine uliotengenezwa kwa gharama kubwa sana. Dar tuitakayo ni multibillion project sio hizi slogan za kukurupuka, mitaa kibao ya jiji barabara ziko hoi mitaro ya maji machafu iko hoi hivi vitu viwili tu kuviweka vizuri ni mamilioni ya dola na mpango madhubuti!!! Leo tunaonyeshwa picha za kutengeneza mtandaoni.
Vizuizi vya pingili ni fasheni mpya tuliaza kuona strabag lakini kwakuwa wenzetu wale walikuwa na mpango madhubuti, vya kwao havichukizi kivile
Sisi nasi tukaiga zilianza barabara ya Lumbuma kule watu wanakokatiza kusikohusika zikapigwa pingili za miti na kupakwa rangi na uzio wa Seng'enge! Ilikuwa haina namna ili kulinda bustani zetu katikati ya mji
Wenye kuona fursa wakachanganya na za kwao, kwenye maghala yao kuna tani za mabomba haziuziki, fasta ukatengenezwa mkakati pingili zikawa za mabomba ya chuma badala ya miti! What a nice deal! Zikapakwa na rangi ya Taifa sasa sijui zikichafuka nani ataziosha au zikioza na kuharibika?
Kilichonisikitisha sana ni pingili za barabara ya Sam Nujoma kutoka mwenge kwenda ubungo! Kwa kasi ya ajabu yakachimbwa mashimo na pingili zikafukiwa hata maeneo yasiyohitaji pingili, bwana mmoja akatangaza kuwa ukigonga pingili moja unalipa 5 , kesho yake kona ya mlimani city jamaa mmoja akazilaza kama kumi   
Kibaya zaidi bustani ya ile barabara ilikuwa imejazwa udongo uliotengeneza vifusi ila waweka pingili hawakulizingatia hilo pingili zikawekwa na rangi na minyororo juu! Siku chache baadae wakagundua kosa na kuleta excavator kuja kuondoa vifusi! Lilianza kidogo tu pale mwenge likachemsha kwasababu ya pingili
Upuuzi huu wa kukurupuka bila mipango umeleta gharama kubwa na umegeuka kichefuchefu, pingili nyingi zimegongwa mvua ya wiki iliyopita imezichafua rangi sasa sijui hii ndo Dar es salaam tuitakayo? Tusubiri mwakani sio mbali