Dar es Salaam tuitakayo, Jiji la pingili!

Dar es Salaam tuitakayo, Jiji la pingili!

Tuache kulalamika lalamika kama wanawake bhanaa.., haipendezi kwa kweli.., sure nawaambia. Hiki kimradi mnachokibeza kimependezesha sana mji na kimeonyesha mwanga kwa miaka ijayo. Kazi kulalamika tu..
Unadharau sana wanawake siyo? Unajua kuwa unaitwa mwanaume (kama wewe ni mwanaume lakini) kwakuwa kuna wanawake?

Kwahiyo kwako hivyo vi-activity vya kuendeshwa na "UKUTA" vinaipendezesha Dsm? Kwako Dsm inapendeza hivo?

Waambie wawatumie wataalam waliopo Halmashauri wakae washindanishwe ku-plan mwonekano wa kila Municipal kisha nzuri ndiyo itumike kupendezesha Jiji.

Siyo mnakaa kulamba nyayo za "mabwana zenu"
 
Duuuu, mbona mim naona kama zitakua mwarobaini wa kukatiza ovyo barabara lkn pia zitasaidia kulinda bustan zetuu?? Anyway sikuhiz kila jambo la serikali linaonekana baya! Hata Bombadier ziliitwa mapanga boi

Tuna mawazo tofauti, tukubaliane hivyo tu coz hata mimi naona ni kitu kizuri, wapo wanaoona it's waste of money and energy. Sasa hivi wameanza Mandela road, kuna maeneo yalikuwa ovyo sana, pale chama wameweka bomba baada ya kujenga daraja, kwangu it's a massive move kwa sababu sasa hivi watu wanapita juu, at least 99% ya watu wanapita juu. Wameshaanza kupanda miti na kila siku asubuhi ukipita kuna gari inamwaga maji, I hope with time zile bomba zotawekwa njia yote. Ukipita nyerere road kunapendeza sasa hivi.

Popote nilipoona zile bomba, kuna tofauti kubwa, kuna greenish moja nzuri inaanza kuonekana, challenges zipo, zitakuwepo tu coz jiji limezidiwa, halina miundombinu mizuri, watu wake ni wachafu wa akili na mazingira yao.

Hilo la biashara kila mahali ni tatizo kubwa, hata mimi linanikera, bahati mbaya sana mh. Rais alipiga marufuku kufanya biashara ovyo, Makonda akajitahidi, hasa kariakoo na ubungo sijui nini kilimpata mkulu, akaruhusu tena kariakoo kuchafuliwe...pathetic sana!!!

Ni mawazo tofauti tu, inabidi tuvumiliane
 
Nani kalipia yake mabango yenye mipicha mikuuubwa namna ile?
GSM baada ya kupata tender (ambayo haikutangwaza) ya kusupply bomba na chain zilizotumika kuweka pingili. Na wameshindwa hata kufikiri hao waliosimamia mradi kwenda kuweka bomba salender bridge ambapo kuna bahari. Baada ya wiki ukipita bomba zishashika kutu. Tanzania yetu ya kubana matumizi.
 
Hiki ndio nilichokuwa namaanisha
1477290063121.jpg
1477290070483.jpg
1477290074966.jpg
tingatinga limeshindwa kuendelea na kazi kwa sababu ya vyuma ambavyo vingewekwa baada ya kusawazisha
1477290137098.jpg
1477290145013.jpg
hapa ni round about ya vinyago , kulikuwa na uharaka wa nini kusimika hizo pingili kabla ya kuondoa vifusi? Naamini nimeeleweka sasa
 
GSM baada ya kupata tender (ambayo haikutangwaza) ya kusupply bomba na chain zilizotumika kuweka pingili. Na wameshindwa hata kufikiri hao waliosimamia mradi kwenda kuweka bomba salender bridge ambapo kuna bahari. Baada ya wiki ukipita bomba zishashika kutu. Tanzania yetu ya kubana matumizi.
Ikifika December nyingi zitakuwa hazipo kwa kugeuzwa chuma chakavu
 
(Tusameheane kwa post za mfululizo)

Nimekutana na mabango makubwa ya kampuni ya matangazo ikiwa na mapicha makubwa kubwa ya viongozi wa kisiasa wakipanda miti na nyingine ya barabara iliyojaa mnazi ile ya mapambo

Nikajiuliza hii ndio Dar tunayoitaka kweli? Mnazi kwenye barabara chache za lami! Vipi miundombinu yote kwa ujumla?

Pale jangwani ndio kama kuingia kwenye moyo wa nchi au jiji vipi vile vibanda? Njia zote kuu za kuingia Dar zimesongwa na shughuli za biashara zilizo shaghala baghala, hakuna mpangilio kabisa mikaa chips mafundi washi mafundi magari machinga vitoroli nk nk

Kilichoonekana kwenye mabango ni upuuzi mwingine uliotengenezwa kwa gharama kubwa sana. Dar tuitakayo ni multibillion project sio hizi slogan za kukurupuka, mitaa kibao ya jiji barabara ziko hoi mitaro ya maji machafu iko hoi hivi vitu viwili tu kuviweka vizuri ni mamilioni ya dola na mpango madhubuti!!! Leo tunaonyeshwa picha za kutengeneza mtandaoni.

Vizuizi vya pingili ni fasheni mpya tuliaza kuona strabag lakini kwakuwa wenzetu wale walikuwa na mpango madhubuti, vya kwao havichukizi kivile
Sisi nasi tukaiga zilianza barabara ya Lumbuma kule watu wanakokatiza kusikohusika zikapigwa pingili za miti na kupakwa rangi na uzio wa Seng'enge! Ilikuwa haina namna ili kulinda bustani zetu katikati ya mji

Wenye kuona fursa wakachanganya na za kwao, kwenye maghala yao kuna tani za mabomba haziuziki, fasta ukatengenezwa mkakati pingili zikawa za mabomba ya chuma badala ya miti! What a nice deal! Zikapakwa na rangi ya Taifa sasa sijui zikichafuka nani ataziosha au zikioza na kuharibika?

Kilichonisikitisha sana ni pingili za barabara ya Sam Nujoma kutoka mwenge kwenda ubungo! Kwa kasi ya ajabu yakachimbwa mashimo na pingili zikafukiwa hata maeneo yasiyohitaji pingili, bwana mmoja akatangaza kuwa ukigonga pingili moja unalipa 5 , kesho yake kona ya mlimani city jamaa mmoja akazilaza kama kumi   

Kibaya zaidi bustani ya ile barabara ilikuwa imejazwa udongo uliotengeneza vifusi ila waweka pingili hawakulizingatia hilo pingili zikawekwa na rangi na minyororo juu! Siku chache baadae wakagundua kosa na kuleta excavator kuja kuondoa vifusi! Lilianza kidogo tu pale mwenge likachemsha kwasababu ya pingili

Upuuzi huu wa kukurupuka bila mipango umeleta gharama kubwa na umegeuka kichefuchefu, pingili nyingi zimegongwa mvua ya wiki iliyopita imezichafua rangi sasa sijui hii ndo Dar es salaam tuitakayo? Tusubiri mwakani sio mbali

Tupo Huku Karibu sana hii haina mashiko kwa sasa Trending topic ni Mpigie kura Rais Magufuli kwenye Forbes Africa Person of the year
 
Ni mtazamo tu! Watapiga kura wenye viherehere, mngejua mnazidi kumpoteza na kumpotosh....!!!!
Na ndio maana unaleta thread kama hizi kwasababu ya chuki yako na huyo mtu. Kwako wewe unaona ni sawa ilivyokuwa zamani katikati ya barabara kuwe na michanga kwa sababu ya watu kuvuka hovyo kila sehemu na kukanyaga majani. Ngoja tusubiri huo mwaka uishe labda dua lako la hii kampeni lisifanikiwe litakuwa kweli.
 
Na ndio maana unaleta thread kama hizi kwasababu ya chuki yako na huyo mtu. Kwako wewe unaona ni sawa ilivyokuwa zamani katikati ya barabara kuwe na michanga kwa sababu ya watu kuvuka hovyo kila sehemu na kukanyaga majani. Ngoja tusubiri huo mwaka uishe labda dua lako la hii kampeni lisifanikiwe litakuwa kweli.
[emoji1] [emoji1] [emoji1] kumbe hata wewe hujanielewa
 
Back
Top Bottom