Write your reply...
mambo mengine yanakera kwa kweli,huku kwetu nyerere road kuna pingili zile zilizopakwa rangi ya bendera zinasikitisha sana unakuta hapa kuna pingili pale hakuna,hii imelalia kushoto ile imeegamia kulia,pingili zingine zimeng'oka zimelala pembeni,wala hakuna mtu anayeshughulika nazo,zile taa za barabarani(achana na traffic lights) zile taa zinazoleta mwanga barabarani,nazo pia zinatia huruma,zimechakaa,nyingine zimepasuka,nyingine zinawaka nyingine haziwaki,nyingine zimeinamia kulia nyingine kushoto,hivi serikali haiwezi kuajiri watu wa kuzihudumia??au zikabadilishwa kabisa?mbona wanaweza kugawa mamilioni mbele ya halaiki? wanashindwa vp kuboresha miundombinu ambayo kila mwananchi hufaidika nayo?unaweza ukaangalia tu kwamba hii nyerere road ni mlango wa wageni wanaoingia tanzania,wanaweza wakaona hawa watanzania ni watu wa hovyo na wavivu kwa kutazama mambo kama haya ambayo sisi tunayaona madogo,mgeni anashuka kwenye airport nzuri na ya kisasa kabisa lakini akitoka tu nje kwenye barabara anashuhudia kituko
sijui hawa viongozi wetu wana matatizo gani aiseee