Dar es Salaam tuitakayo, Jiji la pingili!

Dar es Salaam tuitakayo, Jiji la pingili!

(Tusameheane kwa post za mfululizo)

Nimekutana na mabango makubwa ya kampuni ya matangazo ikiwa na mapicha makubwa kubwa ya viongozi wa kisiasa wakipanda miti na nyingine ya barabara iliyojaa mnazi ile ya mapambo

Nikajiuliza hii ndio Dar tunayoitaka kweli? Mnazi kwenye barabara chache za lami! Vipi miundombinu yote kwa ujumla?

Pale jangwani ndio kama kuingia kwenye moyo wa nchi au jiji vipi vile vibanda? Njia zote kuu za kuingia Dar zimesongwa na shughuli za biashara zilizo shaghala baghala, hakuna mpangilio kabisa mikaa chips mafundi washi mafundi magari machinga vitoroli nk nk

Kilichoonekana kwenye mabango ni upuuzi mwingine uliotengenezwa kwa gharama kubwa sana. Dar tuitakayo ni multibillion project sio hizi slogan za kukurupuka, mitaa kibao ya jiji barabara ziko hoi mitaro ya maji machafu iko hoi hivi vitu viwili tu kuviweka vizuri ni mamilioni ya dola na mpango madhubuti!!! Leo tunaonyeshwa picha za kutengeneza mtandaoni.

Vizuizi vya pingili ni fasheni mpya tuliaza kuona strabag lakini kwakuwa wenzetu wale walikuwa na mpango madhubuti, vya kwao havichukizi kivile
Sisi nasi tukaiga zilianza barabara ya Lumbuma kule watu wanakokatiza kusikohusika zikapigwa pingili za miti na kupakwa rangi na uzio wa Seng'enge! Ilikuwa haina namna ili kulinda bustani zetu katikati ya mji

Wenye kuona fursa wakachanganya na za kwao, kwenye maghala yao kuna tani za mabomba haziuziki, fasta ukatengenezwa mkakati pingili zikawa za mabomba ya chuma badala ya miti! What a nice deal! Zikapakwa na rangi ya Taifa sasa sijui zikichafuka nani ataziosha au zikioza na kuharibika?

Kilichonisikitisha sana ni pingili za barabara ya Sam Nujoma kutoka mwenge kwenda ubungo! Kwa kasi ya ajabu yakachimbwa mashimo na pingili zikafukiwa hata maeneo yasiyohitaji pingili, bwana mmoja akatangaza kuwa ukigonga pingili moja unalipa 5 , kesho yake kona ya mlimani city jamaa mmoja akazilaza kama kumi   

Kibaya zaidi bustani ya ile barabara ilikuwa imejazwa udongo uliotengeneza vifusi ila waweka pingili hawakulizingatia hilo pingili zikawekwa na rangi na minyororo juu! Siku chache baadae wakagundua kosa na kuleta excavator kuja kuondoa vifusi! Lilianza kidogo tu pale mwenge likachemsha kwasababu ya pingili

Upuuzi huu wa kukurupuka bila mipango umeleta gharama kubwa na umegeuka kichefuchefu, pingili nyingi zimegongwa mvua ya wiki iliyopita imezichafua rangi sasa sijui hii ndo Dar es salaam tuitakayo? Tusubiri mwakani sio mbali
Umesahau kuongeza haya yafuatayo: ni miaka 50 toka uhuru kuna barabara kati ya jiji hazina lami wa taa za barabarani, mfano kariakoo, ilala, najiuliza kama city center haina lami haya sie tuishio mashenzini ni linilami itatufikia,!! hakuna njia za waenda kwa miguu, zote either ni mbovu au zina biashara au magari yameegeshwa, hakuna anaejali wala kufuatilia hatari tunayoipata, Sasa hivi tunatembea barabarani pamoja na magari, kama kariakoo,mitaa ya city drive. Cha kushangaza kodi zinakusanywa kila uchao, ushauri wangu mfumo wa jiji kuendeshwa na manispaa 'UVUNJWE NA TUUNDE MAMLAKA YA JIJI AU WIZARA YA JIJI LA DAR ES SSLAAM' pawepo na direct administration ya hii miji mikubwa kama ilivyo kwa jiji la Nairobi, mtindo huu wa kuendesha jiji kwa vikao vya madiwani ni vikao vya posho visivyo na tija na tenda feki ambazo kwa kiwango kikubwa ndio zimetufikisha nchi hii hapa tulipofikia matokeo yake tunaenda kuwa omba omba kwa nchi kama 'MOROCCO' ambao tumepata wote uhuru miaka ya sitini,,, AIBU!!!!
 
Wako kwenye maombi ya mheshimiwa nini?
Upo bado bongo au umeshaenda masafa tena? Nimeona ombaomba wa misikiti na viwanja nikakumbuka mtukufu wa Zenj siku ya mwenge alisema hawana shida na misaada ya hao watu. Nahisi walimaanisha ya Mangaribi siyo ya manshariki na mankati.
 
1477453909265.jpg
kazi ya kuweka pingili bila kufanya levelling kwanza Ilifanyika kwa kasi kubwa LAKINI kazi ya kurekebisha kosa la kwanza inamaliza mwezi sasa haijakamilika na sasa kinachoonekana ni uchafu! Hapo ni mwenge mkabala na kituo cha mafuta cha PUMA upande wa barabara ya Sam Nujoma
 
Tuache kulalamika lalamika kama wanawake bhanaa.., haipendezi kwa kweli.., sure nawaambia. Hiki kimradi mnachokibeza kimependezesha sana mji na kimeonyesha mwanga kwa miaka ijayo. Kazi kulalamika tu..
Umewadhalilisha wanawake...post yako inawafanya waonekane wasio na maana wala akili (common sense).
Kwa nini utumie mwanamke kama alama ya dhana mbaya na ya kukera??
Jirekebishe.
 
Umewadhalilisha wanawake...post yako inawafanya waonekane wasio na maana wala akili (common sense).
Kwa nini utumie mwanamke kama alama ya dhana mbaya na ya kukera??
Jirekebishe.
Naamini kapitiwa na amelitambua kosa lake hivyo atajirekebisha
 
Mkandarasi wa dar katika ubora wakes
1477746145194.jpg
 
MREJESHO
Miti mingi imekufa pingili nyingi za chuma zimegongwa ama kung'olewa uchafu umerudi maeneo husika...Dar es salaam tuitakayo ni operation iliyofeli kilichobaki ni mabango makubwa
 
MREJESHO
Miti mingi imekufa pingili nyingi za chuma zimegongwa ama kung'olewa uchafu umerudi maeneo husika...Dar es salaam tuitakayo ni operation iliyofeli kilichobaki ni mabango makubwa
Hivi huwa yanalipiwa na nani
 
Back
Top Bottom