Tetesi: Dar es Salaam SGR Terminus kupewa jina la Rais Samia

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,860
12,291
Habari zenu wana JF wenzangu,

Hizi ni tetesi kutoka kwa mtu wa ndani ya kitengo fulani, ambapo amesema mpango huo wa kuipa Terminus hiyo jina la raisi Samia utafanyika siku ya ufunguzi wa safari za train hizo zinazotumia umeme.

Mdau huyo amesema kwamba lengo kuu la kuipa Terminus hiyo kubwa, nzuri na yenye kuvutia kuliko Terminus yoyote barabarani Africa ukiondoa tu ile ya Johannesburg nchini Afrika kusini, inatokana na mchango mkubwa wa raisi huyo katika kumalizia mradi huu mkubwa na wenye manufaa kwa Taifa, uliyoachwa na mtangulizi wake ambae ni baba wa pili wa taifa hili (baada ya Nyerere) na mzalendo namba mbili (baada ya Nyerere) hayati John Pombe Magufuli.

Inasemekana Terminus hiyo itaanza kuitwa rasmi kwa jina la "Samia SGR Terminus" siku hiyo ya ufunguzi wa Terminus hiyo, na bila shaka litapokekelewa kwa mikono miwili na viongozi wote wa mkoa wa Dar es Salaam pamoja na wizara inayohusika na maswala hayo ya kitaifa.

Sisi wana Dar es Salaam na watanzania kwa ujumla tunasubiri kulipokea suala hili kwa mikono miwili. Tunajua haters huwa hawakosekani, lkn hilo halina shida kwani kelele za mpangaji hazimzuii mwenye nyumba kulala usingizi mtamu.

Samia SGR Terminus imekamilika, tujiandae kwa ufunguzi wa safari mbalimbali.

images (3).jpeg
 
Hakuna majina mazuri mazuri ya kuipa miradi yetu hadi ipewe majina ya viongozi?
Kwani hata hayo si mazuri mkuu? Mbona kuna barabara zetu zimepewa majina hata ya watu tusiowajua. Ukiuliza unaambiwa sijui alikuwa mpigania uhuru wa Togo, Msumbiji au sehem fulani.
 
View attachment 2593948
Wangeiita Ashraf Hakimi
 
Kwani hata hayo si mazuri mkuu? Mbona kuna barabara zetu zimepewa majina hata ya watu tusiowajua. Ukiuliza unaambiwa sijui alikuwa mpigania uhuru wa Togo, Msumbiji au sehem fulani.
Ndio maana nikauliza hakuna majina mengine mazuri? Yaani tumekosa ubunifu wa majina? Basi yapewe hata majina ya Wanyama
 
Back
Top Bottom