Dar es Salaam: Jiji lenye upungufu mkubwa wa Street lights

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,261
6,543
Mida ya Saa mbili usiku Jana Jumapili nikiwa na drive kurudi nyumbani mbagala toka ubungo niliamua nipitie njia ya katikati ya Jiji 'morogoro road' nikaunganisha akiba,posta mpya,Samora,Stesheni,Dawasco hadi Bp bandari kilwa road.

Nimeshangazwa kuona mji na hasa katikati ya ]iji pakikosa taa nadhani hii in aibu!Mbali ya barabara zinazopita mitaa ya posta mpya kituoni kuonesha kiwango duni/kuchoka pia maeneo hayo yanasaidiwa sana kumulikwa na taa chache za majengo.

Na cha ajabu hata majengo mengi yapo kizani tofauti na yanavyoonekana mchana hayana taa za nje!..hivi Leo hii sanamu ya askari ya Bismini round about ya Samora in Giza Giza,Kituo chetu Kikuu Tanzania cha Reli cha enzi na enzi kipo gizani!

Ni aibu hata kama unatembeza mgeni kutoka nje hata watalii waone hali hii inauma hasa kwa wachache tuloona miji ya wenzetu inavyowaka usiku kwa taa na marembo,hivi kweli mtaa wa Ohio ,Ifm ,Embassy hotel panakua Giza vile?City centre?tena ya jiji kuu la nchi?

Naomba wahusika waliangalie hili kwa kweli, halmashauri,Meya na pia mheshimiwa mkuu wa mkoa litazameni hili kwa uzito wake.maeneo ya Gymkhana ,Ohio zipo report za watu/Wageni kushambuliwa na kuporwa na vibaka...Giza inachangia haya matukio!
 
Sidhani kama Tanzania tuna cha kujivunia.

Miaka 60 hata mambo madogo yanatushinda kama haya.
 
Ahsante Kikwete.

Leo tuna uhodari wa kulalamika taa za barabarani hatuna.

Wakati unachukuwa Urais kutoka kwa Mkapa nchi nzima ilikuwa kiza. Tumeona juhudi zako kuanzia awali za kuutafuta umeme, ingawa hapo awali tu akina Lowassa wakakuangusha sana kwenye hilo lakini tunashukuru hukukata tamaa, umehakikisha kwa miaka yako 10 unawapatia umeme takriban 50% ya Watanzania wote na umehakikisha unatuwachia miradi ya umeme zaidi ya kututosheleza (over 100%) itapokamilika.

Tutakukumbuka sana Kikwete kwa record hiyo adhimu.

Sasa Magufuli sambaza taa za mjini.

Makonda, aibu jiji lako kuwa kiza. Umeme unao wa kutosha, taa tu zinakushinda? Tena siku hizi wala huhitaji taa za barabarani za umeme wa Tanesco. Zipo za solar.
 
Mnawekewa vibao vya alama za barabarani mnang'oa na kwenda kuuza chuma chakavu. Hizo taa za barabarani si mtaenda kufunga majumbani kwenu.
 
Waliotengeneza/kuirekebisha barabara ya uhuru haina taa hata moja na ukitembea usiku sidhani kama unaweza toka kariakoo na kifika karume salama lwa kifupi barabara ya uhuru haina taa.....
 
Mtoa mada tembelea Daraja la Kigamboni....ni pazuri saana na ni kivutio cha watalii na litaingiza pesa za kitalii saana.Hapo taa kwa mwendo kasi
 
Waende Iringa waone jinsi Taa za Barabarani zinazotuma Solar zinavyopendezesha mji.
 
Tusaidie kuokoa nauli na hela ya malazi naomba utuwekee picha.
Hiyo hapo, Sahani ya juu ndio inakama mwanga.
upload_2016-7-25_9-11-20.jpeg
 
Attachments

  • upload_2016-7-25_9-10-43.jpeg
    upload_2016-7-25_9-10-43.jpeg
    5.4 KB · Views: 42
Mnawekewa vibao vya alama za barabarani mnang'oa na kwenda kuuza chuma chakavu. Hizo taa za barabarani si mtaenda kufunga majumbani kwenu.
Katika hizi taa zilizopo nyumba gani zimefungwa..!?
 
Mida ya Saa mbili usiku Jana Jumapili nikiwa na drive kurudi nyumbani mbagala toka ubungo niliamua nipitie njia ya katikati ya Jiji 'morogoro road' nikaunganisha akiba,posta mpya,Samora,Stesheni,Dawasco hadi Bp bandari kilwa road.

Nimeshangazwa kuona mji na hasa katikati ya ]iji pakikosa taa nadhani hii in aibu!Mbali ya barabara zinazopita mitaa ya posta mpya kituoni kuonesha kiwango duni/kuchoka pia maeneo hayo yanasaidiwa sana kumulikwa na taa chache za majengo.

Na cha ajabu hata majengo mengi yapo kizani tofauti na yanavyoonekana mchana hayana taa za nje!..hivi Leo hii sanamu ya askari ya Bismini round about ya Samora in Giza Giza,Kituo chetu Kikuu Tanzania cha Reli cha enzi na enzi kipo gizani!

Ni aibu hata kama unatembeza mgeni kutoka nje hata watalii waone hali hii inauma hasa kwa wachache tuloona miji ya wenzetu inavyowaka usiku kwa taa na marembo,hivi kweli mtaa wa Ohio ,Ifm ,Embassy hotel panakua Giza vile?City centre?tena ya jiji kuu la nchi?

Naomba wahusika waliangalie hili kwa kweli, halmashauri,Meya na pia mheshimiwa mkuu wa mkoa litazameni hili kwa uzito wake.maeneo ya Gymkhana ,Ohio zipo report za watu/Wageni kushambuliwa na kuporwa na vibaka...Giza inachangia haya matukio!
Unalosema ni kweli kabisa. tena mi nadhani tu si aibu bali inafanya uendeshaji wa magari unakuwa mgumu sana. Siju hao ambao kwao kuna mataa marabarani wakiendesha DSM inakuwaje. Unguja kwa sasa yanawekwa mataa kwenye mitaa mbalimbali kwa kweli inafurahisha na kurahisisha uendeshaji wa magari usiku na faida nyingine za kuwepo kwa taa!
 
Back
Top Bottom