Loh. . . pole sana.
Mi najua huduma ya kwanza kabisa ni kufunga juu kidogo ya ulipogongwa ili sumu isisambae, au hata hiyo tu walishindwa?
Loh. . . pole sana.
Mi najua huduma ya kwanza kabisa ni kufunga juu kidogo ya ulipogongwa ili sumu isisambae, au hata hiyo tu walishindwa?
Yaani hata mimi nilishangaa sana zahanati kukosa huduma ndogo tu ya kuhudumia waliogongwa na nyoka.... Sijui wanaojeruhiwa na nge wanahudumiwa vipi!!pole sana mkuu....
Sasa wanashangaa nyoka tu, mbona huku kwetu 'new manzese' mabwepande, mlevi anaweza kuliwa na fisi makalio.
Labda aligongwa kwenye kiuno, wakashindwa wamfungeje.
Pole mhanga.
Heshima wakuu...
Mwenzenu jana nusura nife baada ya kugongwa na nyoka, maeneo ya huko Ubungo Maziwa. Ilikuwa ni mida ya jioni nikitoka katika mihangaiko ya kila siku. Baada ya kugongwa ilibidi niwahi katika zahanati zilizo jirani, lakini kila nilipoenda walikuwa wakinishangaa eti ni jambo la ajabu mtu kugongwa na nyoka Dar.
Zahanati ya mwisho nilipoenda manesi walipigwa na mshangao kabisa, eti wakitaka kujua ni wapi huko nilikokuwa hadi nigongwe na nyoka. Lakini kilichonishangaza zaidi ni kuwa zahanati tatu nilizopita hawakuwa na huduma ya kutoa kwa mtu aliyegongwa na nyoka. Ilibidi nikodi teksi inikimbize muhimbili ndiko nilipata huduma ya kwanza....
Hiki ndicho nilichokiona, maana zahanati moja nesi aliongea kwa mshangao "Dar nako kuna nyoka?? Nilidhani ni huko maporini mikoani tu?".....Nilitamani nimrukie nimpige vichwa, bahati yake maumivu yalinizidi.....pole sana. labda wanadhanini dr hakuna nyoka. wamejisahau
pole sana mkuu....
Sasa wanashangaa nyoka tu, mbona huku kwetu 'new manzese' mabwepande, mlevi anaweza kuliwa na fisi makalio.
Ha ha haaah!! hapana TIQO ilikuwa ni njia, na yule nyoka alikuwa anavuka nadhani alisikia vishindo na aliniona hivyo akajificha, nilivyofika jirani akanigonga kisha akakimbilia sehemu kulikuwa na mawe. alikuwa mkubwa mweusi.Ulikuwa unavizia mtu kwenye nyasi nini?
Labda aligongwa kwenye kiuno, wakashindwa wamfungeje.
Pole mhanga.
je ukidungwa kichwani,? Kamba utaifunga shingoni? Hatari sana
Unamaanisha nilitegeshewa??nimjuavyo nyoka mpaka akugonge either umemkanyaga au unatishia maisha yake, hapa dar nyoka wapo ila ni wapole sio wagongaji bali kuna wakutegeshewa ndo wamejaa