DAR: Askari Polisi wanne wauawa na raia 2 wajeruhiwa, silaha zaporwa!

mifumo yetu ya ulinzi ni mibovu mpaka kituo cha polisi kinavamiwa bila polisi kujua ni uzembe wa hali ya juu
 
Mungu azilaze roho zao mahal pema.Ni wakati wa kuwa macho hizi ni dalili mbaya mungu atunusuru
 
Hivi karibuni Rais wetu akiwa ktk mojawapo ya mikutano yake nafikiri alikuwa Mlimani UDSM,alitoa kauli hiyo tena kwa msisitizo.Ss nimeshangaa kuona majambazi ndo wameamua kuifanyia kazi kauli/agizo lake.Je ndo kusema wanamjaribu mkulu? ama wanataka kudhibitisha kwamba jeshi letu halijajipanga kikamilifu...
 
aliwaambia wawe majaji wahukumu coz haina haja ya mahakama.wadogozetu police wamejitolea kupana ili rais afurah
 
1: Mafuta ya Vaseline

2: Maji lita 2 kwa ajili ya kunawa uso.

3: Viatu vya michezo kwa ajili ya kutoka nduki.

4: Plasta kwa ajili ya kufunga majeraha madogo madogo.

5: Vijiti vidogo vidogo na kamba kwa ajili ya kuunga mifupa.

6: Nyumbani uage na kuandika wosia.

7: Pamba kwa ajili ya kuziba masikio usisikie milio ya bunduki.

8: Ule chakula chepesi usishindilie ugali ili uwe mwepesi kukimbia.

9: Bendera ya Yanga maana jamaa watakuwa na bendera ya Simba.

10: Ongezea wewe.....
 

Attachments

  • 1472038231830.jpg
    1472038231830.jpg
    15.2 KB · Views: 36
Mkuu, kama jamii tuna tatizo baya sana vichwani mwetu zinazotokana na political inclinations. Kuna watu humu jamvini wanashabikia watu kuvunjwa viuno na nyonga na kuuliwa kwa ajili ya maandamano na mikutano ambayo ni haki yao kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi. Wamefikia kiwango cha kuwataka eti fulani na fulani watangulie mbele ya maandamano wakiwa na familia zao ili wavunjwe viuno ama kuuawa kabisa. Huu ni ukosefu wa busara na utu. Mimi nilidhani watu hao wangepaswa kutoshabikia umwagaji damu, na wangesisitiza umuhimu wa amani, na kutafuta suluhu za mtafaruku kwa njia ya amani; jambo ambalo kama taifa tumewahi kuheshimiwa sana huko nyuma. Kinachoendelea hivi sasa ni udhihirisho wa mgawanyiko wa kijamii kiitikadi. Wanaoona wanakandamizwa kinyume cha sheria wanapata mahali pa kupumulia kama kwenye tukio kama hili. Na wale wanaoshabikia state violence dhidi ya madai ya haki za kikatiba na kisheria kwa kundi lingine ndio wanaolaani kwa jazba kitendo hiki wakikiona kuwa si cha kiutu, lakini cha kuvunja viuno vya wadai haki za kikatiba na kidemokrasia nihalali kwao.

Vyovyote vile, mauaji ya Polisi hayakubaliki, na ni jinai kama jinai zinginezo. Jamii zilizostaarabika haziwezi kukubaliana na mambo maovu ya kiwango hiki. Vivyo hivyo, na hao pro state violence wajaliwe kuona kwamba amani ya nchi ni tunda la haki yaani kuheshimika kwa katiba kama msingi mkuu wa utawala wa jamii yetu. Yaliyo ndani ya katiba yaheshimike kama yalivyo, na yaliyo nje ya katiba yapingwe na yashugulikiwe kwa mujibu wa sheria za nchi. Binafsi sipendi matumizi ya nguvu yasiyo ya lazima kwa vitu ambavyo busara, hekima na maongezi ya kawaida kabisa yangeliweza kutatua tatizo.
Umenena vyema sana mkuu,lakini ni nani wa kukusikiliza?
 
*Hii inatoa picha sio nzuri*
Tokea lile tukio la uvamizi wa bank ya crdb huko mbade na nchi yetu kupoteza askari kadhaa katika tukio hilo,nimekuwa nikiona katika mitandao ya kijamii na hata mitaani watanzania wenye akili zilizopoteza utu na ubinadamu wakipongeza tukio hilo lililopoteza binadamu wenzetu wakiwa kazini.
Hilo jambo limenitisha na kunishtua sana!kwa kuwa hili ni jambo jipya kwa tanzania kujitokeza.Bila shaka kuna jambo la kujifunza kama nchi au taifa kwa nini tumefikia hatua hii ya kupoteza roho ya utu.
Polisi ni binadamu kama mimi na wewe na isitoshe ameapa kulinda raia na mali zao,pia ni ndugu zetu kwa kuwa nao wamezaliwa na mama kama mimi na wewe,tumefika mahala mtu analinganisha picha ya mazoezi na maiti yenye damu kwa nia ya kupongeza kufa kwa binadamu mwenzake!!hii ni hatari ambayo inaanza kuota katika bongo zetu.
Hali hii kama taifa tunatakiwa tusiipuuze hata kidogo,tujiulize wenyewe tatizo hili linatokea wapi ili tulidhibiti na tanzania iendelee kuwa mahala salama pa kuishi.
Watanzania tuliishi kwa upendo bila kujali dini,kabila wala kazi ya mtu lakini leo tunafika mahala kufurahia msiba!hii haiko sawa hata kidogo.
Nawashauri walio na mamlaka waangalie upya mfumo wa kushughulikia masuala yahusuyo jamii ili kujihami na msingi huu wa chuki unaojengeka taratibu vichwani mwa watanzania wachache baadae watakuwa wengi na hapo ndipo uwezo wa kudhibiti utakapokwama.
Nawashauri watanzania wenzangu turejee katika utu na ubinadamu wetu wa awali bila kuzijenga akili zetu kwa chuki na tusije kuviachia vizazi vijavyo urithi wa damu.
Naipenda Tanzania na mungu tuepushe na hili balaa.

Oscar Pius
 
Kwa sababu walijuwa ni movie ya Mwigulu na Sirro haijiongezi kabisa pole kwa Vijana wetu kupotezwa kwa ajili ya watu kuweza kupata vyeo
 
Polis siku hizi wamegeuka kuwa aduhi wa raia na Mali zao badala ya kuwa rafiki wa raia, ndo maana watu wanashangilia matukio Kama hayo, ukiangalia siku zote za maisha yako polis hajawahi kukusaidi lolote zaidi ya kukunyang'anya kidogo ulicho nacho sasa utamfurahia kwa lipi?
 
Haya yanatokana na uhusiano usiomzuri kati ya raia na Polisi, sio jambo jema kbs ila hii chuki imejengwa na wao wenyewe kupitia wanasiasa na siasa yenyewe.
s
Kosa kubwa, lililofanyika waliomzunguka hawako tayari kumwambia ukweli kua "alipata kura" kidogo. Sana sana, wanaishia kumwambia hawa ni vijana wate wa IT. Wakijitahidi wanasema tulikua nao wote kipindi cha uchaguzi. Full stop.
Very cheap position by Juliana sijui nani, who does she think she is, eti yeye anatujua chuki zetu kwa mani? hili ndio tatizo la awamu ya 4 ya JK kuwadanganya hawa warembo uchwala kwamba they are the most intelligent young kids simply because they could be used like toilet papers. Listen to her, unawajua wakina mani, and who are you to communicate your position. Sisi sio wanafiki tunajadili situation napa hatutafuti u DC wala upambe kwenye timu so and so, we are above that. We are saying the truth that mkulu hana strategy na approach yake ni poor. hatuzunguzii hawa na wale hapa Tanzania ni yetu sote sio yenu na wao wanaowatumia. Kimenuka sasa wanoawatumia hawa uwezo wa kuwalinda any more, the reality is that you are totally exposed na mnashughulikiwa sasa kwa kuwa watu wametokwa na huruma. Hivi utamhurumiaje mjeshi anayewavunja watu miguu, tena vijana kama wewe kwa vile tu, si waumini wa chama chako cha CCM (baba wa kambo).
 
s

Very cheap position by Juliana sijui nani, who does she think she is, eti yeye anatujua chuki zetu kwa mani? hili ndio tatizo la awamu ya 4 ya JK kuwadanganya hawa warembo uchwala kwamba they are the most intelligent young kids simply because they could be used like toilet papers. Listen to her, unawajua wakina mani, and who are you to communicate your position. Sisi sio wanafiki tunajadili situation napa hatutafuti u DC wala upambe kwenye timu so and so, we are above that. We are saying the truth that mkulu hana strategy na approach yake ni poor. hatuzunguzii hawa na wale hapa Tanzania ni yetu sote sio yenu na wao wanaowatumia. Kimenuka sasa wanoawatumia hawa uwezo wa kuwalinda any more, the reality is that you are totally exposed na mnashughulikiwa sasa kwa kuwa watu wametokwa na huruma. Hivi utamhurumiaje mjeshi anayewavunja watu miguu, tena vijana kama wewe kwa vile tu, si waumini wa chama chako cha CCM (baba wa kambo).
wameshikwa hofu na woga wanachora movie wakidhani public itasympathise nao ndio kwanza vicheko na cherekocheroko li strategy lao limebuma kwa kweli they have small brain
 
Back
Top Bottom