DAR: Askari Polisi wanne wauawa na raia 2 wajeruhiwa, silaha zaporwa!

Ninahisi kuna mambo matatu hayaendi vizuri katika mfumo wa jeshi la polisi na kutokea utendaji wenye mashaka. Mosi idara ya upelelezi nahisi inapwaya. Sijawahi sikia mara nyingi polisi kutibua mipango ya uharifu. Ni taarifa za mapambano na mauaji. Ukiua jambazi umekosa nafasi ya kupata mtandao wao. Mti kata mizizi, si matawi. Pili napata picha kama mahusiano ya raia na polisi panajengwa ukuta wa zege, yakiwa ni matokeo ya hisia kuwa polisi hawatendi haki na kufuata sheria wakati wa kazi zao. Na tatu ni muda mrefu sasa mafunzo na wanafunzi waingiao chuo cha polisi vimekuwa vikitiliwa shaka. Tusiwe wepesi wa kutoa pole na kuandaa mazishi ya heshima kwa maaskari wetu. Bora kukinga kuliko kutibu.
 
Kwani polisi wetu wakibadilishana lindo, huwa umakini wao hupungua? Au nitukio kama matukio mengine.
Tahadhari ya Kamanda kuwa kila ''askari akija kwako aoneshe kitambulisho nimeipenda"
 
polisimiezi sita haitoshi wanakuwa hawajaiva, mijambazi inakaa polini kama savimbi ina mazoezi ya kutosha wengi wao waheasi jeshi
 
Kwani polisi wetu wakibadilishana lindo, huwa umakini wao hupungua? Au nitukio kama matukio mengine.
Tahadhari ya Kamanda kuwa kila ''askari akija kwako aoneshe kitambulisho nimeipenda"
polisi wengi hawana vitambulisho,sijui kama itawezekana katika utendaji wao.
 
shida ya vyombo vyetu vya dola ni kutoa matamko ya kututoa wasiwasi raia kuwa amani ipo wakati dalili zinaonyesha hali inaweza kuwa mbaya huko mbeleni
 
Tatizo jeshi letu la polisi limekuwa likichanganya siasa katika utendaji wake,thus why wananchi hawalipendi.
Hii inapelekea watu washangilie hata vifo vya askari.
Ni lazima polisi wajiulize wapi wamekosea.
Na,je raia wakipata silaha kwa wingi polisi watahimili??
Binafsi sifurahishwi na utendaji wa polisi kwa sasa,i hate them!!


The Hyper;
To hate others si kimungu hata kidogo. Nadhani ungewaomba wajipime kwa matukio kama haya. Alivyouliwa huyu askari mdogo ndivyo pia aweza uliwa huyo mkuu.
Huenda ni "Sniper" aliifanya kazi hiyo kwa zile silaha zetu zilizoibwa sehemu sehemu, sasa wanawarudi. Hivyo, hii ni barua tosha kwa polisi kuwa; Hampo salama. Hivyo, wajipime tu wameharibu wapi uhusiano. Vinginevyo, who knows the next victim??
Lakini, Do not hate your neighbor.
 
Polisi wanajenga taswira mbaya sana mbele ya jamii.tutegemee matukio mengi ya aina hii kwa siku za mbeleni

Dah kwel kabisa! Mambo mengi wanayoyafanya hawa FFU toka kipindi kile cha mtu akigoma "APIGWE TU" yanatia hasira, hawajui kuwa wanajenga chuk ht na raia wa kawaida ukiacha majambazi. Wakikamata mtu wanapiga km kiroba!
 
rest in peace askari wetu,unyama wa namna hii haukubaliki popote pale.pumzikeni kwa amani makamanda.
 
Kwani mazoezi yamekwisha? Si nilisikia askari wanafanya mazoezi ya ukuta sasa umebomoka au kumebomoka kwingine. Yule wa juzi alimtaja mtume.
 
Ni makosa makubwa kuua wasimamizi wa amani katika jamii.
aisee police wanne??? Ni hatari hii yaan kwa police wanne kuuwawa kwa mara moja ni hasara kubwa sana kwa taifa tunaomba serikali ifanye msako mkali sana katika hili kwakweli.
 
Katika Mkutano wa leo wa Jeshi la Polisi na Waandishi wa Habari kuhusiana na mauaji ya askari Polisi yaliyofanyika jana,ningependa kujua kamaa waandishi walipewa fursa ya kuuliza maswali na kama walipewa nafasi ningependa pia kujua waliuliza maswali gani.
 
Back
Top Bottom