Wakuu-
Nadhani niseme hili kwa ukweli kabisa na bila kuungaunga maneno.
CHADEMA/CDM hawajipanga kabisa kwa ajili ya uchaguzi huu. Nadhani bado wako kwenye ile excitement au furaha ya Lowasa na imani kuwa watashinda uchaguzi wakiwa naye. Mwenendo wao unatia shaka kama kweli hiki ni chama kinachotaka kwenda ikulu. Hii ni wiki sasa inapita na CDM hawajaanza kampeni. Haiwezekana eti unapanga kampeni zako zianze wiki moja baada ya filimbi kulia. Kwangu mimi hii nikukosa mbinu. Ukipita mitaani hamna poster hata moja ya mgombea Urais wa CDM au wabunge na hata madiwani wao. Hii ni dalili mbaya na inaonyesha kushindwa na kutokuwa na mipango. Kuhusu kiwanja cha Jangwani kuzuiwa, chama makini lazima kiwe na PLAN B na sio kungangania sehemu moja. Kwanini wasiende kuzindua campaign sehemu nyingine? CDM wanakubalika Mbeya Mjini, Moshi Mjini, Arusha Mjini- kwanini wasiende huko? Sasa Imani yenu kuwa CCM imechokwa kila sehemu mbona haiwapi confidence yakuenda sehemu zingine? Nchi yetu ni kubwa sana, huwezi kupiga siasa Dar halafu ukadhani umeshinda uchaguzi. Jamani kati ya watu milioni 24 waliojiandikisha DAR ni watu 2.8 milioni tu. Elekezeni akili zenu kwenye HESABU HIZI si kuwa na maneno, maneno ambayo hayana tija.
Kupambana na CCM kunahitaji mbinu na maarifaa sio maneno matupu. Angalia CCM walivyokuwa organised. Myonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Hili halina ubishi. Angalia nyomi ya Magufuli kila sehemu anayoenda. Hii yote inaonyesha hawa watu wamejipanga. Hata mkibisha CCM bado inapendwa. Kama inachukiwa ni sehemu za mjini tu, ambazo kihesabu zinaweza zisiwe na maana sana kulinganishwa na huko kwingine.
Haiwezekani campaign za chama ziwe zinamzunguka mtu mmoja. Chama ni taasisi na si mtu. Na hilo ndilo naliona kwa CDM. Yaani kila kitu ni Lowasa. Viongozi wao wanatakiwa wawajibike. Bado sijaona nia hasa ya kuingia ikulu zaidi ya makelele ya mabadiliko ambayo hayana vitendo vya kusambaza hilo kwa wananchi. Makelele pekee hayawezi kushinda uchaguzi. Acheni kuchanganyikiwa na anzeni mipango sasa ili tuwe na opposition yenye nguvu bungeni. CHADEMA KUWENI NA PLAN B KILA WAKATI.