Dalili mbaya za kushindwa kwa ukawa/chadema

Dalili mbaya za kushindwa kwa ukawa/chadema

KATIKA ufunguzi wa Kampeni za CCM, Leo tarehe 23_August 2015, viwanja vya Jangwani jijini, ile ISHARA KUBWA YA KIFO CHA CCM IMETIMIA.

Katika ufunguzi huo ambao kwa namna isiyo ya kawaida watoto wote wa awamu za CCM walikutana, tukianza na Makongoro anawakilisha awamu ya kwanza (badala ya marehemu baba yake Mwl Nyerere), kisha alikuwepo Mwinyi mwakilishi Wa awamu ya pili lakini pia alikuwepo Mkapa Wa awamu ya Tatu na Jk anayemalizia. CCM Nzimanzima ilitimia na wasimamizi Wa awamu zake zote.

IPO ISHARA moja tumeiishi tukiiamini kwenye maisha ya binaadam kwamba ikitokea ndani ya mwaka mmoja kwa watoto wa familia moja kwa pamoja mkakutana nyumbani kumwona mzazi, basi mjue mzee wenu huyo mwaka huo lazima aitwe na Mola.

Maisha yangu yote nimekuwa nikichunguza na kuchambua ISHARA HII. Nilicho gundua ni kweli. Kila MTU ukimuuliza mzazi wake alivyo fariki atakujibu "ah Tena Bahati tu nilikwenda msabahi kabla hajafa" Hii ni ISHARA ambayo haikwepeki, utakuta automatic mnakutana kumwona mzee wenu na soon anarudisha tarakimu zake.

Hata safari zenyewe za kumwona Mzee wenu huwa za ajabu au kushtukiza au inatokea tu kijisababu kinakufanya at that time uwe home.

Mfano mzuri ni Mkapa, hakuwa na mpango kabisa Wa kuhudhuria ufunguzi Wa kampeni. Walitaka wamweke kwenye timu ya kampeni akakataa. Mwenyezi Mungu akaona ili aiangushe CCM lazima kanuni za ishara zitimie, akatengeneza Tukio, waziri wake mkuu, yule mpinzani Wa Lowassa, aliyesema CCM wakimpitisha lowassa atazunguka nchi nzima kumpinga, Mwenyezi Mungu akaanza nae, akamfungua macho Sumaye, akaona ukweli kwamba sababu zote walizompaka matope Lowassa si za kweli, na kwa kasi ya ajabu akakunja kona na kuingia ukawa.

Baada ya tukio hilo likamchimbua Mkapa, akafura na kuvamia jangwani akimpitia na Mwinyi kwa staili ya kuongeza nguvu kumbe ni Mpango Wa Mungu aiangushe CCM.

Mfano Mwingine ni Makongoro. Makongoro ambaye yuko against na familia yake na jamaa za Nyumba ya babake yeye peke yake ndiye anayejihusisha na CCM ili ale. Mapigo mawili yaani lile la kutupwa nje kabisa kwenye utia nia Wa urais ndani ya CCM na lile la kuondolewa na kutupwa tena hata kwenye Ubunge KAWE vingetosha kumuathiri na kuketi kando na CCM na kuungana na fimilia yake.

Lakini Mwenyezi Mungu bado akamtaka ili atimize ishara siku ya Leo, akamfanya achaguliwe kwenye timu ya kampeni tena kamati ya hela na kuahidiwa ubunge kwenye nafasi kumi za prezda. Kwa matofali hayo jamaa akabakia chamani hadi Leo alipo fanyika nguzo muhimu kutimiza ishara ya kifo.

The Very same to CCM, WATOTO WOTE WA CCM WA AWAMU ZOTE NNE KWA MPIGO WAMEKUTANA KWA MZEE WAO CCM. Wanadhani wamekwenda kwa tukio, au kutia nguvu, au kufanya kampeni kumbe wameitwa maksudi na nguvu ambazo hata wao hawawezi kuzicontrol ili protokali za elimination cycle zitimie na zimetimia.

Hii ni kanuni kubwa sana ya nguvu za maisha. Hakuna linalo weza kufanyika kuokoa CCM baada ya ishara Hii kutimia.

Mtaona ishara zaidi kuanzia Leo, CCM itaanza na kuzidi kudhoofu. Wataanza kutukanana na kusalitiana wenyewe kwa wenyewe. Mtaona na kuamini kwamba ISHARA HII HAIKOSEI.
Ni wajinga tu ambao huenda vitani bila kusoma majira na nyakati za ishara. Zamani wafalme wenye akili wakitaka kwenda vitani walingojea ishara kwanza kutoka kwa nabii. Hakuna mwenye akili aliye thubutu kwenda vitani pasipo subira ya ishara kutoka kwa nabii.

Manabii walikuwa na namna yao ya kusoma ishara za Mwenyezi Mungu. Nabii akiona ishara flani ndipo anamstua mfalme aende vitani na asipoona ishara anamwambia live mfalme kwamba ishara hajaona amavipi aende vitani tu hivyo hivyo kwa risk zake. Na kila mfalme aliyediriki kwenda vitani kwa ubabe wake au ujuzi wake Wa vita au kiburi cha wingi Wa jeshi lake alinyukwa vibaya na kufia vitani. Wadau wa mambo ya dini wanajua sana mambo hizi.

Wafalme wenye akili, hatakama wana jeshi na nguvu kiasi gani, hawawezi kuthubutu kwenda vitani pasipo Ishara. Mamburura, wapuuzi na wajinga ndio huenda kichwakichwa wakafyekwa.

Ushindi Wa chochote huasisiwa na Mwenyezi Mungu, Na Mungu akisha panga kitu chake zipo ishara zitaonekana tu.

Mimi si shabiki wala mfuasi Wa CCM, ni mfuasi Wa mabadiliko. Lakini asilani siandiki haya kwa mvuto wa utashi Wa mapenzi yangu kwenye mabadiliko lakini ni devine fact ambazo ziko hivyo wala sio utashi wangu kuzibadili.

Asilimia zaidi ya 82 ya watanzania wanataka mabadiliko. Lakini nikawa najiuliza bado CCM Inaweza kung'ang'ania kubakia madarakani ama kimabavu, wizi au matumizi mabaya ya vyombo vya Dola. Hivyo mbali na wananchi kutaka mabadiliko lakini CCM wanaweza kudiriki kumwaga maelfu ya Damu ili wabakie madarakani. Hofu Hii nilikuwa Nayo na nadhani watu wengi walikuwa na hofu kama Hii. Lakini baada ya Ishara Hii, CCM haipo. Hakuna umwagaji damu wala nini. CCM HAIPO TENA. MABADILIKO HAYA KUNA MKONO WA MWENYEZI MUNGU. NANI ANAYE WEZA KUSHINDANA NA Mungu?!
 
Malalamiko punguzeni kila kukicha nyie na media wao hawapigi kura na wachache wanaosoma na kuangalia.kura ziko vijijini .kura za mjini haziwapeleki ikulu .na hesabu hazidanganyi .dr.magufuli anakata mbuga leo hii kesha fika kwenye ngome yenu mbeya ananadi ilani na sera za chama chake, nyie mnabaki kulalama haitawasaidia ua ndiyo ile slogani yenu ya ufisadi/mfumo imekufa.dr. Anaelezea nini atakifanya mabadiliko yaja kuonyesha hizo slogan zenu ccm itavyofanya kazi chini ya magufuli kwani ni chama cha mapinduzi kilivyoasisiwa
 
Hiyo sio lugha wala style ya UKAWA. . . . .,Ngoja waje utajua
 
Kuna mambo ya msingi umeonge
Ila hilo la mgufuli kampeni na ahadi zake naona kama anachemka hivi, naona ni kama mtu hana malengo, ana kiwewe, ile papara ya pale jagwani naona inaendelea, magufuli apunguze spidi na atulize kichwa chini la sivyo atachoka mapema sana, na safari baada ya dakika 90 kuna 30 za nyongeza, maana naona ashajifunga tayari..
ukawa usisahau kulinda kura tume ya ccm isije ikawaliza
 
nyinyi vijana mliopangishiwa nyumba kama wake wenza na january kazi yenu kubwa ni kurushia makombora ukawa na kuichafua ikifika tr 25 mtafte makazi
 
Mugisher

Wewe ni ccm,hiyo habari ya cdm kushindwa mbona ndio furaha kwako,vinginevyo utakuwa umeamua kuja ki umbea umbea
 
Last edited by a moderator:
OK. unaweza kuwa na point Fulani, sasa sielewi kama unayo macho na masikio juu ya rough za ccm dola kutumia dola zake kuzuia kila aina ya jitihada za UKAWA kufungua kampeni na kuziendeha.
Naona mmepata sababu ya kuhalalisha kushindwa kwenu kuweka mikakati ya kukabiliana na nguvu ya chama Dola. Mlijua kuwa mnapambana na chama dola ambacho kitatumia mbinu safi na chafu kubaki maarakanina walisawaambia kuwawataunga hata GOLI LA MKONO. Je nyinyi mlijipanga vipi au maneno ya Mzee Mkapa kuhusu nyie yana ukweli?
 
#Kawembe huwa hufikirii halafu pia hutumii busara katika kutatua matatizo. Nchi hii usipokuwa makini ni sawa na mtoto asiyena uwezo wa kumhama mama yake mkatili. MANENO MATAMU YA MAGUFULI HAYABADILI MFUMO WA CCM. MAGUFULI HANA UZOEFU NA CHAMA SO ATAENDELEA KUBURUTWA NA SYSTEM YA CHAMA

Mkuu huo ndio ukweli ulivyo lkn kwa pro ccm hawataki kuukubali ukweli huo,sote ni mashahidi leo hii magufuri anaahidi kuboresha elimu,kwa miaka 54 ya chama tawala madarakani eti bado wanaahidi?walishindwa nini kufanya hivyo miaka yoote?watanzania tusikubali kabisa kudanganywa tena.
 
Katika kuzunguka kwangu nimegundua kitu kimoja kuwa yale maeneo yasioikubali au kuikumbatia ccm ndio yenye maendeleo compared na yale yanayoongozwa na ccm miaka yote. Ndio maana naamini walio mbele kwa maendeleo wana uwezo mzuri wa kufikiri kuliko zile sehemu zisizo na maendeleo. Mfano Angalia Mbeya, Arusha, Mwanza, Iringa na hata Dar es salaam angalia Kawe na Ubungo then fananisha na Temeke na Ilala. Sizungumzii magjorofa nazungumzia standard life of living.
 
Ukimsikiliza mtu anayeiamini ccm au anayeishabikia utagundua pia kwa nini wanadamu watachomwa Jahannam
 
Msikae Jf kuaminisha wanasoma habari zenu.Hakuna kusubiri hapa Tuelezeni SERA NA ILANI YENU TUZIPIME NA WENGINEO MNAVYOCHELEWA DR. MAGUFULI NDIO AMESHAWAPIGA BAO ENDELEENI KULALAMIKA NYIE HAMUAMINIKI KIZUNGUMKUTI!!!
 
Hata hapa tu umeshaipigia kampeni, katika mikutano saba ya magufuli minne ameongelea sana UKAWA so hata nyie mnaitangaza, ndo maana unaona kampeni.hazijaanza.kwa kuwa tamasha.la fiesta limeshindwa kuacha kumbukumbu kwenye vichwa vya watu.....
 
Coz kama nchi hii ilipo hapa na haliza za watanzania zilivyo lakini mtu bado anashabia Tz kweli mtaji wa ccm ni ujinga wa watanzania
 
Mugisher

Well said..

Wadhamini wamegoma kuwapa pesa za kampeni ndo wapo wanajichanga
Mzee sabodo na mtei wamesema hawezinkumdhamini mtu kutoka ccm wanajua ameenda tu kuwapumbaza kiin macho lowasa ni ccm pure brother
Yan ni sawa na mkristo aliebatizwa kwenda uislam.
 
Last edited by a moderator:
Coz kwa nchi ilivyo sasa na hali za watanzania zilivyo mbaya kiuchumi lakini bado mtu anaishabikia ccm? kweli mtaji wa ccm ni ujinga wa Watanzania
 
Kwani Kampeni Zimeanza? Mbona Sijaona Chama Chochote Kikipiga Kampeni Huku Kwetu Zaidi Ya Kusikia Jina La Lowassa Likitamba Mtaani.
 
Ya ukawa yanakuhusu nn ww unafikir kutangulia ndio kushinda usijidanganye media zipo hata campaign kwenye media zinapigwa tu vile vile mtu mmoja mmoja tu subir kimbunga kinakuja na huwa kinaanza taratibu baadae kinaezua kila kitu tulia naona una hofu sana ya kushindwa ww.
 
Back
Top Bottom