Uzuri ni kwamba hizo ni dalili za huko kwaoMara nyingi tunapojadili habari za sayansi giza... Lawama zote kejeli hata matusi hutupiwa mtu mweusi anayeonekana kukumbatia mila zisizo na faida wala ithibati...
Nimejaribu kuwaelimisha wengi kuwa habari za sayansi giza haziko Afrika tu bali duniani kote
Hapa leo kuna dalili kumi ambazo jamii nyingine nje ya Afrika zinaamini kwamba ukikutana nazo basi tambua kifo chako hakiko mbali... Hizi ni imani na sayansi giza za mapokeo... Inawezekana kabisa kwa sasa jamii husika haiziamini wala kuzishika sana lakini bado wanazo kwenye makabrasha yao... Hebu twende moja baada ya nyingine
1. England: huko wenyeji wake waliamini kuwa mbwa akilia usiku kucha nje ya nyumba yako bila sababu basi kuna uwezekano mkubwa mwanafamilia akafa kesho yake
2. Ndege wakichezacheza na kurukaruka nje ya dirisha lako huku wanatoa sauti kama za maombolezo au vilio
3.Roma: uko nyumbani pekeyako ama na wanafamilia, ukiwa wa kwanza kuangalia saa na kukutana na mshale wa saa zile za ukutani ndio umegota( jam) yaani hausogei mbele lakini sauti ya tok!tok! tok. Basi ukiweza aga kabisa maana kuliona giza la siku ya pili inaweza kuwa kwa kudra tuu
4.America ya Kusini : Unapomuona kipepeo mweupe anarukaruka ndani ya nyumba yako na baadae kutokomea kusikojulikana... Tambua wazi huyo ni mjumbe wa kifo na kaja kukupa taarifa rasmi ya kwamba kesho wewe ndio safari...
5. Maryland : Kwa imani za watu wa huko... Mende akipanda kiatu chako... Wewe siku zako za Kuishi hapa duniani na kula bata zimekwisha... Kifuatacho ni maandalizi tu ili usife na madeni ya watu...
6. Ulaya: Ukimuona mwanamke aliyepauka uso na kusawajika.... Ndugu yangu omba Pooh tu hasa akikushika mkono usalimiane naye... Kama ulikuwa hujala cha mwisho fanya hivyo haraka
7. India : ukiwa uko sebuleni ama chumbani na picha yako ukutani ikaanguka yenyewe mbele yako... Huna haja ya kuwaza yajayo tena... Kuna uwezekano mkubwa kabisa usifikishe masaa 48
8. Irish : Imani zao za kishirikina zinasema kuwa Kama uko katikati ya picha ya watu watatu na bila sababu ukakutana nayo... Kifuatacho ni kutandika tanga... Kwakuwa Kama ukipona basi tambua kuna muujiza umekuokoa
9: Japan : hakuna kitu kibaya na cha kuogopwa kule kama ukiwa umeshika kioo kisha kikakuponyoka na kuanguka chini na kuvunjika kikiwa na taswira yako kabla hakijaanguka... Ukizidisha sana maisha ni masaa 15......
10: Ugiriki ya zamani: Imani yao kwenye ushirika na mambo ya giza wanaamini ya kwamba ukiponyokwa na mwamvuli uliofunguliwa ndani ya nyumba... Tambua umeponyokwa na roho... Hapo huna maisha tena... Muda mchache ujao utakuwa na jina la marehemu.... Yaaani unakuwa marehemu mtarajiwa....
Inawezekana kabisa mojawapo kati ya haya yalishawahi kukutokea lakini hukuwahi kuogopa wala kuwaza kifo na mpaka leo uko hai.. Jeff yangewatokea wenye imani zao?
Hapa kwetu Afrika bundi kulia nje ya nyumba yako ni dalili mbaya za kifo hasa kama kuna mgonjwa ndani ya nyumba yako (kisayansi hili limethibitishwa kuwa bundi huwa na uwezo wa kunusa kifo kwa mgonjwa) lakini kwa wenzetu wachina ni bahati kubwa bundi kulia nje ya nyumba hasa asubuhi
Hitimisho
Mwisho wa siku imani inabaki kuwa imani (japo imani huzaa roho) kwahiyo si lazima unachoamini wewe kifanye kazi kwangu.... Perception creates reality!!!!!
Dalili ninazo kama nne kati ya hizo hivyo nisipoonekana mdogo wangu waeleze wote kuwa nilikuwepo ila nimeondoka.[emoji15][emoji15][emoji848][emoji848][emoji26][emoji26][emoji26][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144]
Kwani kifo kina mahali ulipo au ni popote?Uzuri ni kwamba hizo ni dalili za huko kwao
[emoji15][emoji848][emoji25][emoji25][emoji25][emoji25][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144]Dalili ninazo kama nne kati ya hizo hivyo nisipoonekana mdogo wangu waeleze wote kuwa nilikuwepo ila nimeondoka.
Kumbukeni mwisho wa Dunia ndo siku ya mauti yako hakuna mwisho mwingine zaidi ya hapo!! Tuishi tukitambua kuwa hapa Duniani tunapita tu sio mahala pa kudumu!! Ahsanten na Mwenyezi Mungu awabariki na kuwajaalia roho za kutenda mema daima popote mlipo na muendako [emoji115][emoji115][emoji115][emoji115][emoji115][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]Jaman KIFO HAKINA BAUNSA so hakuna anayeweza kukingia kifo Ila ninachoamini wote tutarudi mavumbini na haijulikani siku wala saa wala dakika wala sekunde lakini tutaondoka tuuu!! Kinachoniuma zaidi nikuwa huko tunapokwenda hatujui tunaenda kupokelewa na nani maana hanasa za dunia zimekuwa nyingi balaa ukitubu tu huchukui hata masaa tayari umeshafanya anasa tena Ila kikubwa ni kuishi vizuri na watu na kufanya japo machache yanampendeza muumba wote....
Muumba watu najua hachoki kutusameheehhe hivyo usisubirie mpaka uwe kitandani maututi ndo uanze kutafuta msamaha jitahidi angalau kabla hujalala basi unasema tu maneno haya MWENYEZI MUNGU ASANTE KWA KUNIWEKA HAI MPAKA DAKIKA HII, NISAMEHE DHAMBI ZANGU NILIZOTENDA IWE KWA KUTAZAMA KWA MACHO, KUTAMKA KWA KINYWA CHANGU , LAKINI PIA UNILINDE MUDA HUU NAPOENDA KUMPUMZIKA NA NIAMKE SALAMA...AMEN
Kumbukeni mwisho wa Dunia ndo siku ya mauti yako hakuna mwisho mwingine zaidi ya hapo!! Tuishi tukitambua kuwa hapa Duniani tunapita tu sio mahala pa kudumu!! Ahsanten na Mwenyezi Mungu awabariki na kuwajaalia roho za kutenda mema daima popote mlipo na muendako
Jibu la ilo swali nazani utakuwa nalo ila ninachojua kuwa IMANI huwa zinatofautiana kwa mtu ma mtu hata sehem na sehemKwani kifo kina mahali ulipo au ni popote?
[emoji15][emoji15][emoji15][emoji26][emoji26][emoji26][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]Yaani nkifutiliaga nyuzi za huyu kikongwe nakumbuka mashart niliokuwa napewa home na wazee, kuwa marufuku kula maini utakuwa mwepesi, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji961]
Nina miezi takribani sita iyo namba mbili nasikia sana vindege asubuh vinakwaruza kioo dirishani kwangu na vinapiga kelele.... Kwaiyo nitakufa soon? Mshindwe
[emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]coincedence? Imani huzaa roho!? [emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144]nadhani kuna ukweli kumhusu bundiSiku moja tulitoka sehemu na rafiki yangu, kufika njiani tukaona bundi kasimama njiani ikabidi tusimamishe gari yule bundi akakimbia kesho yake kulipokucha nikapata taarifa ndugu yake na yule rafiki yangu amefariki kwa ajali ule ule usiku tulioona bundi.