Dalali akichukua pesa zaidi yako utakubali

Dalali akichukua pesa zaidi yako utakubali

Ili kujiondoa kwenye huo mtihani Dalali ataambiwa kwa makaratasi Bei ambayo ninataka na yeye atakula 10%.. Mfano nitasema nyumba yangu iende kwa 20M na dalali utapata 10%

Pili nitaongeza Term nyingine kwamba katika ongezeko la zaid ya 20M dalali atakula 30% kwenye kiasi ambacho kimeongezeka kwenye Bei Halisi(20M)

Hapo Alete hata mteja wa 500M ni yeye tu.. Fair and Square
 
Haya hapa unakuwa uko sahihi so hata akikubali anakuwa kakubali kwa makubaliano.sio umwambie tu nataka mil 10 akileta mteja wa mil 60 uanze nongwa.
 
Acha tamaa,zingatia makubaliano.

Na hapo kwenye hiyo 10 yako itabidi umpe na chake Cha udalali .
Mkuu umetoa jibu la mtu ambaye hajafanya biashara ya aina hiyo na asiyejua lolote kuhusu.

Dalali ni taaluma, ni ofisi na ni mshauri wa mwemye mali.

Kwa hiyo hawezi kuuza nyumba kimaghumashi nje ya utaratibu wa kiofisi na kisheria pamoja na makubaliano ya kazi.

Wewe unapouza nyumba unapanga bei yako, unapomtafuta dalali ataiangalia kisha atafanya tathimini kutokana na hali ya soko la kijiografia na kutoa ushauri kwa mwenye mali.

Mwenye mali kabla ya kutoa 'go ahead' watakubaliana na dalali malipo yake kutokana na % fulani ya malipo yatakayopatikana kutokana na mauzo ya mali.

Kwa hiyo let say kama nyumba ilikuwa inauzwa mil. 10, kisha yeye akaiuza kwa mil 100, hawezi kuchukua mil. 90 kisha akapewa tena malipo ya %yake kutoka mil. 10.

Kitachofanyika hapo ni yeye kunufaika na kupanda kwa % ya malipo ya kazi yake mliyokubaliana awali.

Hivyo kama ni 5% ya mauzo ya 10,000,000 ni 500,000 sasa kwa mil. 100,000,000 atalipwa 5,000,000.

Nakueleza hivyo kutokana na uzoefu, maana hatua ya mwisho huwa ni kati ya muuzaji mwenye mali na mnunuzi, kuna kujaza mikataba ya kisheria ya uuzianaji wa nyumba na kijwanja.

Hivyo hakuna longo longo itakayofanywa na dalali na mteja bila ya mwenye mali kujua.
 
Mfano wewe unauza nyumba yako kwa milioni 10 umezunguka kutafta wateja mwaka mzima umekosa

Ukaamua kutafta dalali ukampa Kazi ya kuuza

Jioni ya siku hiyo anakuja na mteja na anainunua hiyo nyumba kwa milioni 100 dalali anatoa milioni 10 yako anakupa Kisha yeye anabaki na milioni 90

Je utakubali?

Mkuu iko hivi, unapotafuta dalali, unampatia mkadirio wa bei unayotaka kuuza, mf:hiyo mil. 10, kisha yeye ataitathimini na kukupa ushauri wake wa mkadirio wa bei kutokana na soko la sehemu husika.
Na malipo ya dalali hutokana na asilimia ya mauzo ya mali itakayouzwa, yaweza kuwa ni, 2% au 5%, vyovyote mtakavyokubaliana.

Lakini kila eneo huwa kuna asilimia wamejiwekea kama bei ya kufanya kazi ya kutafuta soko na kuuza mali flani.
Kwa hiyo dalali akipata soko la kuuza mali kwa bei ya juu kuliko mkadirio wa mwenye mali, yeye atanufaika na kupanda kwa asilimia ya malipo yake mliyokubaliana na si nje ya hapo.

Na mali ikiuzwa kwa bei ya chini, pia asilimia ya kumlipa dalali hushuka.

Na hakuna ujanja ujanja utakaofanywa na dalali pamoja na mteja bila ya mwenye mali kufahamu, maana kuna process za kubadilishana nyaraka hapo ujue, pamoja na bei mliyouziana.
 
Mkuu umetoa jibu la mtu ambaye hajafanya biashara ya aina hiyo na asiyejua lolote kuhusu.

Dalali ni taaluma, ni ofisi na ni mshauri wa mwemye mali.

Kwa hiyo hawezi kuuza nyumba kimaghumashi nje ya utaratibu wa kiofisi na kisheria pamoja na makubaliano ya kazi.

Wewe unapouza nyumba unapanga bei yako, unapomtafuta dalali ataiangalia kisha atafanya tathimini kutokana na hali ya soko la kijiografia na kutoa ushauri kwa mwenye mali.

Mwenye mali kabla ya kutoa 'go ahead' watakubaliana na dalali malipo yake kutokana na % fulani ya malipo yatakayopatikana kutokana na mauzo ya mali.

Kwa hiyo let say kama nyumba ilikuwa inauzwa mil. 10, kisha yeye akaiuza kwa mil 100, hawezi kuchukua mil. 90 kisha akapewa tena malipo ya %yake kutoka mil. 10.

Kitachofanyika hapo ni yeye kunufaika na kupanda kwa % ya malipo ya kazi yake mliyokubaliana awali.

Hivyo kama ni 5% ya mauzo ya 10,000,000 ni 500,000 sasa kwa mil. 100,000,000 atalipwa 5,000,000.

Nakueleza hivyo kutokana na uzoefu, maana hatua ya mwisho huwa ni kati ya muuzaji mwenye mali na mnunuzi, kuna kujaza mikataba ya kisheria ya uuzianaji wa nyumba na kijwanja.

Hivyo hakuna longo longo itakayofanywa na dalali na mteja bila ya mwenye mali kujua.
Chai
 
Ah maaamaae namruka dalali live kweupeeeee akiwa anaona, namwambia tugawane nusu kwa nusu kama hutak nakula yote pesa yote pekee yangu
unakula vipi sasa pesa wakati ukigoma mteja haleti 😄. wajanja ukizingua wanaua biashara. kuna mama ghorofa anataka mil 200 jamaa wakaleta mteja kwa mil 400
kilichofuata ITV...biashara wakaua na asiuze mpaka hivi leo miaka 8
 
Dalali wanaanza kuiponda mali yako 😂 na mnunuzi akiona hadi dalali anakataa mali bc anaamini amejaliwa sana 😂
 
Dalali mjanja (Mwene mtaji)apo anamalizana naww kwanza kwa kuinunua kwanza hiyo nyumba kwakiasi ulichokihitaji then anauza kwahiyo milion mia,sizan kama utalalamika popote utakapoona au kusikia kua nyunba uliyouza juzi milion 10 leo imeuzwa kwa milion 100
kuna bosi wangu msukuma alikua ndo zake yule jamaa kapiga sana pesa kwa staili hiyo 🤣
 
moja ya tatizo kubwa la binaadamu ni ubinafsi, badala ya kuchukua 80 yake aliyoitaka alipanik kwa 40 atakazokula dalali
hilo nalo ni neno naafiki
sema jambo lingine watu wengi hawapendi kuwatumia wathaminishaji kujua thamani halisi ya mali kabla ya kuiuza. wanajiropokea bila kujua. matokeo yake wengi wanakua wameweka makadirio madogo bila kujua thamani ni kubwa. mfano sisi tuliuza eneo milioni 90..wa pembeni yetu siku moja nyuma tena kwa ukubwa unaokaribiana aliuza kwa milioni 55. aliposikia tumeuza kwa bei hiyo jamaa aliumia dhahiri mpaka akawa anamtafuta tuliyemuuzia. lakini sisi tuliuza kulingana na thamani halisi ya ardhi ya eneo husika
 
Ilishawahi nitokea kabisa. Nilinunua shamba mwaka 2012 maeneo ya morogoro interior sasa ilipofika mwaka 2022 nikaamua kuliuza ila Kwa kugawa viwanja (ukubwa wa 30*20). Basi nikakata viwanja locally tu nikapata viwanja 20 nikatafuta dalali nikamwachia kazi. Bei 500,000 Kwa kiwanja kimoja .Baada ya wiki mbili dalali kanipia simu tayari anayo wateja wa viwanja vitano. Basi nikajongea Morogoro. Baada ya salamu dalali swali la kwanza akaniambia unakumbuka uliniambia niuze kiwanja shilingi ngapi? Nikamtajia then akaniambia sasa 2500000 ipo cash hayo mengine niachie ni ya kwangu, akaniambia hao wadau wakikwambia unauzaje waambie 1,200,000 Kwa kiwanja, yaan Mimi napokea laki Tano yeye laki Saba. Nilibadilisha gia angani nikamwambia mm nakula laki Tisa wewe utapokea laki tatu, hutaki napanda gari naondoka. Aisee ule mzozo ulikuwa sio wa kitoto lakini mwishowe anaikataaje laki tatu Kwa kiwanja kimoja? Mimi nikaambualia 4,500,000 na yeye 1,500,000
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom