Kifulambute
JF-Expert Member
- May 8, 2011
- 2,539
- 758
Hii imetokea jana katika Hospitali ya Sekouture mkoani Mwanza ambapo daktari aliyejulikana kwa jina moja tu la Rehema, mwajiriwa wa hosipitali ya Bugando aliyekuwa pia akifanya kazi hospitali ya Sekouture na ni shangazi wa mtuhumiwa, alipoteza ushahidi wa mtuhumiwa ambaye anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi vibaya Fidelis Lyimo.
Katika hali ya kushangaza mgonjwa alikuwa amelazwa katika hospitali ya Sekouture kwa matibabu na alipewa referal kwenda hospitali ya Bugando kwa matibabu zaidi baada ya kuona hali ya mgonjwa ni mbaya, lakini cha ajabu Dr Rehema aliingia kati na kuomba file ndipo alipotoa nyaraka zote zilizotoka polisi na kuanzisha file jipya ambalo linaonesha Fidelis (mgonjwa) hana tatizo lolote na akaweka mazingira Bugando asilazwe ili kuweza kumlinda mtuhumiwa na baadae mgonjwa aliweza kuwekwa chumba maalumu tu pale mapokezi.
Taarifa zaidi zinasema ilipofika asubuhi, kaka wa mtuhumiwa alifika hospitali (Bugando) asubuhi na mapema kudai apewe gharama za matibabu ili amtoe mgonjwa, wakati manesi wanajiandaa kumpatia ndipo akatokea dada wa mgonjwa na hali ikabadilika, yule mkaka alipoulizwa akadai hamjui Fidelis. Stori ni ndefu sana wajumbe.
My Take:
Kuna michezo mingi sana huwa inafanywa kati ya baadhi ya watendaji wa polisi na hospitali zetu panapotokea jambo kama hili na tumekuwa tukipoteza ndugu zetu kwa uzembe ama kulinda wahalifu ambao tunaishi nao....watanzania tuwe na woga wa Mungu, mgonjwa yule tangu Jumapili hajapata tiba mpaka leo kwa kumlinda mtuhumiwa