Daktari wa Sekou Toure apoteza ushahidi wa mtuhumiwa

Kifulambute

JF-Expert Member
May 8, 2011
2,540
752
Hii imetokea jana katika Hospitali ya Sekouture mkoani Mwanza ambapo daktari aliyejulikana kwa jina moja tu la Rehema, mwajiriwa wa hosipitali ya Bugando aliyekuwa pia akifanya kazi hospitali ya Sekouture na ni shangazi wa mtuhumiwa, alipoteza ushahidi wa mtuhumiwa ambaye anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi vibaya Fidelis Lyimo.

Katika hali ya kushangaza mgonjwa alikuwa amelazwa katika hospitali ya Sekouture kwa matibabu na alipewa referal kwenda hospitali ya Bugando kwa matibabu zaidi baada ya kuona hali ya mgonjwa ni mbaya, lakini cha ajabu Dr Rehema aliingia kati na kuomba file ndipo alipotoa nyaraka zote zilizotoka polisi na kuanzisha file jipya ambalo linaonesha Fidelis (mgonjwa) hana tatizo lolote na akaweka mazingira Bugando asilazwe ili kuweza kumlinda mtuhumiwa na baadae mgonjwa aliweza kuwekwa chumba maalumu tu pale mapokezi.

Taarifa zaidi zinasema ilipofika asubuhi, kaka wa mtuhumiwa alifika hospitali (Bugando) asubuhi na mapema kudai apewe gharama za matibabu ili amtoe mgonjwa, wakati manesi wanajiandaa kumpatia ndipo akatokea dada wa mgonjwa na hali ikabadilika, yule mkaka alipoulizwa akadai hamjui Fidelis. Stori ni ndefu sana wajumbe.

My Take:

Kuna michezo mingi sana huwa inafanywa kati ya baadhi ya watendaji wa polisi na hospitali zetu panapotokea jambo kama hili na tumekuwa tukipoteza ndugu zetu kwa uzembe ama kulinda wahalifu ambao tunaishi nao....watanzania tuwe na woga wa Mungu, mgonjwa yule tangu Jumapili hajapata tiba mpaka leo kwa kumlinda mtuhumiwa
 
Inasikitisha!!!

Ni shida sana yaani mtu yupo tayari mgonjwa kufa lkn amlinde tu mwenzake asipatwe na shida...mfano dakitari angeamua tu kumtibu na akapona vzr huwezi jua yawezekana mgonjwa akamsamehe tu mtuhumiwa ama wakayamaliza nje ya mahakama...sasa wanazidi kumweka mgonjwa anazidi kuumia...sijui akili gani hizi
 
... daktari aliyejulikana kwa jina moja tu la Rehema, mwajiriwa wa hosipitali ya Bugando aliyekuwa pia akifanya kazi hospitali ya Sekouture na ni shangazi wa mtuhumiwa, alipoteza ushahidi wa mtuhumiwa ambaye anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi vibaya Fidelis Lyimo.

Taarifa zaidi zinasema ilipofika asubuhi, kaka wa mtuhumiwa alifika hospitali (Bugando) asubuhi na mapema kudai apewe gharama za matibabu ili amtoe mgonjwa, wakati manesi wanajiandaa kumpatia ndipo akatokea dada wa mgonjwa na hali ikabadilika, yule mkaka alipoulizwa akadai hamjui Fidelis.
Inachanganya
 
Mi hata sijaelewa. Faili la mgonjwa huwa lina ushaihidi gani?
 
Mi hata sijaelewa. Faili la mgonjwa huwa lina ushaihidi gani?
Mie nahisi labda ushahidi unaokuwepo ni ule wa doctor wa kwanza kumtibu majeruhi,kwamba historia yake ni kama alimchunguza akakuta mgonjwa kavilia damu tumboni,ameumia kichwani may be kuna hali ya majeruhi kuonekana kupigwa sana na matibabu aliyoshauri kupewa mgonjwa na vitu kama hivyo..sina uhakika nimehisi tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom