Daktari: Muhimu kupima figo angalau mara moja kwa mwaka

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Wananchi wanashauriwa kufanya vipimo vya magonjwa ya figo angalau mara moja kwa mwaka, ili kupunguza hatari ya utambuzi wa magonjwa hayo katika hatua za hatari.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo wa Hospitali ya Saifee Tanzania iliyopo Kinondoni, Dk Mercy Mwamunyi amesema hayo alipokuwa akiwahudumia wananchi waliojitokeza kupimwa viashiria vya magonjwa hayo bure, huduma iliyotolewa na hospitali hiyo.

"Wagonjwa wengi tunaokutana nao wanakuwa wamefikia hatua ya nne au tano na dalili nyingi zinaanza kuonekana na kuleta madhara, allisema.

Alisema waliokutwa na viashiria walitakiwa kufanyiwa vipimo vya figo, kibofu na mirija yake (KUB) na kupewa dawa na ushauri zaidi.

Herman Kavishe, mkazi wa Temeke alisema amejitokeza kupima kwa kuwa anahisi maumivu ya tumbo na alishakwenda hospitali nyingine kupima kuambiwa figo ina tatizo na kupatiwa matibabu, ingawa hayakufanya kazi.

Meneja Mahusiano na Biashara wa hospitali hiyo, Christina Manongi alisema watu zaidi ya 200 walijitokeza kupata huduma hiyo.

Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Big Bon, Mohamed Buhashwan ambayo ilikuwa mdhamini mkuu wa tukio hilo alisema wanatambua umuhimu wa afya, ndiyo maana wameungana na hospitali hiyo kutoa huduma.

Figo new.jpg

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom