Daktari: Diamond Anamuua Baba’ke!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,809
34,193
BABA D.jpg

Baba mzazi wa Diamond, Mzee Abdul Juma.

Mwandishi wetu, Amani

DAR ES SALAAM: “Msongo wa mawazo ni tatizo kubwa duniani linalotokana na kusheheni kwa mawazo ya kila wakati, husasan kuhusu maisha au afya. Kwa hiyo anachofanya Diamond kwa baba yake ni sawa na kumuua kwa sababu ya kumsababishia msongo,” ndivyo alivyosema daktari Rweyemamu wa hospitali moja ya jijini Dar.

Daktari Rweyemamu alizungumza na Amani hivi karibuni kufuatia habari zinazoandikwa na Magazeti Pendwa ya Global Publishers kuhusu nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwamba amemtelekeza baba yake, Abdul Juma.

Diamond-Platnumz-1.jpg

Msanii Diamond Platinumz

AZUNGUMZIA HISTORIA

“Nimekuwa nikisoma habari mbalimbali kwenye Magazeti Pendwa ya Global, lakini hili la Diamond kumtelekeza baba yake mimi naona lina mapana yake. Najua utetezi wa Diamond ni kwamba, baba alimtelekeza mama yake (Sanura Kasim) yeye akiwa mtoto.

“Kwa hiyo malezi yote, ameyapata kwa mama mpaka kufika kwenye kiwango cha mafanikio. Lakini pia nimewahi kusoma kwamba, baba aliomba msamaha yaishe, atambulike kama baba lakini mtoto akagoma.”

MAGONJWA YA BABA

“Kuna wakati nikasoma kwamba, yule mzee anasumbuliwa na miguu, mara sijui ugonjwa wa kansa ya ngozi. Pia amekuwa mtu wa kuumwa mara kwa mara.”

MSONGO WA MAWAZO

NI CHANZO

“Yule mzee atakuwa na magonjwa mengi, hasa yanayotokana na msongo wa mawazo. Mawazo yake kwa sasa ni kitendo cha kuona mafanikio ya mwanaye akilinganisha na maisha yake magumu bila msaada.

“Binadamu yeyote, anapomwona mtu wake wa karibu amefanikiwa na yeye hali duni lakini huyo aliyefanikiwa anaweza kumsaidia yeye akaondokana na hali duni, lazima asumbuliwe na msongo.”

MIGOGORO, UGUMU

WA MAISHA

“Lakini pia migogoro inayotokea katika familia, ni moja kati ya sababu zinazoweza kumpa mtu msongo wa mawazo, hasa pale ambapo utaichukulia ‘serious’ kwa kuwa inagusa moja kwa moja maisha yake. Ugumu wa maisha unachangia pia.”

MWILI UNAVYOATHIRIWA

NA MSONGO

“Moja ya sababu ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa kuzorota kwa afya na kusababisha vifo vingi ni msongo wa mawazo. Mwili unavyokutana na hali tofauti aidha kitu cha kutisha au kinacholeta mawazo ndani ya muda mfupi na tofauti hiyo ikashindwa kutambuliwa haraka na ubongo mfano pale unapokutana na jambo usilolitegemea, basi mwili hutoa kichocheo kinachoitwa cortisol ambacho kinamwagwa kwenye damu ili kuuandaa mwili aidha kupigana au kukikimbia kitu hicho.

“Mapigo ya moyo huongezeka, mapafu huchukua kiwango kikubwa cha hewa na mzunguko wa damu pia huongezeka na baadhi ya sehemu za kinga huzidiwa na mzigo mkubwa hivyo kutoa nafasi kwa viumbe adui kuushambulia mwili kirahisi.

“Msongo wa mawazo unapokuwa mkubwa siku hadi siku ndipo kinga ya mwili inavyozidi kushindwa kubaini uwepo wa kichocheo cha cortisol, msongo unapunguza makali ya kinga ya mwili, hivyo matatizo ya afya huongezeka.”

UTAFITI

“Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na World Health Organization, Shirika la Afya Duniani ‘WHO’, maradhi ya moyo, akili, ugumba, ukosefu wa nguvu za kiume na vidonda vya tumbo, pia yanacha-ngiwa na msongo wa mawazo.”

LAZIMA BABA

DIAMOND AWE HIVI

Kwa mujibu wa daktari huyo, lazima baba Diamond wa sasa atakuwa amebadilika tabia, kwamba atakuwa mpole na siyo mwenye furaha kwa muda mwingi.

“Kuishi kwa kubangaiza pesa za kula huku akiwa anajua mwanaye anazo, tena mpaka zinamzidia, baba Diamond atakuwa anamalizika polepole. Lazima kila akiamka, anasema; ‘mateso yote haya, mwanangu yupo lakini hataki kunisaidia.”

WITO WAKE KWA DIAMOND

Daktari huyo alisema kuwa, anamtaka Diamond kurejesha moyo wake nyuma, amtunze baba yake ili amuokoe na kumalizika.

“Namtaka Diamond ajue kuwa, anachomfanyia baba yake ni kumuua bila yeye kujua. Ukuta anaomuwekea katika usaidizi unamfanya mzee huyo kunyemelewa na magonjwa ya moyo na vidonda vya tumbo ambavyo kwa mazingira ya maisha yake yanaweza kumsumbua kwani yanahitaji kipato kizuri.
chanzo.Daktari: Diamond Anamuua Baba’ke!
 
Badooo.. Badooo... Acheni kutelekeza watoto ni bahati Diamond hajafa mpaka sasa kwa kukosa malezi ya baba kwa stress na mengineyo, nahisi hata yule mama alipata vidonda vya tumbo, diamond nae alikosa elimu na kutaabika sana huku mshua akila bata
 
Hebu tuwe fair yaani yeye utotoni hajapata msaada kutoka kwa baba sasahivi kawa star baba anataka msaada kutoka kwa mtoto. Kwanini hajamtafuta alipokuwa akiuza mitumba? Mimi naona baba anataka hela tu hana mapenzi kwa mtoto lakini pia baba ni baba tu hata awe alikususa sio lazima na wewe umsuse.
 
Wengi wanasahau kuwa mtoto unaekataa kumlea au kumtelekeza ana madhara na mzazi kwa namna yyte,
Mtoto wako uliemtupa bila kutoa chochote akifanikiwa wewe utakuwa na madhara asipofanikiwa pia utakuwa na madhara tu,
Akishafanikiwa madhara yake ndio kama haya ya baba diamond kutwa kujipendekeza na hata akikubali kukusaidia hutakuwa na amri nae na utakuwa mtumwa wake tu,
Asipofanikiwa Ndio balaa maana akiwa mwizi, kahaba, bado watu watakunyooshea vidole tu wewe Ndio sababu, kwa hiyo ushauri wangu wanaume msikimbie majukumu ya kulea, watoto hawachelewi kukuuwa
 
Aliokula nao ujana si wamsaidie, Doctor nae asisumbue watu atibu mgonjwa ujuzi wake utapoishia amwache, ati Dai anamuua Baba yake, angekuwa kibaka huyu Mzee angemtafuta?
 
simple tu ka shigongo na gazeti zake wanamwonea huruma kwa nini asimsaidie yeye? aache kelele bana kila siku diamond diamond kwan yanamhusu?
 
View attachment 353369
Baba mzazi wa Diamond, Mzee Abdul Juma.

Mwandishi wetu, Amani

DAR ES SALAAM: “Msongo wa mawazo ni tatizo kubwa duniani linalotokana na kusheheni kwa mawazo ya kila wakati, husasan kuhusu maisha au afya. Kwa hiyo anachofanya Diamond kwa baba yake ni sawa na kumuua kwa sababu ya kumsababishia msongo,” ndivyo alivyosema daktari Rweyemamu wa hospitali moja ya jijini Dar.

Daktari Rweyemamu alizungumza na Amani hivi karibuni kufuatia habari zinazoandikwa na Magazeti Pendwa ya Global Publishers kuhusu nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwamba amemtelekeza baba yake, Abdul Juma.

View attachment 353370
Msanii Diamond Platinumz

AZUNGUMZIA HISTORIA

“Nimekuwa nikisoma habari mbalimbali kwenye Magazeti Pendwa ya Global, lakini hili la Diamond kumtelekeza baba yake mimi naona lina mapana yake. Najua utetezi wa Diamond ni kwamba, baba alimtelekeza mama yake (Sanura Kasim) yeye akiwa mtoto.

“Kwa hiyo malezi yote, ameyapata kwa mama mpaka kufika kwenye kiwango cha mafanikio. Lakini pia nimewahi kusoma kwamba, baba aliomba msamaha yaishe, atambulike kama baba lakini mtoto akagoma.”

MAGONJWA YA BABA

“Kuna wakati nikasoma kwamba, yule mzee anasumbuliwa na miguu, mara sijui ugonjwa wa kansa ya ngozi. Pia amekuwa mtu wa kuumwa mara kwa mara.”

MSONGO WA MAWAZO

NI CHANZO

“Yule mzee atakuwa na magonjwa mengi, hasa yanayotokana na msongo wa mawazo. Mawazo yake kwa sasa ni kitendo cha kuona mafanikio ya mwanaye akilinganisha na maisha yake magumu bila msaada.

“Binadamu yeyote, anapomwona mtu wake wa karibu amefanikiwa na yeye hali duni lakini huyo aliyefanikiwa anaweza kumsaidia yeye akaondokana na hali duni, lazima asumbuliwe na msongo.”

MIGOGORO, UGUMU

WA MAISHA

“Lakini pia migogoro inayotokea katika familia, ni moja kati ya sababu zinazoweza kumpa mtu msongo wa mawazo, hasa pale ambapo utaichukulia ‘serious’ kwa kuwa inagusa moja kwa moja maisha yake. Ugumu wa maisha unachangia pia.”

MWILI UNAVYOATHIRIWA

NA MSONGO

“Moja ya sababu ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa kuzorota kwa afya na kusababisha vifo vingi ni msongo wa mawazo. Mwili unavyokutana na hali tofauti aidha kitu cha kutisha au kinacholeta mawazo ndani ya muda mfupi na tofauti hiyo ikashindwa kutambuliwa haraka na ubongo mfano pale unapokutana na jambo usilolitegemea, basi mwili hutoa kichocheo kinachoitwa cortisol ambacho kinamwagwa kwenye damu ili kuuandaa mwili aidha kupigana au kukikimbia kitu hicho.

“Mapigo ya moyo huongezeka, mapafu huchukua kiwango kikubwa cha hewa na mzunguko wa damu pia huongezeka na baadhi ya sehemu za kinga huzidiwa na mzigo mkubwa hivyo kutoa nafasi kwa viumbe adui kuushambulia mwili kirahisi.

“Msongo wa mawazo unapokuwa mkubwa siku hadi siku ndipo kinga ya mwili inavyozidi kushindwa kubaini uwepo wa kichocheo cha cortisol, msongo unapunguza makali ya kinga ya mwili, hivyo matatizo ya afya huongezeka.”

UTAFITI

“Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na World Health Organization, Shirika la Afya Duniani ‘WHO’, maradhi ya moyo, akili, ugumba, ukosefu wa nguvu za kiume na vidonda vya tumbo, pia yanacha-ngiwa na msongo wa mawazo.”

LAZIMA BABA

DIAMOND AWE HIVI

Kwa mujibu wa daktari huyo, lazima baba Diamond wa sasa atakuwa amebadilika tabia, kwamba atakuwa mpole na siyo mwenye furaha kwa muda mwingi.

“Kuishi kwa kubangaiza pesa za kula huku akiwa anajua mwanaye anazo, tena mpaka zinamzidia, baba Diamond atakuwa anamalizika polepole. Lazima kila akiamka, anasema; ‘mateso yote haya, mwanangu yupo lakini hataki kunisaidia.”

WITO WAKE KWA DIAMOND

Daktari huyo alisema kuwa, anamtaka Diamond kurejesha moyo wake nyuma, amtunze baba yake ili amuokoe na kumalizika.

“Namtaka Diamond ajue kuwa, anachomfanyia baba yake ni kumuua bila yeye kujua. Ukuta anaomuwekea katika usaidizi unamfanya mzee huyo kunyemelewa na magonjwa ya moyo na vidonda vya tumbo ambavyo kwa mazingira ya maisha yake yanaweza kumsumbua kwani yanahitaji kipato kizuri.
chanzo.Daktari: Diamond Anamuua Baba’ke!
Sioni uhusiano wowote wa habari hii na jukwaa la entertainment.Habari hii ingekuwa kwenye mmu ningeielewa.
 
Ebu nisaidieni,Diamond anajiita mmaniema original.Alipata wapi kabila na jina la ukoo kama si kwa baba yake?Inakuwsje Diamond mtoto wa kiume anaendeshwa na mama yake?Alikuepo wakati
wazazi wake wanagombana?Hata kama alikuepo kwa nini asisimame katikati ili awahudumie wazazi wote?Huyo tiffan wake anamfundisha nini?
 
kudadei demond kama unaweza mpe sumu afe kabsa, mimi mwenyewe babangu alitelekeza, kudadeki siku nikisikia anaumwa nasherekea afe potelea kote wamezidi midume wakujua kupiga pumbu tu!
Aiseeee!
 
Angekuwa mama alimtelekeza kidogo unaweza kujirudi sbb alikubeba tumboni kwa shida miezi9.Hata wkt anakulekeza roho ilikuwa inamuuma.
Ila baba shenzii type tena ateseke sana kabla hajafa hakuna ht haja y kumsaidia ni kumuombea zaidi apate na maradhi yote hadi kipindupindu na ebola!shiiiiittt
 
Kwa kichwa cha habari tu huyo Daktari afanye kazi take aache yasiyomuhusu kuongelea sijui mgonjwa sijui nini... mfy... tamaa ya pesa anatia aibu
 
Angekuwa mama alimtelekeza kidogo unaweza kujirudi sbb alikubeba tumboni kwa shida miezi9.Hata wkt anakulekeza roho ilikuwa inamuuma.
Ila baba shenzii type tena ateseke sana kabla hajafa hakuna ht haja y kumsaidia ni kumuombea zaidi apate na maradhi yote hadi kipindupindu na ebola!shiiiiittt
mzazi huwa hakosei hata kama ni kwa namna ipi, ikiwa dunia yetu itakuwa hai kwa miaka 2, huenda maisha ya hyo jamaa yatakuwa mabaya sana,

kama si kutaka kumtoa kafara baba yake, ili aendelee kustawi atakuwa na matatzo ya akili
 
Hakosei mungu tu bana baba ni binadam lazma akosee!au unataka kusema wababa wanaobaka watoto wao ni sahihi sio makosa!

Sent from my TECNO-Y3+ using JamiiForums mobile app
 
Hii iwe fundisho kwa wanaume wanaotelekeza watoto kwa namna au sababu yoyote na kumuachi mama ateseke peke yake, misongo ya mawazo kwa zamu, mama Diamond alimaliza kipande chake mzee nae apambane kumaliza ngwe yake.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom