Daktari: Diamond Anamuua Baba’ke!

Daktari: Diamond Anamuua Baba’ke!

Kama alimtelekeza mama na mwanae, na pengine akaenda kutanua na malaya barabarani aachwe tu kama alivyowaacha yeye bila huruma.
 
kama umeomba msamaha mara zote hizo mtu akashndwa kuelewa just move on mzee.....nenda katubu kwa Mungu wako msikitini yeye atakusamehe la msingi umeshajutia kosa lako baba
 
Daaaah!!! Nikiyakumbuka yale mahaba yako hadi nyege zinapanda dear!!.....Wewe ni kiboko, may God bless you!

Wow naona umeniota haswa hadi umeshindwa kuvumilia na kuamua kuniandikia, endelea tu na ndoto hewa. Kwa avatar yangu na u black beauty sikushangai ndugu kwa kuniwazia kimahaba.
 
Huyo baba anahangaika tu... vipi diamond angekua hana pesa?? je huyo jamaa angesema mwanae anamuua??

Tena akufwee, akufwe kabisa
 
Kitanda usicholalia hujui kunguni wake. Huyo baba acha akinywee kikombe cha uharibifu wake.

Aliyoyapitia Diamond katika maisha ya ukuaji wake anayajua mwenyewe. Kama Shigongo anamuonea huruma amsaidie. Si anatoa habari zake kila siku na zinauzika... amgawie hela kidogo ya mauzo akatibiwe kama kweli anaumwa.

Aligombana na mke kwa nini alitelekeza watoto. Si angeendelea kulea watoto. Au baada ya Diamond kukua na kupata hela bifu limeisha kwa upande wake. Vipi mateso aliyoyasababisha alipowatelekeza. Akale nyasi huko asichoshe watu... kalikoroga wacha alinywe!!!!
 
View attachment 353369
Baba mzazi wa Diamond, Mzee Abdul Juma.

Mwandishi wetu, Amani

DAR ES SALAAM: “Msongo wa mawazo ni tatizo kubwa duniani linalotokana na kusheheni kwa mawazo ya kila wakati, husasan kuhusu maisha au afya. Kwa hiyo anachofanya Diamond kwa baba yake ni sawa na kumuua kwa sababu ya kumsababishia msongo,” ndivyo alivyosema daktari Rweyemamu wa hospitali moja ya jijini Dar.

Daktari Rweyemamu alizungumza na Amani hivi karibuni kufuatia habari zinazoandikwa na Magazeti Pendwa ya Global Publishers kuhusu nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwamba amemtelekeza baba yake, Abdul Juma.

View attachment 353370
Msanii Diamond Platinumz

AZUNGUMZIA HISTORIA

“Nimekuwa nikisoma habari mbalimbali kwenye Magazeti Pendwa ya Global, lakini hili la Diamond kumtelekeza baba yake mimi naona lina mapana yake. Najua utetezi wa Diamond ni kwamba, baba alimtelekeza mama yake (Sanura Kasim) yeye akiwa mtoto.

“Kwa hiyo malezi yote, ameyapata kwa mama mpaka kufika kwenye kiwango cha mafanikio. Lakini pia nimewahi kusoma kwamba, baba aliomba msamaha yaishe, atambulike kama baba lakini mtoto akagoma.”



MAGONJWA YA BABA

“Kuna wakati nikasoma kwamba, yule mzee anasumbuliwa na miguu, mara sijui ugonjwa wa kansa ya ngozi. Pia amekuwa mtu wa kuumwa mara kwa mara.”



MSONGO WA MAWAZO

NI CHANZO

“Yule mzee atakuwa na magonjwa mengi, hasa yanayotokana na msongo wa mawazo. Mawazo yake kwa sasa ni kitendo cha kuona mafanikio ya mwanaye akilinganisha na maisha yake magumu bila msaada.

“Binadamu yeyote, anapomwona mtu wake wa karibu amefanikiwa na yeye hali duni lakini huyo aliyefanikiwa anaweza kumsaidia yeye akaondokana na hali duni, lazima asumbuliwe na msongo.”



MIGOGORO, UGUMU

WA MAISHA

“Lakini pia migogoro inayotokea katika familia, ni moja kati ya sababu zinazoweza kumpa mtu msongo wa mawazo, hasa pale ambapo utaichukulia ‘serious’ kwa kuwa inagusa moja kwa moja maisha yake. Ugumu wa maisha unachangia pia.”

MWILI UNAVYOATHIRIWA

NA MSONGO

“Moja ya sababu ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa kuzorota kwa afya na kusababisha vifo vingi ni msongo wa mawazo. Mwili unavyokutana na hali tofauti aidha kitu cha kutisha au kinacholeta mawazo ndani ya muda mfupi na tofauti hiyo ikashindwa kutambuliwa haraka na ubongo mfano pale unapokutana na jambo usilolitegemea, basi mwili hutoa kichocheo kinachoitwa cortisol ambacho kinamwagwa kwenye damu ili kuuandaa mwili aidha kupigana au kukikimbia kitu hicho.

“Mapigo ya moyo huongezeka, mapafu huchukua kiwango kikubwa cha hewa na mzunguko wa damu pia huongezeka na baadhi ya sehemu za kinga huzidiwa na mzigo mkubwa hivyo kutoa nafasi kwa viumbe adui kuushambulia mwili kirahisi.

“Msongo wa mawazo unapokuwa mkubwa siku hadi siku ndipo kinga ya mwili inavyozidi kushindwa kubaini uwepo wa kichocheo cha cortisol, msongo unapunguza makali ya kinga ya mwili, hivyo matatizo ya afya huongezeka.”



UTAFITI

“Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na World Health Organization, Shirika la Afya Duniani ‘WHO’, maradhi ya moyo, akili, ugumba, ukosefu wa nguvu za kiume na vidonda vya tumbo, pia yanacha-ngiwa na msongo wa mawazo.”



LAZIMA BABA

DIAMOND AWE HIVI

Kwa mujibu wa daktari huyo, lazima baba Diamond wa sasa atakuwa amebadilika tabia, kwamba atakuwa mpole na siyo mwenye furaha kwa muda mwingi.

“Kuishi kwa kubangaiza pesa za kula huku akiwa anajua mwanaye anazo, tena mpaka zinamzidia, baba Diamond atakuwa anamalizika polepole. Lazima kila akiamka, anasema; ‘mateso yote haya, mwanangu yupo lakini hataki kunisaidia.”

WITO WAKE KWA DIAMOND

Daktari huyo alisema kuwa, anamtaka Diamond kurejesha moyo wake nyuma, amtunze baba yake ili amuokoe na kumalizika.

“Namtaka Diamond ajue kuwa, anachomfanyia baba yake ni kumuua bila yeye kujua. Ukuta anaomuwekea katika usaidizi unamfanya mzee huyo kunyemelewa na magonjwa ya moyo na vidonda vya tumbo ambavyo kwa mazingira ya maisha yake yanaweza kumsumbua kwani yanahitaji kipato kizuri.
chanzo.Daktari: Diamond Anamuua Baba’ke!
Dangote

Dangote

Dangote


Naomba umsaidie dingi mana anadhalikika saiv apooo
Dangote
 
baba diamond ni mshenzi sana.. mtu kulea ukwepe ila wewe utake kulelewa na mtoto...

mtu kama huyu unamtupa kwenye dust bin tu... whats goes around comes around
 
kusamehe na kusahau ni jambo la msingi,,,maumivu yanakuwepo ila yatupasa kusameheana na kupatana kabla jua halijatwama
 
Daktari anasoma magazeti ya udaku. Hao ndio wale wanaotoa mimba.
 
Dangote wala usisikilize ushauri wa kutoa msamaha kwa huyo baba ako jina katanua weeeee zimemuishia ndo anarejesha majeshi aende kule akafie mbali
 
Kutoka kwenye chemba kubwa kubwa ya moyo wangu: INGEKUWA MIMI NDIO DIAMOND NINGEMSAMEHE BABA YANGU
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom