Daktari aliyembusu mgonjwa wake asakwa

Daktari aliyembusu mgonjwa wake asakwa

Mytake: Watu hatari kwa wake zetu ni;

*Daktari wanao watibu wake zetu,

*Dreva wanao waendesha wake zetu,

*HouseBoy, Gardeners, Walinzi.

*Wauza duka na urembo wakina mama, wapaka rangi za kucha...

*nk.

*

Mbona Mangi muuza genge humtaji?
 
Kikibwa hapo inatakiwa wanawake watbiwe na wanawake wenzio na wanaume watibiwe na wanaume wenzio

Hilo lingesaidia enzi za Mwalimu mkuu zama hizi kuna usagaji na ukoboaji nothing is safe anymore!
 
Anasakwa kwa lipi?huwezi kumpiga mtu busu kama hakuna prior agreement,waacheni wafu wazikane kwa wafu
 
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo, ameliagiza Jeshi la Polisi na Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, Lucas Mweri, kumchukulia hatua daktari anayetuhumiwa kumbusu mgonjwa wake wakati akimtibu.

Gambo alitoa agizo hilo jana baada ya kupokea malalamiko ya tukio hilo na kueleza kuwa ni la ukiukwaji wa maadili ya kidaktari na aibu kwa wilaya.

Aliliagiza jeshi la polisi kufanya uchunguzi na kuchukua hatua za kisheria ili iwe fundisho kwa mtaalamu huyo na wengine wenye tabia kama hiyo.

Awali ilidaiwa kuwa daktari huyo, Ally Naah anayefanyakazi Hospitali ya Wilaya ya Korogwe ya Magunga, anadaiwa kumbusu mwanamke aliyekwenda kupata matibabu hospitalini hapo.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema siku ya tukio mwanamke huyo aliambatana na mumewe hadi hospitalini hapo kwa ajili ya kupata matibabu na baada ya kufika daktari huyo alimtaka aingie ndani kumfanyia uchunguzi.

Ilidaiwa kuwa, mume wa mwanamke huyo aliyekuwa nje akimsubiri mkewe alipata hofu baada ya kuona muda mrefu umepita bila mkewe kutoka, ndipo alipochungulia dirishani na kumuona daktari huyo akimbusu.

“Yule bwana hakuamini alichokiona, hakuvumilia na alipiga kelele akiomba msaada…Kwa kweli jambo hili ni aibu na limetuondolea uaminifu,” alisema mmoja wa shuhuda wa tukio hilo.

Hata hivyo, habari za kipolisi zinaeleza kuwa tayari tukio hilo limeshaanza kufanyiwa kazi ikiwamo kufuatiliwa eneo lilipotendeka kosa hilo kwa hatua zaidi za kisheria. Mganga Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Dk Olden Ngasa, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema mtuhumiwa alitoroka baada ya tukio hilo.

Source: Nipashe
​
 
Mh ni hatari sn, huyo ni mmoja tu kati ya madaktari wengi wanaodhalilisha wake, dada zetu na hata mama zetu, ni tukio la fedheha sn kwakweli ingawa huyo mwanamke anaonekana alikubaliana na kilichokuwa kinaendelea, nafikiri gazeti pia limetumia tafsida ila ukweli ni kuwa daktari alikuwa anamla denda huyo mwanamke
 
Office abuse, Dr kachemsha pale ni kazini sio mahala pa mapenzi, achukuliwe hatua ikithibitika liwe fundisho, October askari police nao walimiss behave wakiwa kazini walitimuliwa ilipothibitika kadhalika na huyu Dr ikithibitika afukuzwe hata kama mwanamke alikubali.
 
Huyo Mke nae Ana kisiwa katulia tuu? Au alikua anasubiri ushahidi kamili?
 
Mytake: Watu hatari kwa wake zetu ni;

*Daktari wanao watibu wake zetu,

*Dreva wanao waendesha wake zetu,

*HouseBoy, Gardeners, Walinzi.

*Wauza duka na urembo wakina mama, wapaka rangi za kucha...

*nk.

*
Wauza nyama mabuchani na pombe za kienyeji!
 
Hiv yule Mkuu wa Wilaya alomtukana Mwanasheria wa Halmashauri alikuwa wa wilaya gani? Alimwambia yule dada an digrii ya Chupi
 
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo, ameliagiza Jeshi la Polisi na Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, Lucas Mweri, kumchukulia hatua daktari anayetuhumiwa kumbusu mgonjwa wake wakati akimtibu.
Gambo alitoa agizo hilo jana baada ya kupokea malalamiko ya tukio hilo na kueleza kuwa ni la ukiukwaji wa maadili ya kidaktari na aibu kwa wilaya.
Aliliagiza jeshi la polisi kufanya uchunguzi na kuchukua hatua za kisheria ili iwe fundisho kwa mtaalamu huyo na wengine wenye tabia kama hiyo.
Awali ilidaiwa kuwa daktari huyo, Ally Naah anayefanyakazi Hospitali ya Wilaya ya Korogwe ya Magunga, anadaiwa kumbusu mwanamke aliyekwenda kupata matibabu hospitalini hapo.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema siku ya tukio mwanamke huyo aliambatana na mumewe hadi hospitalini hapo kwa ajili ya kupata matibabu na baada ya kufika daktari huyo alimtaka aingie ndani kumfanyia uchunguzi.
Ilidaiwa kuwa, mume wa mwanamke huyo aliyekuwa nje akimsubiri mkewe alipata hofu baada ya kuona muda mrefu umepita bila mkewe kutoka, ndipo alipochungulia dirishani na kumuona daktari huyo akimbusu.
“Yule bwana hakuamini alichokiona, hakuvumilia na alipiga kelele akiomba msaada…Kwa kweli jambo hili ni aibu na limetuondolea uaminifu,” alisema mmoja wa shuhuda wa tukio hilo.
Hata hivyo, habari za kipolisi zinaeleza kuwa tayari tukio hilo limeshaanza kufanyiwa kazi ikiwamo kufuatiliwa eneo lilipotendeka kosa hilo kwa hatua zaidi za kisheria. Mganga Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Dk Olden Ngasa, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema mtuhumiwa alitoroka baada ya tukio hilo.

CHANZO: NIPASHE

AH!! ilitakiwa iwe the opposite..daktari apige kelele ya kuomba msaada baada ya kichapo cha mwizi kutoka kwa mme wake huyo dada.
 
Mytake: Watu hatari kwa wake zetu ni;

*Daktari wanao watibu wake zetu,

*Dreva wanao waendesha wake zetu,

*HouseBoy, Gardeners, Walinzi.

*Wauza duka na urembo wakina mama, wapaka rangi za kucha...

*nk.

*

hata sisi wamachinga msituamini sana.
 
Au ilikuwa ni 'kiss of death'????
naona ni 'French Kiss' huyu Dr na Mama wanajuana kwani naona walinyonyana Ndimi kabisa na kubalishana Mate
sasa dume joga linambana Dr peke yake badala na Mama
 
Busu tu nae ndo akaanza kuomba msaada kwa kupiga kelele bila hata aibu, mkeo anabusiwa unapiga kelele? Si angefanya maamuzi kimya kimya tu. Halafu ilikua busu tu au jamaa alienda extra mile? Yaani mkeo kakaa ndani muda mrefu mpaka unaamua kuchungulia halafu uwakute bado wapo step01 out of 5steps? Angesema ukweli labda alikuta step02.
 
Back
Top Bottom