Daktari aliyembusu mgonjwa wake asakwa

Daktari aliyembusu mgonjwa wake asakwa

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,686
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo, ameliagiza Jeshi la Polisi na Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, Lucas Mweri, kumchukulia hatua daktari anayetuhumiwa kumbusu mgonjwa wake wakati akimtibu.

Gambo alitoa agizo hilo jana baada ya kupokea malalamiko ya tukio hilo na kueleza kuwa ni la ukiukwaji wa maadili ya kidaktari na aibu kwa wilaya.
Aliliagiza jeshi la polisi kufanya uchunguzi na kuchukua hatua za kisheria ili iwe fundisho kwa mtaalamu huyo na wengine wenye tabia kama hiyo.

Awali ilidaiwa kuwa daktari huyo, Ally Naah anayefanyakazi Hospitali ya Wilaya ya Korogwe ya Magunga, anadaiwa kumbusu mwanamke aliyekwenda kupata matibabu hospitalini hapo.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema siku ya tukio mwanamke huyo aliambatana na mumewe hadi hospitalini hapo kwa ajili ya kupata matibabu na baada ya kufika daktari huyo alimtaka aingie ndani kumfanyia uchunguzi.

Ilidaiwa kuwa, mume wa mwanamke huyo aliyekuwa nje akimsubiri mkewe alipata hofu baada ya kuona muda mrefu umepita bila mkewe kutoka, ndipo alipochungulia dirishani na kumuona daktari huyo akimbusu.

"Yule bwana hakuamini alichokiona, hakuvumilia na alipiga kelele akiomba msaada…Kwa kweli jambo hili ni aibu na limetuondolea uaminifu," alisema mmoja wa shuhuda wa tukio hilo.
Hata hivyo, habari za kipolisi zinaeleza kuwa tayari tukio hilo limeshaanza kufanyiwa kazi ikiwamo kufuatiliwa eneo lilipotendeka kosa hilo kwa hatua zaidi za kisheria. Mganga Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Dk Olden Ngasa, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema mtuhumiwa alitoroka baada ya tukio hilo.

CHANZO: NIPASHE
 
Mytake: Watu hatari kwa wake zetu ni;

*Daktari wanao watibu wake zetu,

*Dreva wanao waendesha wake zetu,

*HouseBoy, Gardeners, Walinzi.

*Wauza duka na urembo wakina mama, wapaka rangi za kucha...

*nk.

*
 
Vipi huyo mgonjwa mwenyewe mbona alikua ametulia hadi mumewe alipochungulia napata wasi kuwa huenda wanafahamiana na daktari kitambo hapo ndipo walipata fursa yakukutana mtu namwenziwe.
 
...huyu mwanaume mpuuzi tu, inakuwaje asijue tiba aliyohitaji mkewe ni busu!? Ndo madhara ya kutotoa nafasi ya kumsikiliza mwenzako kwenye mahusiano.

Mkuu wa wilaya boya sana, hajui kuwepo kwa chama cha madaktari!?
 
Mytake: Watu hatari kwa wake zetu ni;

*Daktari wanao watibu wake zetu,

*Dreva wanao waendesha wake zetu,

*HouseBoy, Gardeners, Walinzi.

*Wauza duka na urembo wakina mama, wapaka rangi za kucha...

*nk.

*

*mabosi wa kiume maofisini.
 
Kikibwa hapo inatakiwa wanawake watbiwe na wanawake wenzio na wanaume watibiwe na wanaume wenzio
 
Mytake: Watu hatari kwa wake zetu ni;

*Daktari wanao watibu wake zetu,

*Dreva wanao waendesha wake zetu,

*HouseBoy, Gardeners, Walinzi.

*Wauza duka na urembo wakina mama, wapaka rangi za kucha...

*nk.

*

mkuu umewasahau walima bustani
 
Yaani hapo mume wa mgonjwa ndio wa kushtakiwa . amekiuka sheria ya siri za mgonjwa. ugonjwa ni siri kati ya mgonjwa na daktari .kosa lake huyo jamaa ni kuchungulia dirishani na kusikiliza siri za mgonjwa. huyo mume atafutwe apelekwe kizimbani kwa kosa la kukatisha matibabu ya mgonjwa.
 
Kikibwa hapo inatakiwa wanawake watbiwe na wanawake wenzio na wanaume watibiwe na wanaume wenzio

Mi naona huyo mume angeingia kwa dr na mkewe.........kuna Siri gani ya kumficha mumewe.......?.....
 
Siasa bana!!asa mkuu wa wilaya iyo ishu inamuhusu nn?hiyo ni ishu ya mwenye mke akashtaki polisi,asa eti mkuu wa wilaya amewaagiza polisi,hizi ni siasa tu!
 
Mkuu wa Wilaya hilo ndo jukumu alilopewa linalomfanya alipwe mshahara na serikali? no wonder there
 
Samahani mkuu. kama hutojali Jivike viatu vya mme wa huyo Alipokea Busu. then niambie. Nipe sababu ya kutoamini kuwa Hii sheria kama kweli ipo Dr mnajificha hapa kutuletea ukimwi majumbani kwetu. Ijapokuwa huyo Mke wa jamaa alikubali.
 
Mi naona huyo mume angeingia kwa dr na mkewe.........kuna Siri gani ya kumficha mumewe.......?.....
Ila huyo bidada nae ana vijimambo, ina maana alikuwa anaisikilizia tu hiyo kiss ya Dr. wake?.
 
Back
Top Bottom