Daktari aliyembusu mgonjwa wake asakwa

Daktari aliyembusu mgonjwa wake asakwa

Mi naona huyo mume angeingia kwa dr na mkewe.........kuna Siri gani ya kumficha mumewe.......?.....

Saa nyengine inahitaji moyo.....kama wife anamimba.....unajua anaweza mtia kidole mbele yako....eti anaangalia njia....
 
Saa nyengine inahitaji moyo.....kama wife anamimba.....unajua anaweza mtia kidole mbele yako....eti anaangalia njia....

Poa tu.......kuna shida gani na ni matibabu bana........
 
Walikubaliana,kwanini mwanamke asingechukua hatua wakati akiliwa denda.
 
@Preta kama ni check up au matibabu yanayohusana na nyetini Dr atakapoanza kuangalia nyetini na kumpa order mrembo kaa hivi kaa vile na huku akigusa gusa nyeti na kuzikodolea mimacho kwa karibu, mume aweza kurusha ngumi kwa kuona Dr hastahili kufanya hivyo. Ndiyo sababu kwa usalama wao Madaktari wengi wanawapiga stop akina husbands/boyfriends wasiingie maofisini kwao kama "mgonjwa" ni mdada

Mi naona huyo mume angeingia kwa dr na mkewe.........kuna Siri gani ya kumficha mumewe.......?.....
 
yani copy and pest umeshindwa ndugu ,swala la kupona ni la mwenyezi mungu ,kubwa zaidi kuondoa hayo matatizo ,kama angelikuwa mke wako kafanyiwa hivyo ?
 
Mytake: Watu hatari kwa wake zetu ni;

*Daktari wanao watibu wake zetu,

*Dreva wanao waendesha wake zetu,

*HouseBoy, Gardeners, Walinzi.

*Wauza duka na urembo wakina mama, wapaka rangi za kucha...

*nk.

*

bila kumsahau shemeji
 
Kikibwa hapo inatakiwa wanawake watbiwe na wanawake wenzio na wanaume watibiwe na wanaume wenzio

mzee kipinga;
Acha ubaguzi weyee. Na manersi wanaume wawazalishe wanaume waja wazito?? Sijui weye upo sayari gani lakini ka ni hii ya dunia umepotoka.
Jiulize, mgonjwa huyo alikuwa amezidiwa kiasi gani mpaka aone amalizane na Daktari mle mle ofisini wakati alijua mmewe yupo hapo nje tu ya mlango. Huyo ni kicheche waliokutana na paka shume. Mkuu wa wilaya kwa kukosa kazi anafukuzana na wapendanao. Kuna kaugonjwa kapya kabisa kameingia wilaya hiyo nako dawa yake ni Dakitari kumpapasa mgonjwa wake vizuri na kuonja mate yake kama yana kisukari au vipi??
Mume boya hilo, hamfikishi mkewe kunakooooo. Mngesema huyo mama alilia kilio ndani mmewe akachungulia ningewaelewa. Lakini mambo kimyaa mpaka mume akachungulia mtaalam anavyompimia mke, umeona wapi??
 
@Preta kama ni check up au matibabu yanayohusana na nyetini Dr atakapoanza kuangalia nyetini na kumpa order mrembo kaa hivi kaa vile na huku akigusa gusa nyeti na kuzikodolea mimacho kwa karibu, mume aweza kurusha ngumi kwa kuona Dr hastahili kufanya hivyo. Ndiyo sababu kwa usalama wao Madaktari wengi wanawapiga stop akina husbands/boyfriends wasiingie maofisini kwao kama "mgonjwa" ni mdada

Wanajiweka hatarini mkuu, utaratibu unataka nurse awepo ndani! !
 
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo, ameliagiza Jeshi la Polisi na Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, Lucas Mweri, kumchukulia hatua daktari anayetuhumiwa kumbusu mgonjwa wake wakati akimtibu.
Gambo alitoa agizo hilo jana baada ya kupokea malalamiko ya tukio hilo na kueleza kuwa ni la ukiukwaji wa maadili ya kidaktari na aibu kwa wilaya.
Aliliagiza jeshi la polisi kufanya uchunguzi na kuchukua hatua za kisheria ili iwe fundisho kwa mtaalamu huyo na wengine wenye tabia kama hiyo.
Awali ilidaiwa kuwa daktari huyo, Ally Naah anayefanyakazi Hospitali ya Wilaya ya Korogwe ya Magunga, anadaiwa kumbusu mwanamke aliyekwenda kupata matibabu hospitalini hapo.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema siku ya tukio mwanamke huyo aliambatana na mumewe hadi hospitalini hapo kwa ajili ya kupata matibabu na baada ya kufika daktari huyo alimtaka aingie ndani kumfanyia uchunguzi.
Ilidaiwa kuwa, mume wa mwanamke huyo aliyekuwa nje akimsubiri mkewe alipata hofu baada ya kuona muda mrefu umepita bila mkewe kutoka, ndipo alipochungulia dirishani na kumuona daktari huyo akimbusu.
“Yule bwana hakuamini alichokiona, hakuvumilia na alipiga kelele akiomba msaada…Kwa kweli jambo hili ni aibu na limetuondolea uaminifu,” alisema mmoja wa shuhuda wa tukio hilo.
Hata hivyo, habari za kipolisi zinaeleza kuwa tayari tukio hilo limeshaanza kufanyiwa kazi ikiwamo kufuatiliwa eneo lilipotendeka kosa hilo kwa hatua zaidi za kisheria. Mganga Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Dk Olden Ngasa, alithibitisha kutokea kwa tukio hi
 
Yaani hapo mume wa mgonjwa ndio wa kushtakiwa . amekiuka sheria ya siri za mgonjwa. ugonjwa ni siri kati ya mgonjwa na daktari .kosa lake huyo jamaa ni kuchungulia dirishani na kusikiliza siri za mgonjwa. huyo mume atafutwe apelekwe kizimbani kwa kosa la kukatisha matibabu ya mgonjwa.


Siri wapi wakati ni mwili mmoja,la mkewe ndo la kwake.alikuwa sahihi kuchungulia tu.
 
Huyu mwanaume inaonekana ana wivu sana na kwanini achungulie dirishani kwa nini asigonge mlango aingie ndani? Eti alivyoona akapiga kelele .
 
Jamani Watanzania tuwe makini tunapotoa hukumu watu bila kufikiri kwani naona huyu mkuu wa wilaya amekwenda mbali bila kujua chanzo cha tatizo hizi ni siasa zake. Ni hivi kwanza huyu mkuu wa wilaya alipaswa kuripoti ishu na kukaa asubiri uchunguzi wa polisi, kwani huwezi kuniambia mimi nimeingia kwa Dr ambaye hatufahamiani na ambaye hatujaongea lolote pengine hata kuhusiana na mapenzi alafu anaanza kunibusu tu na nimetulia kama mti wa mnazi, tena kwa mgonjwa niliyekuwa sijazidiwa kwani ningezidiwa ningeingia ndani na my husband wangu, hapa kuna hidden issue, kwanini tusijihoji kwamba huenda hawa watu walikuwa na mahusiano kabla.

Na pili huenda hawa watu walikuwa na mahusiano ambayo yalikwisha hisiwa na mume wa mgonjwa na ndiyo maana alipata sababu ya kumwacha mkewe peke yake aingie kwa daktari ili afuatilie nini kinaendelea, pia kwanini hatujihoji kwamba huu ni mpango wa ulipizaji kisasi uliopangwa wa kumuharibia daktari kazi yake? Kwanini hatujihoji ilikuwaje baada ya mume kuona mkewe anachelewa hakufungua mlango akaenda kuchungulia dirishani! Jamani naifahamu hospitali ya wilaya Korogwe vizuri na nafahamu vyumba vya madaktari vilivyo kwanini mtu achukue jukumu la kuzunguka jengo mpaka aende dirishani kuna nini?

Kitu kingine ninachokihoji je ni yeye peke yake aliyeshuhudia mkewe akipigwa busu je kuna jicho la mtu mwingine aliyeshuhudia hili jambo? Na kwanini hatujihoji kwamba huenda huyu mwanamke ndiye aliyempiga Dr busu, jamani wanawake pia wanawatega madaktari? Any way sipendi kumhukumu mtu kabla sijapata data za kunifanya kufanya hivyo, sina maana ya kumtetea Dr ila nimeona visasi na malipizi yakiwaharibia watu maisha. Korogwe naijua vyema, Huku kupenda umaarufu kutatufikisha pabaya
 
Back
Top Bottom