Dakika zake 15 za umaarufu ndo zimekwisha?

Dakika zake 15 za umaarufu ndo zimekwisha?

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
97,062
Reaction score
136,424
Ni kapteni Tesha!

Huyu nadhani ndo basi tena. Hatutomuona wala kumsikia tena.

Keshajipatia umaarufu ndani ya hizo dakika zake 15 alizokuwa nazo na sasa zimeisha.

Hivyo, ni ama atapotea mwenyewe kwa hiari yake au atapotezwa, hiyo ni kama bado yupo na hajapotea wala kupotezwa.

Alifanya makosa makubwa ya kimkakati.

Mtu mwenye nia ya kufanya kweli, angetenda kwanza halafu ndo kuonyesha sura yake na kutoa tamko lake.

Lakini siyo kuonyesha sura na kutoa tamko la nia.

Sijui alipata wapi hayo mafunzo yake ya uanajeshi!

Habari ndo hiyo. Kwisha habari yake huyo.
 
We sema unataka tu kujua amechukuliwa hatua gani. Kiufupi ni kuwa uchunguzi unaendelea hko jeshini na kubaini nini haswa kilimsukuma. Baada ya uchunguzi kuisha tegemea kumuona mahakama za kiraia.

Kitu pekee kinachoweza kumuokoa ni maandamano ya kiraia, ambayo mpaka sasa ni kama kila mtz anayasubiri ila hakuna anayetaka kutoka.

The last hope of Tesha ni the mass of Tanzanians.
 
Watu kusema kile kinachowaumiza ni kutafuta umaarufu? Kwamba tunavyoinanga serikali mitandaoni tunatafuta umaarufu kumbe?
Tanzania watu tumekuwa na utamaduni wa woga kiasi ambacho hata mtu anaposema ukweli kuhusu ubovu wa uongozi watu wanamwangalia mara mbili mbili. Kwa wale waliosoma kitabu cha Shaaban Robert, Kusadikika, wasadikika unaweza kuwafananisha kabisa na watanzania wa sasa.

Hata mhusika mkuu, Karama, alipojitokeza na kuanza kusema ukweli karibu wasadikika wote walishangaa na kujiuliza haogopi?
 
ila we jamaa mjinga sana.

Kama kweli wewe una mikakati kuliko tesha hebu jitokeze mstari wa mbele wa mapambano na hilo bichwa lako wakubamize.

Unawakejeli wapambanaji huku wewe uko Ulaya unaosha vibwenye vya wazungu.
 
Well! Well! Well!

Labda lengo lake halikuwa kuwepo zaidi ya huo muda unaotaka. The damage is done, ameeka doa aliloweka. For a member of a military kusema aliyoyasema ni doa na damage kwa waliotajwa…

His work was done, if anything else it shall be an icing on the cake.

Infact, damage yake ilikuwa kubwa na ilileta taharuki kwa watu wa huko juu. Tulio na taarifa tunajua mama dully alikuwa kwenye hari gani. It was chaotic, pressure ilipanda hadi 180 mmHg. Her anxiety was off the charts.
 
Ni kapteni Tesha!

Huyu nadhani ndo basi tena. Hatutomuona wala kumsikia tena.

Keshajipatia umaarufu ndani ya hizo dakika zake 15 alizokuwa nazo na sasa zimeisha.

Hivyo, ni ama atapotea mwenyewe kwa hiari yake au atapotezwa, hiyo ni kama bado yupo na hajapotea wala kupotezwa.

Alifanya makosa makubwa ya kimkakati.

Mtu mwenye nia ya kufanya kweli, angetenda kwanza halafu ndo kuonyesha sura yake na kutoa tamko lake.

Lakini siyo kuonyesha sura na kutoa tamko la nia.

Sijui alipata wapi hayo mafunzo yake ya uanajeshi!

Habari ndo hiyo. Kwisha habari yake huyo.
Kwamba unataka aingie live kila siku kama mange kimambi
 
Back
Top Bottom