Dakika Sifuri.

Dakika Sifuri.

Picha yako tu mie hoi.
Nimekufa ndani ya dak 0
Otis the illuminati
 
Bongo unaweza kupewa huduma, kwa ilivyombovu, ukachoka ndani ya dakika sufuri
 
ni sawa na 'in five....'?

Be back in five!
'in no time...'
Na ujue ukiambiwa hivyo utachina tu kama kawa...
suala la muda kwetu ni moja ya majanga ya kitaifa...!
 
kweli wabongo wengi hatujali muda,mtu unaagiya msosi hotelini wanakwambia kitakuwa tayari baada ya dakika 15 lakini wanachukua zaidi ya nusu saa..inakera kweli
 
napiga kamoja tu halafu dakika sifuri nageuka, sii unajua usilete udandala maana haina vanga
 
Na wengi wanatumia kigezo cha foleni kama excuzi mtu ana kwambia nipo shekilango nipe dakikatano anakuja baada ya nusu saa ukimuuliza utasikia foleni kubwa kumbe sio kweli.
 
We unaambiwa nisubiri dk o ,na ww unasubiri si uzuzu ni nn!! Dk 0 ndo ndo dkika ngapi!!
 
Hivi watanzania tumefikia Kutojali muda kiasi hiki?

What the hell is Dakika Sifuri.

Ndio maana ukienda sehemu mbali mbali kupata huduma, ukiuliza bado muda gani unaambiwa Bado Kidogo.

''nitakutumia sio Muda''
''nisubiri kidogo''
''nakuja''
''nitafanya kesho''- hapa hausemwi muda gani.

Watanzania tunahitaji Elimu ya Muda.

Hata wageni wanaotoka nje ya Africa wanatuelewa hivyo.

Kuna siku nimesafari na mtu kutoka Japani, akawa na Laptop yake juu karibu na keyboard ina picha kubwa ya tembo na maandishi "NO HURRY IN AFRICA".

Nilimchukia Mjapani yule na sikuongea naye mpaka mwisho wa safari. Lakini ukweli ni huo - muda sufuri. Tunahitaji kubadilika kama tunapenda maendeleo.
 
akheri ya dakika 0 kuliko nitaoa mwakani huwa ndio mwakani haifiki kabisa
 
kwani tuwe na haraka ya kwenda/kufanya nini,
then utapata nini, ndo maana kila mtu anafanya atakavyo.
 
Kweli UngaLTD mbali. . . Inabidi tuwe na thread ya slang mpya mpya wengine tusipitwe.

Nasikia ungaLTD wanaongoza arusha nzima kwa kupiga cha arusha. ni kweli?!
POPOBAWA.
 
Back
Top Bottom