Daily News mambo si shwari? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Daily News mambo si shwari?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mbongo Orijino, Aug 6, 2009.

 1. M

  Mbongo Orijino New Member

  #1
  Aug 6, 2009
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna habari nimezipata toka kwa mmoja ya wadau juu ya utendaji usioridhisha wa Uongozi wa TSN au wachapishaji wa gazeti kongwe kuliko yote Daily News na Habari Leo, Japo si wazi lakini yasemekana kuna kama kamgomo baridi fulani hivi kutokana na wafanyakazi kutoridhishwa na utendaji huo na yasemekana ni miaka karibia sita sasa hakuna nyongeza ya aina yoyote ya mshahara tofauti na enzi za boss wa zamani ambaye baadaye alipelekwa Ikulu, zaidi kinachofanyika ni kama usanii hivi na uongozi ambao nao kwa sasa upo kama haupo vile kwa kuwapiga kalenda wafanyakazi kila mwaka kama watoto wa kuku vile kuwa watanyonya kesho.


  Zipo tuhuma nyingi na nyingine ziliwahi hata kuandikwa na gazeti fulani juu ya ukabila, upendeleo na zaidi viongozi wake kuwa Ma Vasco Dagama fulani kwa kupishana angani au juu kwa juu tu, na yasemekana wengi wa wafanyakazi ambao wameendelea kuwapo pale wapo kwa ajili ya kontact tu kwa wengi wana makampuni yao ambayo ndo yanawashughulisha zaidi kuliko TSN.


  Wenye data kamili naomba mtupatie na hasa wana JF waliopo hapo TSN (naamini wapo) kwani hili ni shirika la umma na si mali ya mtu binafsi na Watanzania wana haki ya kujua kile kinachojiri hapo kwa faida ya wote.
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Inaweza kuwa umbeya kwa sababu ndugu zangu walio katika tasnia ya habari wananipasha kuwa TSN, kwa sasa, ni moja ya kampuni yenye marupurupu mazuri kwa waandish ukilinganisha na kampuni nyingine
   
 3. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #3
  Aug 6, 2009
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Na huu ndio ukweli wenyewe.

  TSN wanalipa vizuri sana kwa sasa. Hata mie nina rafiki zangu pale waliwahi kufanya kazi MCL na AMGL kabla ya kutua TSN, wanasema mambo ni mazuri sana kulinganisha na walikotoka.
   
 4. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #4
  Aug 6, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  very true mambo mengine ni mambo ya mtu mmoja mmoja na hakuna management isiyokuwa na mafanikio na matatizo, ndio maana kila taasisi ina check and balance systeam kwa maana ya board na management systeam...
   
 5. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #5
  Aug 6, 2009
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  Ingawa Daily News ni gazeti la serikali lakini ninapolisoma "online" nnaridhika na mtirirko wa habari zake ingawa ni ukweli kwamba magazeti ya serikali siku zote hupambapamba mambo.

  Kuna mifano kama ya "The Herald" la Zimbabwe na "Daily News" la India ambayo yana tabia ya kupambapamba.

  Huko nyuma kabla ya magazeti mengine kuongezwa waandishi wa habari wa magazeti ya TNS yalikuwa pia moto.

  Haya mambo mengine yasiyo na "concrete" au hata "shread of evidence" yasipewe nafasi.
   
 6. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #6
  Aug 6, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Magazeti ya Serikali sasa yajitahidi kuandika ukweli katika habari zao.Kuhusu maslahi ni umbea kwa kuwa kama mtu haridhiki angehamia sehemu yenye tija kwake kwani ajira ni huria.
   
 7. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #7
  Aug 6, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Je ni kweli kuwa baadhi ya waandishi wapo hapo TSN kwa contacts tu kwa vile tayari wana makampuni yao ambayo ndio yanawashughulisha zaidi ya wanavyojishughulisha TSN?

  Je ni kweli u Vasco da Gama umezidi TSN?

  Je ni kweli kuna upendeleo na ukabila TSN?

  Nadhani haya ndio maswali ya msingi zaidi ya mleta hoja kuliko suala la maslahi.
   
 8. M

  Mbongo Orijino New Member

  #8
  Aug 6, 2009
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Yaa hapo nadhani umenipata, hizi ndo point za kuzungumzia, kwa si tulio nje yaonekana mambo ni swaaafi lakini ukikutana na mmoja wa waliomo utakosa kusikia manunguniko haya au yale, yawezekana baadhi ya watu wakawa wanalipwa vyema lakini je ni wote? ikiwa ni kweli zaidi ya miaka mitano hakuna nyongeza huko kulipwa vizuri ni kupi?
   
 9. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #9
  Aug 6, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Majungu hayawaishi wa bongo
   
 10. M

  Manitoba JF-Expert Member

  #10
  Aug 7, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 240
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Si kweli kwamba kila asiyehama kazi anaridhika na malipo anayolipwa. Na si kila asiyeridhika ana-opportunity ya kupata sehemu yenye tija zaidi.

  Na mtu asiyeridhika na malipo akiendelea kubaki haimaanishi kwamba ndio amebadili mawazo la hasha. Na kama wewe ndio mwajiri wake, be very afraid. Hakawii kuanza kukuibia halafu ulalamike "wafanyakazi siku hizi wezi".

  Na wala sisemi kwamba kama mwajiriwa haridhiki na anacholipwa basi akaibe, la hasha! Ila inanishangazaga tunapofumbia macho ukweli kwamba mwajiri naye ana wajibu wa kutafuta wafanyakazi wanaoridhika na anachowalipa. Na waajiri wengi makini huwa wanaliangalia hili wakati wa usaili.

  Akifanikiwa kuwafanyisha kazi wasioridhika awe tayari pia kuishi na matokeo yake.

  To every action there is an equal and opposite reaction.
   
 11. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #11
  Aug 7, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Nitamuuliza Isack Mruma, kwani mara nyingi sana tumekutana katika makongamano mbalimbali ya wanahabari.

  Huyu alikuwa TCRA na sasa ndio bosi wa TSN.
   
 12. Mairo

  Mairo Member

  #12
  Aug 7, 2009
  Joined: Jun 4, 2009
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau wengi naona wamekanusha vikali kuwa hakuna tatizo TSN, ila mi napata walakini kidogo na msimamo wao kwasababu hakuna hata mmoja ambaye ametoa facts halisi kuonyesha kuwa anachokielezea mtoa mada ni tofauti. Mimi kwa mfano najua mwishoni mwa mwaka 2006 na mwaka 2007 TSN kulikuwa na atmosshphere ambayo ilipelekea wafanyakazi hasa wa upande wa marketing kuondoka na kutafuta sehemu zingine (nina macollege mate wangu wawili walikuwa hapa waliondoka ktk kipindi hicho). Nakumbuka hata katika kipindi hicho Mkuu wa marketing ambaye alikuwa ametokea CRDB naye aliondoka. Sasa Kwa kwa hoja ya mdau nashawishika kuamini hali inaweza ikawa kweli ipo tete. Kama kuna mtu ana data za uhakika kutuonyesha hoja iliyoko mbele yetu si sawa atuambie kwa undani na sio kusema tu wapo vema.
   
Loading...