Dagaa afungwa miaka 240 kwa ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dagaa afungwa miaka 240 kwa ufisadi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nat867, Aug 9, 2008.

 1. n

  nat867 Member

  #1
  Aug 9, 2008
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 97
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mhasibu wa shule ya sekondari Mbinga, ruvuma kahukumiwa miaka 240 jela kwa makosa 60 ya kughushi nyaraka za serikali na kuiba milioni 240 za mishahara ya watumishi waliostaafu na waliokufa.
  Hakimu wa mahakama ya mkoa ruvuma amesema "kutokana na makosa haya mshitakiwa atapata adhabu hiyo ambayo itamfanya ajue kuwa alifanya kosa kubwa la wizi". Makosa yote yanaenda pamoja so jela ni miaka 5.
  Hii habari inatugusa, hivyo ni muhimu kuuliza mapapa wa rushwa na ufisadi lini watashtakiwa kama huyu. Au ndo tunasubiri mpaka magereza ya VIP Yakarabatiwe?
  Au ndo wanaogopwa kuguswa kwa sababu wanajua waliokula nao katika ufisadi
  tutaishia kufunga dagaa badala ya mapapa. Ngoja usikie ripoti ya mwanyika itakavyokosa meno ya kuuma. Inauma kuona mapapa bado wanapeta.
   
 2. Mauza uza

  Mauza uza JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2008
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 2,045
  Likes Received: 742
  Trophy Points: 280
  Duuuh lakini huyo nae sio kadagaa at least ungesema ni sangara,240m is too much to.Fisadi ni fisadi tuu haijalishi.
   
 3. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2008
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  HALAFU ONA IPPMEDIA WANAVYOPIGA DEBE, UTAFIKIRI KAFANYA KWELIKWELI KUMBE MBWEMBWE TU. WAANDISHI WENGINE WAMELISHWA UNGA WA NDELE. haya ni maajabu hata minyoo inaitwa nyoka. eti huyo mhasibu wa shule ni kigogo? au ndo kumkebehi Rais? uummh makubwa haya!

  JK afanya kweli

  2008-08-09 14:52:15
  Na Mwandishi Wetu, Songea

  Tahadhari ambayo imekuwa ikitolewa mara kwa mara na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bwana Jakaya Kikwete kuwa Serikali yake haitakuwa na msamaha kwa viongozi na watumishi watakaofanya ufisadi kwa kutumia pesa za umma kwa manufaa yao binafsi, imeanza kuliza vigogo baada ya vijana wa kazi kufanya kweli na kumsweka jela kigogo mmoja.

  Hatua hiyo imekuja baada ya vijana wa JK kuvalia njuga sakata la kigogo huyo, hadi kupata ushahidi wa kutosha juu ya namna jamaa huyo alivyolamba mapesa ya umma.

  Kigogo huyo aliyeswekwa jela ni Mhasibu wa Shule ya Sekondari Mbinga mkoani hapa aitwaye Omari Millanzi, 56.

  Mapesa hayo yaliangukia mikononi mwa kigogo huyo baada ya kutumwa na ofisi ya Hazina ili yafanye kazi ya kuboresha elimu.

  Hata hivyo kigogo huyo alizinyaka pesa hizo na kuzikandamizia kwenye mambo yake mwenyewe hadi aliposhtukiwa na kuburuzwa kortini.

  Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Ruvuma, Baptist Mhelela ndiye aliyesikiliza kesi juu ya sakata hilo na baadaye kumuona Millanzi ana hatia katika makosa 60 aliyoshtakiwa.

  Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mhelela alisema kuwa kwa kuzingatia ombi la Mwendesha Mashtaka aliyetaka adhabu kali itolewe kwa mshtakiwa, na kwa kuzingatia vilevile kuwa mshtakiwa amekutwa na hatia ya makosa hayo yote, mahakama imeamua kumfunga jela mshtakiwa huyo kwa miaka mitatu kwa kila kosa, katika mashtaka 30 ya awali, hivyo kutakiwa atumikie jela kwa miaka 90.

  Aidha, Hakimu Mhelela akasema kwa makosa mengine 30, kila kosa litampasa mshtakiwa atumikie jela kwa miaka mitano, hivyo jumla kuwa miaka mingine 150.

  Jumla kuu ya kipindi cha adhabu za mshtakiwa huyo kilipaswa kuwa miaka 240 jela.

  Hata hivyo Hakimu Mhelela alisema kwakuwa adhabu zote zitatumikiwa kwa pamoja, mshtakiwa atakwenda jela miaka mitano.
  Pia Hakimu huyo akaamuru mshtakiwa alipe kiasi chote cha pesa alizoiba kwa mwajiri wake ambazo ni Sh. Milioni 24.1, mara tu baada ya kumaliza adhabu yake ya kifungo.

  Kabla ya hukumu hiyo, upande wa mashtaka ukioongozwa na Inspekta George Omary, ulidai kuwa katika kipindi cha mwezi Januari na Julai mwaka 1998, mshtakiwa Millanzi aligushi nyaraka mbalimbali za Serikali na kuiba pesa hizo, kaisi cha Sh. Milioni 24.1.

  Alipotakiwa kujitetea, ndipo mshtakiwa Millanzi alipomlilia hakimu na kumtaka ampunguzie adhabu akidai kuwa ana umri mkubwa na kuwa vilevile, ana familia inayomtegemea.

  Mara kwa mara, Rais Kikwete amekuwa akisisitiza juu ya nidhamu ya matumizi mazuri ya pesa za umma na kuonya kuwa yeyote atakayekiuka taratibu, atachukuliwa hatua kali za kisheria.

  * SOURCE: Alasiri
   
 4. n

  nat867 Member

  #4
  Aug 9, 2008
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 97
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Samahani wana JF, I did typing error hela alizoiba ni 24m na si 240m. Samahani.Na source ya habari ni TANZANIA DAIMA ya leo.
   
 5. k

  kalld Member

  #5
  Aug 10, 2008
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  duuuh!shombo kali! ati nini????baada ya kifungo alipe??????walioiba mabilioni wanapeta!
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Aug 10, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,487
  Likes Received: 81,782
  Trophy Points: 280
  Niliiyona hii article IPPMEDIA nikataka kujua JK kafanya yapi tena, kumbe ni wale wale mafisadi ambao wakiguswa nchi haitawaka moto, wale wengine bado mkuu anaogopa kumwagia mchanga kitumbua chake maana wanaweza kweli kuitia kibiriti Tanzania ikalipuka moto :(
   
 7. G

  Gustanza_The Senior Member

  #7
  Aug 10, 2008
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nziku, next time, nikikuta gazeti lenye headline ya ujinga kama Alasiri ya leo eti "Kikwete afanya Kweli?," yule aliyeniuzia hilo gazeti atakula kibano hadi ajikojolee!! I mean it!

  Huu ni upuuzi wa hali ya juu! IPPMEDIA ni sawa na nguruwe pori. Hawana hata ethics za uandishi hawa! Pumbaf kabisa!
   
 8. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #8
  Aug 10, 2008
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Kwi kwi kwi... Gustanza usimpe kibano aliye kuuzia gazeti huenda hahusiki na upotoshaji yeye ni mchuuzi tu, lakini inauma!
   
 9. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #9
  Aug 10, 2008
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nadhani nimeona kuna aina fulani ya kaunafiki fulani ka IPP Media kuwa bega kwa bega na JK maana hata ITV ukiangalia sasa hawaishi kutoa na kushabikia hotuba za JK za huko mikoani anakoshinda sasa hivi kuhubiri pumba zake kwamba serikali iko karibu na wananchi.
   
 10. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #10
  Aug 10, 2008
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0

  Hebu rekebisha hapa kwanza ndio wengine tuanze kuchangia

  240 mill = 24.1Mill ????
   
 11. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #11
  Aug 10, 2008
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Hawa ndiyo dawa yao; sheria ichukue mkondo wake.

  Huu ufisadi mdogomdogo kawaida unashughulikiwa kwelikweli maanake hata kidodogo cha kugawana na watunza sheria inakuwa hamna kitu, linalobaki kesi iendeshwe kwa mujibu wa sheria.
   
 12. G

  Gustanza_The Senior Member

  #12
  Aug 11, 2008
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I don't care kama amehusika/hakuhusika kupotosha ukweli. As long as anashiriki kusabaza upotoshaji, then he is just as guilty as mpotoshaji.
   
 13. C

  CottonEyeJoe JF-Expert Member

  #13
  Aug 11, 2008
  Joined: Jan 8, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  On the Real wanaJamii wenzangu... What the hell is wrong with us Tanzanians, mbona ?????? Who's fault is it that we are this way???? And how can we get back on the right path... Some questions to ponder before 2010, Go out and Vote to make a difference.
   
 14. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #14
  Aug 11, 2008
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ukiiba 100 Million Ukamlipa Lawyer 40 Million Una Nafasi Ya Kukwepa Jela Lakini Ukiiba 24 Millioni Huna Hela Ya Kumlipa Lawyer Hivyo Jela Lazima Unless Hakimu Ndugu Yako.
   
 15. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #15
  Aug 11, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mwizi ni mwizi tu. Na fisadi ni fisadi tu bila kujali rangi yake au ukubwa wake. Huyu alistahili hukumu hii maana naye ni fisadi tu.
  Hata hivyo kama hawa vigogo wakubwa nao ni mafisadi na wanatakiwa adhabu kama ya huyu. RA, Karamagi, EL, na BWM pamoja na kundi jingine kubwa ambalo wao wanadhani magereza zinapanuliwa kwa ajili ya wengine na wao wapelekwe mahakamani. Itajulikana huko hatima yao.
   
 16. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #16
  Aug 11, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mchukia Fisadi, naungana na wewe. Pamoja na hayo,
  NAOMBA KUTOA TAARIFA:

  Watuhumiwa wakuu wa Ufisadi, akiwamo Jeetu Patel, wamo katika orodha mpya ya wafadhili wa CCM 2010. Na huenda wakawa wamejadiliwa katika vikao vyao vya ndani vya hivi karibuni. Je, hawa kweli tutegemee kufikishwa mahakamani? Au ndio hao dagaa tu?
   
 17. Z

  Zanaki JF-Expert Member

  #17
  Aug 11, 2008
  Joined: Sep 1, 2006
  Messages: 544
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wakati nasoma hii nilikuwa nasubiri kile kipengele ambacho huwa kinatumiwa na majaji wakitoa hukumu kama hii kuwa "iwe ni fundisho kwa wengine..." It seems hili ni fundisho ambalo kamwe halitafundishika.
   
 18. M

  Maktauwo Member

  #18
  Aug 11, 2008
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naona matatizo makubwa mawili

  1. Habari hii imeandikwa kwa ushabiki na kujikomba kwa hali ya juu
  na kwenda kinyume kabisa na maadili ya uandishi. Inanikumbusha siku chache zilizopita mchora katuni wa Kenya alivyochora waandishi wa habari wa Tanzania wakimlamba miguu Rais Kikwete.

  2. Tatizo kwenye figure ambapo chini tunaona ni sh 24.1 na mwanzo ni sh240.
   
Loading...