Lisa
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 1,549
- 1,075
Hahahahahaahaaaaaaaaaaaaa! umenifurahisha sana hapo kwenye blue kaka Mtambuzi, maana umenikumbusha mbali sana , hivi hizo sabuni zipo kweli? maana ni siku nyingi sana sijaziona.Loh!Kibaya zaidi watoto wengine hugeuzwa kishada, kutoka nyumba moja hadi nyingine.... mara kwa babu na bibi, mara kwa mjomba, mara kwa mama mkubwa, mtoto hana uhakika kesho ataamkia wapi.... mwishowe mtoto anakosa malezi yenye msimamo, maana anachokatazwa kwa bibi akienda kwa mama mkubwa kinaruhusiwa, na anachokatazwa kwa mjomba kwa bibi na babu ni ruksa, yaani mtoto anakuwa na malezi vipande vipande utadhani sabuni ya kodrai............... LOL
Back to topic, unalosema ni kweli kabisa, wanawake tunafanya makosa hayo sana, kuzaa na kuwapeleka watoto kwa wazazi, halafu hupeleki matumizi yoyote, kule ambako mwanao yupo, hili mm nimeleiona sana wakati naenda kwa bibi yangu moshi, unakuta mtu kaleta mtoto pale kamwacha hapo hamjali kabisa, sasa mzigo unakuwa kwa bibi kumlea na kumsomesha, unakuta mtoto analima kahawa, akamue maziwa wakauze ndiyo apate pesa ya sabuni na sukari, au wazazi wetu wapeleke vitu na nguo ambazo hatuvai tena yeye ndiyo anaziona mpya kwake.Mpaka roho zilikuwa zinatuuma, ikabidi tumwambie mama amchuke ndipo akaja kwetu.
Nawaomba wanawake wenzangu kuliko uje kutesa mtoto wako hapa duniani, ni kheri usizae.tumia dawa za mpango wa uzazi.