Dada zetu na tabia ya kutelekeza watoto…..!

Dada zetu na tabia ya kutelekeza watoto…..!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,443
nancy-mtethwa.jpg

Bibi na wajukuu zake...............

Ipo tabia moja ambayo imeshamiri kwa upande wa kina dada au wanawake wengi ya kuwatelekeza watoto wao nyumbani kwa wazazi wao. Suala la kuwatunza hao watoto wenyewe kama wazazi huwa halipo, wakishazaa hujua jukumu lao limekwisha, hivyo majukumu yote ya kuwatunza na kuwalea watoto wao, huyaacha mikononi mwa wazazi wao.

Wanawake hawa hufanya hivyo kwa kisingizio kwamba, wanakwenda kutafuta fedha za matumizi kwa ajili ya watoto wao, kwa kuamini kwamba, wanapowaacha watoto hao nyumbani kwa wazazi wao (Kwa babu na bibi wa watoto), kazi yao ya utafutaji wa fedha huwa rahisi zaidi.

Ukweli ni kwamba, watoto waliotelekezwa na mama zao, huongeza mzigo mkubwa kwa wazee hao, ambao walio wengi tayari wameelemewa na mzigo wa hali ngumu ya kiuchumi. Akina dada wenye tabia hii huwa hawapo tayari kuwajibika wao binafsi, wala kuwawajibisha wanaume waliowapa mimba, kwa lengo la kutaka kuendelea na starehe zao bila bughudha ya watoto na wengine huona watoto kama mzigo utakaowazuia kufanya shughuli zao za kuwapatia kipato.

Kulingana na hali ngumu ya kimaisha na utegemezi waliyo nayo wazazi hawa wanaopelekewa mzigo wa watoto, hukubali kwa haraka kuishi na wajukuu zao, kwa lengo kusaidiwa na kunufaika kiuchumi, kutoka kwa hao watoto wao, pale watakapotumiwa misaada na fedha za matumizi kwa ajili ya wajukuu zao.

Lakini kwa bahati mbaya sana baadhi ya wazazi hao hujikuta wakiumia kwa kukosa misaada hiyo toka kwa watoto wao kama walivyoahidiwa. Kwani wazazi wengine wenye hao watoto hutokomea kabisa mijini na kusahau watoto wao na wengine hujikuta wanarudi majumbani kwa wazazi wao na kuwa mzigo mwingine, kwa kuwa jitihada za kutafuta fedha za matumizi ya watoto wao zimeshindikana.

Ipo mifano mingi ya watoto wanaotunzwa na babu na bibi zao, ambao wanaonekana kwa kila hali kukosa malezi bora na huduma muhimu za msingi, kutokana na wazazi wao kutotuma fedha kwa ajili ya matumizi ya watoto wao. Kina mama wenye tabia ya kutelekeza watoto wao kwa wazazi wao bila kutuma fedha za matumizi kama walivyoahidi, wanapaswa kuondokana na tabia hiyo mara moja. Si vyema kusukumia majukumu hayo mazito kwa wazazi wao ambao tayari wameshazeeka.
 
Kwakweli. Unapoamua kuzaa heri ufikiri mpango wa malezi ya mwanao na kuwa ni jukumu lako kabisa. Kama bado ulihitaji ujana heri ni kuwa makini kuliko kuja mletea mtoto shuruba asizostahili. Haikubaliki kabisa
 
Kina dada wanajipa mimba na kuzaa wenyewe?
Kaka nimeshazungumzia jambo hilo, haya soma hapo kwenye bold nyekundu
Ukweli ni kwamba, watoto waliotelekezwa na mama zao, huongeza mzigo mkubwa kwa wazee hao, ambao walio wengi tayari wameelemewa na mzigo wa hali ngumu ya kiuchumi. Akina dada wenye tabia hii huwa hawapo tayari kuwajibika wao binafsi, wala kuwawajibisha wanaume waliowapa mimba, kwa lengo la kutaka kuendelea na starehe zao bila bughudha ya watoto na wengine huona watoto kama mzigo utakaowazuia kufanya shughuli zao za kuwapatia kipato.
 
Kaka nimeshazungumzia jambo hilo, haya soma hapo kwenye bold nyekundu

Kwa nini hawataki kuwawajibisha wanaume waliowapa mimba? Ni kina dada wa wapi hao uliowaona hivyo? Una statistics gani za ku support haya?

Unaweza kuwa institution ya mambo haya wewe kama unaweza ku support statements zako.

Usije tu kuangalia sample space ya types za mtaani kwenu ukaja na generalization hapa.

Tueleze vizuri.
 
Kwakweli. Unapoamua kuzaa heri ufikiri mpango wa malezi ya mwanao na kuwa ni jukumu lako kabisa. Kama bado ulihitaji ujana heri ni kuwa makini kuliko kuja mletea mtoto shuruba asizostahili. Haikubaliki kabisa
Kibaya zaidi watoto wengine hugeuzwa kishada, kutoka nyumba moja hadi nyingine.... mara kwa babu na bibi, mara kwa mjomba, mara kwa mama mkubwa, mtoto hana uhakika kesho ataamkia wapi.... mwishowe mtoto anakosa malezi yenye msimamo, maana anachokatazwa kwa bibi akienda kwa mama mkubwa kinaruhusiwa, na anachokatazwa kwa mjomba kwa bibi na babu ni ruksa, yaani mtoto anakuwa na malezi vipande vipande utadhani sabuni ya kodrai............... LOL
 
hao wazazi ndo wanapenda kujiletea mizigo upendo gani wa kubebeshana mizigo wakati wazazi wao wako hai,inategemea na familia uliyotoka aisee kama kwetu huwezi kwenda kumuachia mama mtoto labda umpeleke kusalimia baada ya mda fulani unamchukua na pia anaenda na mlezi, hako katabia kakuendekeza kulea wajukuu wakati mama zao wanakula bata ni ujinga na hiyo inasababisha mabinti wengi wanarukaruka na kuzaa ovyo wakijua bibi na babu wapo watalea.
 
Mtambuzi kwanza nimekumic....
Pili asante kwa ujumbe mzuri kwa wadada wanaokwepa matokeo ya kile walichokipanda
sijajua kasumba hii itaisha lini maana wabibi wa watu huko wanaelemewa na wajukuu
kama huyo anao watano dhuuu two more to come hadi atafungua shule sasa
 
Last edited by a moderator:
Kwa nini hawataki kuwawajibisha wanaume waliowapa mimba? Ni kina dada wa wapi hao uliowaona hivyo? Una statistics gani za ku support haya?

Unaweza kuwa institution ya mambo haya wewe kama unaweza ku support statements zako.

Usije tu kuangalia sample space ya types za mtaani kwenu ukaja na generalization hapa.

Tueleze vizuri.

mhhhhhhhh haya we mtaka statistics
kama kusoma hujui basi bila shaka utakuwa unaona
sina maana ya kukukwaza
kuna vitu vingine unatumia observaton method njia ya kawaida ambayo hata kipofu anaiweza
 
Kwa nini hawataki kuwawajibisha wanaume waliowapa mimba? Ni kina dada wa wapi hao uliowaona hivyo? Una statistics gani za ku support haya?

Unaweza kuwa institution ya mambo haya wewe kama unaweza ku support statements zako.

Usije tu kuangalia sample space ya types za mtaani kwenu ukaja na generalization hapa.

Tueleze vizuri.
Hebu ngoja nilale kwanza maana naona unataka kulianzisha kama kawaida yako....Nitakujibu kesho.

Usiku mwema.............
 
Kwa nini hawataki kuwawajibisha wanaume waliowapa mimba? Ni kina dada wa wapi hao uliowaona hivyo? Una statistics gani za ku support haya?

Let me vouch for Mtambuzi. Mimi ninao binamu kadhaa (wa kike) ambao wamezaa watoto na kwenda kuwarundika kwa mama zao (bibi wa watoto).

Kuna mmoja karundika wanae watatu kwa mama yake (shangazi yangu/bibi wa wanae). Alizaa mara ya kwanza tukadhani ni bahati mbaya na atajifunza, wapi. Akapeleka mtoto kwa shangazi, baba wa mtoto hajulikani alipo, shangazi akawa mlezi asilimia 100.

Mara ya pili tena akapigwa kibendi akazaa, mzunguko ule ule ukajirudia. Mtoto analelewa na shangazi hadi leo hii. Mara ya tatu hivyo hivyo. Baba wa hawa wawili wanajulikana lakini hata hajishughulishi nao kuhusiana na wanae.

Sasa hivi ni mjamzito tena na anaishi na mwanaume. Hao wanae watatu wanaoishi kwa shangazi hajui wanakula nini, hajui shuleni wamesoma nini kwa sababu haishi nao na wala hajishughulishi katika maisha yao ya kila siku.

Hatoi mchango wowote ule wa kifedha. Hela za nguo, sare za shule, karo, na mahitaji mengine hatoi kama inavyopaswa hivyo majukumu yote hayo yanamuangukia shangazi.

Yeye kazi yake ni kula starehe tu na wanaume zake huko. Hata huyu mwanaume aliyenaye sasa wamekutana huko huko kwenye maviota ya starehe.

Unaweza kuwa institution ya mambo haya wewe kama unaweza ku support statements zako.

Usije tu kuangalia sample space ya types za mtaani kwenu ukaja na generalization hapa.

Tueleze vizuri.

Kwa hiyo kwa maongezi tu ya kawaida kama hapa jamvini sidhani kama mtu anahitaji kuja na takwimu za tafiti rasmi kama ulivyohoji.

Ni mambo yaliyo kwenye familia za kutosha kabisa (kiidadi) kuweza kuwa ni moja ya mambo yanayojulikana kwa uwazi.
 
hao wazazi ndo wanapenda kujiletea mizigo upendo gani wa kubebeshana mizigo wakati wazazi wao wako hai,inategemea na familia uliyotoka aisee kama kwetu huwezi kwenda kumuachia mama mtoto labda umpeleke kusalimia baada ya mda fulani unamchukua na pia anaenda na mlezi, hako katabia kakuendekeza kulea wajukuu wakati mama zao wanakula bata ni ujinga na hiyo inasababisha mabinti wengi wanarukaruka na kuzaa ovyo wakijua bibi na babu wapo watalea.

Unachosema ni kweli kabisa lakini kumbuka watu tumetofautiana haiba. Kuna wengine kwa asili ni wapole na wenye huruma sana na wazo la kukataa wajukuu wanaliona ni baya sana kwa sababu hao wajukuu kwanza si kosa lao na pili ni damu yao kabisa.

Sasa wakiyaweka hayo yote kwenye mlinganyo inawawia vigumu sana kukataa kuwatunza wajukuu wao ilhali wakijua wakikataa kufanya hivyo basi hao wajukuu watahangaika zaidi na kuteseka zaidi.
 
watateseka vipi kama wazazi wao wako hai,hii mambo tunayaendekeza wenyewe matokeo yake unakuta bibi analea wajukuu zaidi ya watano hana mbele wala nyuma hayo si ndo mateso kwa watoto,mama anapotunza watoto wake kwa shida ndipo anapopunguza kukata nyonga kwa kasi maana anajua mzigo ulivyo mzito,bora nionekane sina huruma kuliko kupeana majukumu mazito mazito kama haya wakiwa yatima nitalea tofauti na hapo no no no.
 
Kwa nini hawataki kuwawajibisha wanaume waliowapa mimba? Ni kina dada wa wapi hao uliowaona hivyo? Una statistics gani za ku support haya?

Unaweza kuwa institution ya mambo haya wewe kama unaweza ku support statements zako.

Usije tu kuangalia sample space ya types za mtaani kwenu ukaja na generalization hapa.

Tueleze vizuri.

ktk hali ya kawaida hili jambo ni common sana sio kila kitu mpaka iletwe statistics ndo ikuingie akilini kwani we umekulia Europe kwamba hiki kitu ni kigeni maskioni na machoni kwako.
 
mada nzuri Mtambuzi mie naona iko safe zaidi kupeleka watoto kwa wazee kuliko kuwaacha na housegal,..........................tatizo siku hizi kwao imekuwa mzigo kwa sababu hawaachiwi hela ya kutosha au pengine wanachoka sana,mie nashauri kama unapeleka watoto kwa bibi peleka hela ya matunzo na pia kama una uwezo muwekee hoiuse maid yeye awe msimamizi tu, wenyewe walikulea kwa tabu leo uzeeni unataka uwachoshe pia????ila hii mada kwa nini umelenga wanawake tu? au kwa vile ndio wanaoshinda na watoto nyumbani?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom