DADA YENU MAPENZI YAMENIKABA KOO

DADA YENU MAPENZI YAMENIKABA KOO

Sababu kubwa wanajua mapenzi, wametulia na kukua kiakili kimwili na kiroho na hawasumbui ka vijana, na wanajua wanacho kitaka. So ku date nao raha sana haya ya uchumi kila mtu hujishugulisha
Wanawake hivi ni kweli huwa mnaamini kwenye akili zenu wanaume waliowazidi umri hasa mkubwa ndiyo wazuri kwa mapenzi kwasababu wametulia au ni sababu za kiuchumi?
 
Muoaji huwa haonji hafu mi huyo ananiheshimu hataki ngono huyo ndo naweza mu consider mume walah. Wahuni wenzangu tutabanjuka tu
Dada shikilia msimamo wako huo huo me nilisomaga ma ushauri ya huku ooh unabania bania nn kiliwe na nyerere hatimaye nkaachie wakt namaliza chuo mwaka wa tatu

Ila me nashukuru wa kuoa wanajitokeza wengii tu na hao wakuoa ndo ata hawajanionja
 
Habari za weekend wanajamvi..

Mimi ni member mzoefu,nmeona nitumie ID mpya ili niwe huru zaidi kujielezea...nmefikwa kooni nahitaji ushauri

Mm ni mtu mwenye msimamo wa dini na nina misimamo yangu ya maisha,nashkuru Mungu nimesoma vzuri na nina kazi nzuri... (sio slay queen)..Anyways,,binafsi kwa mara ya kwanza kabisa nmeanza kujihusisha na mahusiano nilikua chuo mwaka 2 kuingia wa3...(field),,,Nilikutana na kijana na hapo ndio ilikua mwanzo wa mahusiano na mwanzo wa hata ku-kiss
Mahusiano yale yalidmu miezi kadhaa na nliyaacha baada ya kugundua yule mwanaume hakuwa wa dini yangu (alinidanganya dini)...na mm mtu wa hvo naona hatutafika mbali na mm sipendi kua na mahusiano yasio na future....uzuri ni kwamba sikusex nae

Sikujihusisha tena na mahusiano mpka nkamaliza chuo,nkawa kitaa nasaka ajira...nikakutana na mkaka wa makamo,,nikaona at least huyu age yake imeenda labda kweli anataka ku-settle down...
tulikaa kwenye mahusiano kwa muda wa miezi kama 7..huyu kaka nilimkuta na watoto wawili wa mama tofauti...mama wa mtoto wa kwanza alishaolewa,ana familia yake..mama wa mtoto wa pili walikua wameachana na huyu kaka alikataa mimba (kwamba hawakua na makubaliano ya yule dada kubeba mimba ila m.ke aliilengesha)...

Ukweli huu alinambia mwanzo kabisa akiwa ananitongoza,,basi me nkajua ntaweza yavumilia,,mahusiano yetu yalikua mazuri lakini likija swala la kuombwa mechi me nkawa nakaza..jamaa akawa ananiambia sasa tutakuaje kimahusiano kama kaka na dada?!,,,nkamwambia mm siwezi kulala na wewe... (siamini katika sex before ndoa)...akawa ananambia inabdi kwanza nizae au kama nikunioa basi niwe na mimba ila yeye hawezi uziwa mbuzi kwenye gunia...tuliendaaaaa ikafika point nkaona kabisa haya mahusiano nayalazimisha!,basi kila mtu akashika shughuli zake...

Akawa ananitafuta siku moja moja (hakutaka kuamini kweli naweza mkatalia kusex),basi tukionana hakuna jipya msimamo wangu ni ule ule..

Nkapata kazi nkapangiwa mkoa wa mbali na jamaa,,mawasiliano yetu yakaena yakawa yanafifia kabisaa..ila akawa kila akija mkoa niliopo ananitafuta (nature ya kazi yake anasafiri sana)..

Nkamwambia yaan wew siku zote huniuliziagi ila mpaka uje huku...anazuga na sababu zisizo za msingi..

Siku moja nkaona amepost picha ya mtoto (nikajua ni yule mtoto aliemkataaga),,kama vile wameelewana na yule mzazi mwenzie...basii siku aliokuja mkoa niliopo,,nkamuuliza akasema mm nmefata mtoto ila yule mwanamke sijarudiana nae...lakn yule mwanamke anacoment kabisa kwenye picha zake mara mume,mpenzi,kiboko yangu n.k....ikifika birthday ya m.ume mdada atajishughulisha cake na mazawadi kedekede...

anakuja huku nilipo anakataa hawajarudiana ila inta unaona yule mwanamke na the guy wameenda trip zanzbr na mtoto...hio siku nikanyanyua mikono juu nkasema hapa sina hata matumaini..nkawa mkali kwa jamaa nkamwambia tafadhali naomba ukija huku nilipo fanya yaliyokuleta usepe...nkawa mkali...nkafuta namba zake...akawa hata akinitext whatsapp simjibu!

sasa nkakaa kama miezi 8 au 9..nkajaribu mahusiano mengine...nafs yangu inakua ngumu kumuamini mwanaume tena!,naona uongo umezidi kiasi kwamba huyu mwanaume akanambia mm sionyeshi kumpenda na sina feelings nae (kilichoni dissapoint kwa huyu kaka ni na yeye ana watoto na hakuniambia before...)na mm nkapunguza mawasiliano na last week tukaachana kabisa..baada ya kujua ana watoto mzuka ule wa mahusiano ukafa..sitaki baby mama dramas

Nafsi yangu kusema ukweli ilimpenda sana sana sanaa huyu kaka mwengine ambae amaerudiana na baby mama wake (na hawaezi oana dini mbalimbali kabisaaaa),,...ila mwanamke sa hvi ni mjamzito anazaa mtoto mwingine baada ya miaka 8

Nafsi yangu ina maumivu makali sana jaman,nifanyaje nisahau na niweze move on?,!,yaan nmeshalia sana sana kwa Mungu wangu,kumuomba aniwezeshe nisahau jaman...

Nisaidieni wanajamvi..ni kweli kabisa siwezi pata mwanaume atakaekubali mvumilia mwanamke mpka amuoe?!,, Nahisi subira yangu ya kujitunza uanamke wangu inanishinda (Im 26 now)...,

Na pili huyu mwanaume namtoaje akilini jaman?!...

NB::: comments ntazisoma kupitia account yangu ya kawaida hapa nimemaliza...nmetumia hii ili nijimwae mwae...
biashara hiyo haipo dada mboga ikipikwa lazima uweke chumvi kujua kama inatosha kwa matumizi lazima uonje zama zimebadilika! hata nguo unaposhona lazima upimwe kujua size yako!usipoteze mda fanya kama alivyokwambia
 
Hivi najihesabu vip namimi nilikua kwenye mahusiano na mtu na wakati sijapata tunda. Huyo naona ni kama rafiki ambaye alinitunuku tubusu busu tu. Hongera kwa msimamo wako ila hata mimi sioi mpaka nipate tunda.
 
Jaribu kulegeza kidogo misimamo utakosa wachumba kwa sababu ya kubana sana papuchi. Hebu nikuulize miaka 26 ni msichana mkubwa na ushavunja ungo je hamu zako unazimalizaje?
 
Je umewahi kulala na mwanaume? Namaanisha kuzini. Kama bado basi MUNGU atakupa wako. Kama tayari basi mfuate huyo uliyezini naye mara ya kwanza akakutoa bikira ndio mumue wako. Sisi na sie tuko na wale tuliowatoa bikira wale walioachwa na watu huwa tunawapitia tu
 
Ila wanawake wengi hampo tayari kuanzia chini na vijana wenzenu...sizungumzii wewe 28 na yeye 28.

kila kilicho na msingi huwa imara...biashara, nyumba,elimu, n.k
Hahahaha hatuwez fananisha mahusiano na elimu,biashara etc
Vijana hamjielewi mkivumiliwa nyie mnachukilia kama fursa ...akipata huyo anaoa mwingine wewe anakuona unakasoro/mapungufu
Mahusiano na vijana ni kama kucheza biko
 
Nadhani unaamini ni sababu za kifedha Ila ni zaidi ya hiyo.
Afu hawaelewi pesa ni mwanzoni tu , ukishaanza kupendana wala huwez kumchuna ila unampenda yeye kama yeye.....na kama akikuchukulia poa kisa pesa zake unaliacha tu
Mahusiano ni zaidi ya pesa
 
Hahahaha hatuwez fananisha mahusiano na elimu,biashara etc
Vijana hamjielewi mkivumiliwa nyie mnachukilia kama fursa ...akipata huyo anaoa mwingine wewe anakuona unakasoro/mapungufu
Mahusiano na vijana ni kama kucheza biko
Im telling you.

Jaribu kufanya kila jambo lolote bila kujenga foundation ya kutosha uone...litakuangusha.


Wengi mnapenda kuvuna kwenye mapenzi ilihali hamtaki kulima kupanda na kupalilia...You need to struggle, sweat... Jenga msingi wa mahusiano anzia chini...

Ukianzia chini chances za kukwaruzana kwa mambo madogo ni chache...Mnakuwa mnajuana vya kutosha na ukiona viahatarishi maamuzi yanakuwa sio tatanishi.
 
Back
Top Bottom