DADA YENU MAPENZI YAMENIKABA KOO

DADA YENU MAPENZI YAMENIKABA KOO

Dini gani Wewe?
By the way jitunze utapata aliye bora
 
Habari za weekend wanajamvi..

Mimi ni member mzoefu,nmeona nitumie ID mpya ili niwe huru zaidi kujielezea...nmefikwa kooni nahitaji ushauri

Mm ni mtu mwenye msimamo wa dini na nina misimamo yangu ya maisha,nashkuru Mungu nimesoma vzuri na nina kazi nzuri... (sio slay queen)..Anyways,,binafsi kwa mara ya kwanza kabisa nmeanza kujihusisha na mahusiano nilikua chuo mwaka 2 kuingia wa3...(field),,,Nilikutana na kijana na hapo ndio ilikua mwanzo wa mahusiano na mwanzo wa hata ku-kiss
Mahusiano yale yalidmu miezi kadhaa na nliyaacha baada ya kugundua yule mwanaume hakuwa wa dini yangu (alinidanganya dini)...na mm mtu wa hvo naona hatutafika mbali na mm sipendi kua na mahusiano yasio na future....uzuri ni kwamba sikusex nae

Sikujihusisha tena na mahusiano mpka nkamaliza chuo,nkawa kitaa nasaka ajira...nikakutana na mkaka wa makamo,,nikaona at least huyu age yake imeenda labda kweli anataka ku-settle down...
tulikaa kwenye mahusiano kwa muda wa miezi kama 7..huyu kaka nilimkuta na watoto wawili wa mama tofauti...mama wa mtoto wa kwanza alishaolewa,ana familia yake..mama wa mtoto wa pili walikua wameachana na huyu kaka alikataa mimba (kwamba hawakua na makubaliano ya yule dada kubeba mimba ila m.ke aliilengesha)...

Ukweli huu alinambia mwanzo kabisa akiwa ananitongoza,,basi me nkajua ntaweza yavumilia,,mahusiano yetu yalikua mazuri lakini likija swala la kuombwa mechi me nkawa nakaza..jamaa akawa ananiambia sasa tutakuaje kimahusiano kama kaka na dada?!,,,nkamwambia mm siwezi kulala na wewe... (siamini katika sex before ndoa)...akawa ananambia inabdi kwanza nizae au kama nikunioa basi niwe na mimba ila yeye hawezi uziwa mbuzi kwenye gunia...tuliendaaaaa ikafika point nkaona kabisa haya mahusiano nayalazimisha!,basi kila mtu akashika shughuli zake...

Akawa ananitafuta siku moja moja (hakutaka kuamini kweli naweza mkatalia kusex),basi tukionana hakuna jipya msimamo wangu ni ule ule..

Nkapata kazi nkapangiwa mkoa wa mbali na jamaa,,mawasiliano yetu yakaena yakawa yanafifia kabisaa..ila akawa kila akija mkoa niliopo ananitafuta (nature ya kazi yake anasafiri sana)..

Nkamwambia yaan wew siku zote huniuliziagi ila mpaka uje huku...anazuga na sababu zisizo za msingi..

Siku moja nkaona amepost picha ya mtoto (nikajua ni yule mtoto aliemkataaga),,kama vile wameelewana na yule mzazi mwenzie...basii siku aliokuja mkoa niliopo,,nkamuuliza akasema mm nmefata mtoto ila yule mwanamke sijarudiana nae...lakn yule mwanamke anacoment kabisa kwenye picha zake mara mume,mpenzi,kiboko yangu n.k....ikifika birthday ya m.ume mdada atajishughulisha cake na mazawadi kedekede...

anakuja huku nilipo anakataa hawajarudiana ila inta unaona yule mwanamke na the guy wameenda trip zanzbr na mtoto...hio siku nikanyanyua mikono juu nkasema hapa sina hata matumaini..nkawa mkali kwa jamaa nkamwambia tafadhali naomba ukija huku nilipo fanya yaliyokuleta usepe...nkawa mkali...nkafuta namba zake...akawa hata akinitext whatsapp simjibu!

sasa nkakaa kama miezi 8 au 9..nkajaribu mahusiano mengine...nafs yangu inakua ngumu kumuamini mwanaume tena!,naona uongo umezidi kiasi kwamba huyu mwanaume akanambia mm sionyeshi kumpenda na sina feelings nae (kilichoni dissapoint kwa huyu kaka ni na yeye ana watoto na hakuniambia before...)na mm nkapunguza mawasiliano na last week tukaachana kabisa..baada ya kujua ana watoto mzuka ule wa mahusiano ukafa..sitaki baby mama dramas

Nafsi yangu kusema ukweli ilimpenda sana sana sanaa huyu kaka mwengine ambae amaerudiana na baby mama wake (na hawaezi oana dini mbalimbali kabisaaaa),,...ila mwanamke sa hvi ni mjamzito anazaa mtoto mwingine baada ya miaka 8

Nafsi yangu ina maumivu makali sana jaman,nifanyaje nisahau na niweze move on?,!,yaan nmeshalia sana sana kwa Mungu wangu,kumuomba aniwezeshe nisahau jaman...

Nisaidieni wanajamvi..ni kweli kabisa siwezi pata mwanaume atakaekubali mvumilia mwanamke mpka amuoe?!,, Nahisi subira yangu ya kujitunza uanamke wangu inanishinda (Im 26 now)...,

Na pili huyu mwanaume namtoaje akilini jaman?!...

NB::: comments ntazisoma kupitia account yangu ya kawaida hapa nimemaliza...nmetumia hii ili nijimwae mwae...
Unahofia nn kuvua kivazi au walikufanyia FGM so unaona noma? Hata tunaponunua kitabu lazima ukague muonekano wa maandishi, mpangilio wa karatasi na mkolezo wa wino.
 
Back
Top Bottom