Dada yake MBOWE aikacha CHADEMA ajiunga na CCM!!

Dada yake MBOWE aikacha CHADEMA ajiunga na CCM!!

Tuwakimbie waiwaji kwa kasi kubwa, hadi 2015, yabaki yenyewe ili tuyatambue yaone aibu
 
Ritz hawezi kuchangia hoja yoyote ya madawa ya kulevya hata meno ya tembo kwani wanaofanya kazj hizo ni mababu zake Wa ukoo Wa magamba
Wewe unawezavkuchangia hoja ya nyie kumwagia watu tindikali, kuwalisha sumu na kujilipua mabomu ili mpate huruma ya wananchi?
 
Wakati Mwenyekiti wa taifa CHADEMA mh Freeman Mbowe na baadhi ya Wabunge wakihojiwa na jeshi la polisi mkoani Iringa kwa kile kinachodaiwa na jeshi hilo ni kupitiliza muda wa kuhutubia ktk mkutano uliofanyika siku ya jumamosi, Dada yake na Mbowe GRESI MBOWE,ameamua kuikacha CDM na hatimae kujiunga na CCM!!

SOURCE; Gazeti la Uhuru (Radio Free Afrika)

Mbowe ni jina la ukoo kama ilivyo Mushi,Kimaro,Tarimo,Kereti,Mrema n.k.
 
Hakuna Dada wa Mbowe ambaye ni Mmpumbavu kiasi hicho. Grace Mbowe ni dada wa afande Gervace Mbowe OCS wa Makuyuni aliyewasaidia wasomali kumpiga mbunge Nassari. Hawana uhusiano wowote na Freeman Mbowe

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Kimsingi Chadema ni chama cha kifamilia hilo lipo wazi wala haliitaji PhD kulitambua.

Mmiliki wa Chadema ni Mtei, na Mwenyikiti wa Chadema ni Mbowe, ambaye ni mkwe wa Mtei,

Kuna uwezekano mkubwa wa kimaslahi ndani ya familia ndiyo maana Grace Mbowe, kuamua kuondoka Chadema na kwenda CCM.

Tutasikia mengi pindi Grace Mbowe, atakapofunguka zaidi.

Mkuu Ritz baada ya Mtei kung'atuka alifuatia Mbowe?naomba unijibu tuwe wakweli,nirudi katika mada sio Habari,kipindi kile mtoto wa nyerere alipokua upinzani ndo ilikua Habari
 
Kwani umeambiwa CHADEMA ni chama cha familia!?? let her go. Hata babaake Mbowe alikuwa ccm, na Mtei pia
Ukoo wa tundu lisu upo bungeni kwa kupeana, ukoo wa ndesamburo upo bungeni kwa kuzawadiana na hata ukoo wa mbowe umezawadiwa uenyekiti kutoka ukweni
 
Dada yake Mbowe kajitambua, ameona haiwezekani akili ndogo iongoze akili kubwa.

Hongera sana Grace Mbowe.

Kama nyumbani wanamkataa Mbowe, kulikoni.

Wewe kaa Huko Huko ulipo, baba,mama, watoto chama kimoja hakuna anayefikiri zaidi ya hapo!

uwezo wa kufikiri wa familia yako ni kutiliwa Mashaka, hakika mpo Kwenye ukoo wa panya Kila mtu mwizi,

mwisho wenu ni aibu tu subirini 2015.
 
Mbowe ni jina la ukoo kama ilivyo Mushi,Kimaro,Tarimo,Kereti,Mrema n.k.

Usitake kupoteza mada kubali ukweli, ni dada yake toka ni toke, baba na mama mmoja.

Link hii hapa kasome: http://www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/15665-dada-wa-mbowe-atimkia-ccm

Hapa kuna mawili, yawezekana kaka kakiuka makubaliano au dada kauona ukweli kuwa chama hakina mwelekeo wa kuchukua nchi 2015 so kaona aanze mapema.
Ukiisoma vizuri kule Hai (dada alikorudisha kadi) mwenyekiti wa CCM anasema Jan - Aug 2013 tayari wana-CDM 550 wamerudi CCM. Wamewastukia wapiga dili wa CDM!!
 
Kimsingi Chadema ni chama cha kifamilia hilo lipo wazi wala haliitaji PhD kulitambua.

Mmiliki wa Chadema ni Mtei, na Mwenyikiti wa Chadema ni Mbowe, ambaye ni mkwe wa Mtei,

Kuna uwezekano mkubwa wa kimaslahi ndani ya familia ndiyo maana Grace Mbowe, kuamua kuondoka Chadema na kwenda CCM.

Tutasikia mengi pindi Grace Mbowe, atakapofunguka zaidi.

Grace Mbowe hana uhusiano na Freeman Mbowe. Grace ni dada wa afande Gervas Mbowe ambaye naye hana uhusiano na Freeman Mbowe

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Hakuna Dada wa Mbowe ambaye ni Mmpumbavu kiasi hicho. Grace Mbowe ni dada wa afande Gervace Mbowe OCS wa Makuyuni aliyewasaidia wasomali kumpiga mbunge Nassari. Hawana uhusiano wowote na Freeman Mbowe

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
Leo mtasema yote lakini mwisho wa siku dada yake Mbowe karudi CCM.
 
Grace Mbowe hana uhusiano na Freeman Mbowe. Grace ni dada wa afande Gervas Mbowe ambaye naye hana uhusiano na Freeman Mbowe

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
Wewe ndiyo msemaji wa ukoo wa Mbowe?
 
Ben Saanane,

Kwa hiyo unataka kutuambia Grace Mbowe siyo dada yake Freeman Mbowe? ni majina tu.

Mkuu umeulizwa Guangzhou kupitia Islamabad na Doha unaenda lini? Mimi binafsi nakuaga kabisa manake wachina kama sio waarabu watakunyonga muda sio mrefu kama wanavyonyonga magamba wenzio kila uchao; tuta-miss "busara" zako hapa jamvini. Buriani kaka.
 
Hakuna Dada wa Mbowe ambaye ni Mmpumbavu kiasi hicho. Grace Mbowe ni dada wa afande Gervace Mbowe OCS wa Makuyuni aliyewasaidia wasomali kumpiga mbunge Nassari. Hawana uhusiano wowote na Freeman Mbowe

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Ikiwa ndivyo ilivyo basi naamini kuwa lengo la mhariri wa gazeti hilo la uhuru ni kujaribu kutafuta njia ya kuweza kupata wasomaji wengi,kwani kwa sasa gazeti la uhuru huishia kufungiwa mandazi mtaani.

Pia ikumbukwe kwamba gazeti lolote ukiliondoa Tanzania daima,na Mawio bila kuweka vichwa vya habari vinavyoitaja CHADEMA au Viongozi wake halipati wasomaji!!
 
DADA wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Grace Mbowe, amejiunga na Chama Cha Mapinduzi ( CCM) akitokea Chadema, kwa kile alichodai haoni jambo jipya katika chama hicho.

Grace amesema amehama kutokana na kuwepo propaganda zisizotekelezeka. Hata hivyo, amesisitiza kwamba kuwepo kwake katika Chadema, siyo kwa sababu ya familia.

Alikabidhi kadi hiyo jana kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Hai. Alisema itikadi za kisiasa, zisihusishe masuala ya kifamilia, kwani upendo wao uko pale pale.
Alisema kilichomfanya kujiunga na chama hicho ni utashi wake. Alidai Chadema wanafanya propaganda za kuwadanganya wananchi.

Alisema itikadi za chama, haziwezi kuingilia masuala ya kifamilia, hivyo kwake siyo ajabu kuondoka Chadema, kwani kila mtu ana utashi wake wa kisiasa.

"Nimeamua kwa hiari yangu mwenyewe bila kushawishiwa na mtu, ndio maana nimetoka Dar es Salaam kuja Hai kwa ajili ya kurejesha kadi ya Chadema na kujiunga na CCM, suala la itikadi lisihusishe masuala ya kifamilia kwani upendo wetu upo palepale,"alisema Mbowe.

Alisema, "kuwapo kwangu Chadema siyo kwa sababu ya familia, hivyo hakuna wa kunizuia, natoka kwa utashi wangu, na tutaendelea kuheshimiana na mdogo wangu Freeman Mbowe katika masuala ya kifamilia."

"Freeman Mbowe ni mdogo wangu wa kuzaliwa kabisa, hakunishawishi kuingia Chadema, hivyo sioni haja ya kuendelea kubaki huku wakati sioni jambo jipya, mimi tangu naifahamu CCM iko vile vile, bali propaganda za upinzani ndizo zinawalaghai wananchi," alisema.

Aliviasa vyama vya siasa, kuwa sasa umefika wakati wa kuacha malumbano na maandamano ya itikadi, yasiyokuwa na faida yoyote, badala yake huu ni muda wa kujenga nchi kwa ushirikiano.

Awali, akipokea kadi ya Chadema, Katibu wa CCM Wilaya ya Hai, Hassan Mtenga alisema alichokifanya Grace ni uamuzi wa busara, baada ya kutazama Chadema ilipo na inapokwenda.

Alisema wimbi la wanachama wa Chadema kurudisha kadi na kujiunga na CCM, limekuwa kubwa wilayani Hai. Alisema tangu Januari hadi sasa amepokea wanachama 530.

Mtenga aliwataka wananchi kutambua kwamba Jimbo la Hai, siyo kitovu cha upinzani bali Chadema ni chama kilichotoa upinzani kwa CCM katika uchaguzi mkuu wa 2010. Alisema hali hiyo, ilitokana na makundi ya CCM.

Alisema kwa sasa watu asitarajie tena suala hilo kutokea.

Chanzo: HABARI LEO
 
Safi sana, sasa anasubiriwa mbowe mwenyewe

Nampongeza sana kwa kuondokana na wamwagia watu tindikali

Ni huo huo ukoo unaotaka kuukwepesha na ukweli. Ukoo wa freemason aikaeli mbowe

Mkuki kwa nguruwe, mtasema yote mwaka huu

Tuwakimbie waiwaji kwa kasi kubwa, hadi 2015, yabaki yenyewe ili tuyatambue yaone aibu

Wewe unawezavkuchangia hoja ya nyie kumwagia watu tindikali, kuwalisha sumu na kujilipua mabomu ili mpate huruma ya wananchi?

Virus detected!

Ukoo wa tundu lisu upo bungeni kwa kupeana, ukoo wa ndesamburo upo bungeni kwa kuzawadiana na hata ukoo wa mbowe umezawadiwa uenyekiti kutoka ukweni

Dj zero sio kichwa mkuu, rekebisha hiyo
Wewe jamaa lazima utakuwa ni kichaa huwezi kupangilia hoja zako kila siku tindikali huna jipya jitambue
 
Mkuu umeulizwa Guangzhou kupitia Islamabad na Doha unaenda lini? Mimi binafsi nakuaga kabisa manake wachina kama sio waarabu watakunyonga muda sio mrefu kama wanavyonyonga magamba wenzio kila uchao; tuta-miss "busara" zako hapa jamvini. Buriani kaka.
Dada yake Mbowe aikacha Chadema ajiunga na CCM.
 
Dada yake Mbowe kajitambua, ameona haiwezekani akili ndogo iongoze akili kubwa.

Hongera sana Grace Mbowe.

Kama nyumbani wanamkataa Mbowe, kulikoni.

hivi siyo mchaga maana wachaga wote wako chadema..kwa mjibu wa Nape NNAUYE
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom