Cyrilo: Kukamatwa kwa ndege na mikurupuko ya Prof. Kabudi na kutojua sheria za SADC. Je, kutishwa na kumtimua ndio alipendekeza Kabudi?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Rafiki yangu Yericko Nyerere ameandika kwenye kitabu chake cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi, umuhimu wa kupeana taarifa (za maana) baina ya mahakama, wizara ya mambo ya ndani na idara zake... Hapa ni katika kuboresha tasnia ya usalama wa taifa.

Mimi naamini kama taasisi ya Urais (ikulu), wizara ya mambo ya ndani na idara zake pamoja na mahakama wangeshirikana kwa kupeana taarifa- (bila kuathiri haki za kiraia) ndege yetu isingekamatwa na Mkulima Hermanus huko J'burg - SA.

Kumbe, kesi iliyotolewa hukumu na mahakama kuu ya nchi moja mwanachama wa SADC inaweza kusajiliwa na hukumu hiyo ikatekelezwa na mahakama kuu ya nchi nyingine mwanachama wa jumuia ya SADC. Ndio maana mkulima Hermanus aliamua kusajili hukumu ya kesi ya mahakama kuu ya Tanzania iliyoamuru alipwe fidia ya pesa zake, akaisajili huko J'burg Afrika kusini - kwa kufuata kanuni za jumuia ya SADC.

Swali?
Waliomfutia uraia na kumzuia Hermanus asiingie nchini - (bila shaka walilenga kumdhulumu madai yake) Je! Hawakujua kama angeweza kusajili hukumu ya mahakama kuu ya Tanzania katika mahakama kuu ya Gauteng - Afrika Kusini?

Je! Hakuna mtu miongoni mwa watoa maamuzi aliyejua kanuni hii ya SADC?

Kuna mtu anaitwa Profesa Kabudi Paramaganda, waziri wa mambo ya nje na mwenyekiti baraza la mawaziri wa nchi za SADC. Mapema mwezi Agosti alitawala vyombo vya habari akionekana kuhubiri kwenye mimbari za mkutano wa SADC, na zaidi ya hapo ni mbobezi wa sheria. Huyu ameshiriki kikamilifu kumfutia uraia Bwana Hermanus.

Je! Profesa Kabudi, kwa nafasi hizo alizokuwa nazo hakujua kanuni hii ya SADC?

Hakuna namna ya Profesa Kabudi kuepuka lawama kwenye jambo hili. Uzalendo uchwara wa kukurupukia mambo unatugharimu sasa - tunakwenda kulipa gharama kubwa kwa mkupuo. Mkulima amekuwa akidai deni kwa miaka 37, hiyo subira ni ya kimalaika - lakini awamu ya tano ikamuona msumbufu, ikamfutia uraia wake wa kuasili na kumzuia kuingia nchini. Lengo ni nini kama sio kumdhulumu? Au kama ana makosa mengine kwanini asishitakiwe?

Imekula kwetu. Taarifa kutoka J'burg zinadai kuna namna mbili tu ya kuipata ndege yetu Aribus 220-300 yenye thamani ya dola 90 milioni; Moja ni kumlipa Hermanus fedha zake zote kwa mkupuo, Pili ni kuweka dhamana ya mali yenye thamani sawa au zaidi ya deni analodai Hermanus. Hakuna kitu watafanya wanasheria wa serikali ya Tanzania waliokwenda South Afrika zaidi ya kupiga selfie. Hivyo yani.

Next time, jambo linalogusa mahakama, mambo ya nje, mambo ya ndani na idara zake, liamuliwe baada ya majadiliano na kupeana taarifa kutoka pande zote husika.
Wapo watu walijua kinachoweza kutokea lakini wakisema tu! wanaitwa wasaliti, maadui...ooh sio wazalendo! Sasa tukome kukurupuka.
FB_IMG_1567086394273.jpg
 
Rais wetu mpendwa ni vyema ukamtimua kazi Prof Kabudi, inaonekana anajua sana theory na anataka kuleta theory in real life, Makinikia hatuelewi aliishia wapi, Korosho na wale wakenya wakamuingiza chaka, hili la ndege pia chaka..

Huyu Prof inawezekana ni mzuri sana kwenye kufundisha lakini sio kwenye uhalisia wa mambo huku duniani..
 
Kuna wimbo huwa wanaimba watoto unaitwa mchimba kisima kaingia mwenyewe. Hili tumeingia wenyewe ndani ya kisima. Tumelizua jambo, tukatumia mahakama zetu kulihukumu, tukampangia fidia kiduchu, alipolalamika akaishia kupigwa ban asiingie nchini.
Tumekaingia katika makubaliano ya kikanda. Tukaipeleka ndege SA, bahati haikutumiwa na viongozi au timu yetu ya Taifa, ameikamata. Muda huu tunahangaika yeye anapiga mvinyo taratiiiiibu. Nani mjanja, sisi au yeye?
 
Mkuu nakubaliana na karibia 80% ya yote uliyo ongea na kushauri.

Hiyo 20% iliyobaki naomba ufafanuzi kuna tofauti gani za kiutendaji kati ya IDARA YA USALAMA WA TAIFA na SHIRIKA LA UJASUSI?

Nini kinashindikana utekelezaji wake kisheria au kimuundo wa utendaji chini ya IDARA YA USALAMA lakini kitawezekana ndani ya SHIRIKA LA UJASUSI?

Ukitoa ufafanuzi hapo utakuwa umetufumbua wengi na utakuwa umewasaidia uliokusudia kuwasaidia ushauri yaani serikali.

NB: Kuna uwezekano hizo tofauti na changamoto zimeelekezwa ktk kitabu cha Yericko Nyerere, mimi sijakisoma na naamini wengi hawajakisoma kutokana na sababu tofauti mfano namna ya kukipata pale ulipo, gharama, n.k.
 
Professa K anatakiwa atoe ufafanuzi kwani shutuma juu yake ni nzito na kama kweli ndiye aliyetufikisha hapa kwa kumzuia jamaa kuingia Tz na kushauri malipo yakome basi anatakiwa ajitathmini (sidhani kama yule alyemtoa jalalani atafanya hivyo-kumuwajibisha).
Uzalendo unatakiwa uende na sheria hasa ukichukulia kuwa tuna aminishwa ya kuwa huyu ni mbobezi katika sheria.
 
Back
Top Bottom