Cyprian Kachwele wa Azam FC atua Vancouver Whitecaps FC Canada

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,308
24,200
24 November 2023
Vancouver, Canada

Mshambuliaji hatari wa Azam FC, Cyprian Kachwele umri miaka 18 amesainiwa katika klabu ya Vancouver Whitecaps FC
1700936272200.png

Taarifa ya klabu hiyo ya Canada inayoshiriki katika ligi ya Major League Soccer ya Marekani ya Kaskazini kupitia kocha mkuu Ricardo Clark inasema tayari wamemuingiza katika programu ya kuzoea mazingira mapya, na kumsaidia awaze kuanza katika timu ya kwanza ya klabu ya Vancouver Whitecaps FC
Cyprian Kachwele's first looks on the pitch Club Reporter, Sarita Patel, welcomes Whitecaps FC 2 newcomer Cyprian Kachwele and checks in with Head Coach Ricardo Clark.
Source : Vancouer Whitecaps FC

Ligi ya soka ya Marekani ya Kaskazini ya MLS ina wachezaji kadhaa maarufu kutoka mataifa mbalimbali duniani huku wengine wamecheza ligi kubwa za ulaya. Mfano wa mchezaji mwenye jina kubwa ni Lionel Messi mchezaji wa Inter Miami ambayo pia inashiriki ligi hiyo akiwa na wenzake kina Sergio Busquets, Jordi Alba na Javier "Chicharito" Hernadez mchezaji wa LA Galaxy aliyepitia Sevilla (LaLiga) Manchester United (Premier League) , Real Madrid (LaLiga) kwa kutaja kwa uchache

Toka maktaba:
Msimu ujao wa ligi ya MLS utaanza mwezi February tarehe 25, 2024. Pia timu ya Vancouver Whitecaps FC itashiriki michuano ya 2024 CONCACAF Champions cup inayoshrikisha timu za Marekani ya Kaskazini, Marekani ya Kati na Caribbean.
 
Kila la kheri kwake, akakaze tu, ukishatoboa huku, ukikaza kurudi nyumbani kutaka mwenyewe tu, atabaki anazunguruka timu kadhaa za huko.
Kiwango bora uwanjani + management nzuri= umeula.
 
Ni ajabu sana Tanzania ni ngumu sana mchezaji wa umri wa miaka 17 au 18 kuaminiwa kuchezea katika timu ya kwanza (first eleven) ya klabu za NBC premier league ya Tanzania, kina Mbwana Samatta historia inaonesha aliaminiwa na TP Mazembe ili kuweza kufika alipo kimataifa

Na huyu Cyprian Kachwele inaonesha atakuwa Centre forward tajwa duniani katika muda mfupi kaliba ya kina Romelu Lukaku wa Belgium , ana kila kitu cha kufikia ukubwa kwa kuwa, kama ilivyokuwa kwa Samatta ameonekana na Whitecaps FC ya ligi ya MLS ya Marekani ya Kaskazini na kuaminiwa nje akiwa na umri mdogo.

Photo: Romelu Lukaku Centre forward
1700883284258.png


Je, mababu zetu waliocheza miaka ya 1960, 1970, 1980 waliweza kuaminiwa kuchezea kikosi cha kwanza / first eleven timu kubwa za ligi kuu wakiwa na miaka 17, 18 kama ilivyo Marekani ya Kusini, Ulaya au na wao walikubaliwa wakati wakiwa tayari ma-Father kama kina Clatuos Chama, Reliants Lusajo n.k
 
Simba, Yanga, Namungo, Geita Gold bila kusahau National Team Taifa Stars muige mfano wa Vancouer Whitecaps kubaini vipaji vya vijana na kuwapa nafasi ktk timu zenu za kwanza / first eleven hata akiwa na umri wa miaka 16.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom