TANZIA Daktari Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa Azam FC) afariki dunia

Mjukuu wa kigogo

JF-Expert Member
Sep 19, 2023
201
438
Bwana Alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.Ameen

FB_IMG_1709055086340.jpg
---
Klabu ya Soka ya Azam, imetangaza kifo cha aliyekuwa daktari wa timu hiyo, Mwanandi Mwankemwa, kilichotokea leo jioni katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke.

Dkt. Mwankemwa alianza majukumu yake Azam FC, mwaka 2008, na katika kipindi chote cha utendaji wake, amehusika kuwasindikiza wachezaji katika matibabu ya ndani na nje ya nchi.

Mwankemwa aliingia katika udaktari michezoni mwaka 1982 na wakati huo alianza na timu JKT Ruvu.

Sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake yeye sote tutarejea.
 
RIP ,Dr. Mwamkenwa, such a gentleman, lovely father na amejitolea sana kulea vipaji vingi vya wanamichezo wetu,kuanzia wanariadhaa wa olimpiki hadi wanasoka wetu
 
Back
Top Bottom