Prosper C Manasse
JF-Expert Member
- Dec 8, 2015
- 635
- 692
Wazo Zuri Lakn Kumbuka Askari Wanaishi Sehemu1 Wakat Walimu Wanaishi Sehemu Tofauti Tena Si Kwa Umojamimi naona afadhali angefanya utaratibu wa kununua STAFF BUSES... Mbona wanajeshi asa hivi wana "military buses"
Lengo lake linaweza likawa zuri ila idea yake ya kufanikisha ilo lengo ndo utata unaazia apo....
Alaf ingekua poa zaidi kama ayo mabasi yanakua STAFF kwa wafanyakazi wa Manispaa nzima... inawezekana kabisa kufanikisha ilo jambo!!
Hawakulazimishwa, kama hawataki si waendelee kulipa nauli tu kwani Kuna shida?Sifa nyingine bwana ni hatari,sasa hata mwalimu hujaongea nae kama anashida ya nauli,unakurupuka tu ,unataka wasafiri bure kwenye daladala!!basi waambie wakachukue na mboga bure kariakoo!!!
Good comment!!!unajua watu wanaichukulia hii issue ni kama vile Amri imetolewa kumbe wala... asiye taka hachukui kitambulisho anayetaka anapewa ... take it as a favor mnapewa na wamiliki wa mabasi kutokana na mchango wenu kwa watoto wao na sio sheria
Mxee ndio nini?Ukuu wa wilaya kaupata kwa kudunda mxee wa watu mlitegemea nini
mkuu hata mimi nachukia juu ya kukurupuka kwa huyu mfuta viatu ila hapa nampaSifa nyingine bwana ni hatari,sasa hata mwalimu hujaongea nae kama anashida ya nauli,unakurupuka tu ,unataka wasafiri bure kwenye daladala!!basi waambie wakachukue na mboga bure kariakoo!!!
Kwa hiyo na askari ambao hawalipi nauli nao wamedhalilishwa??Nahc kama kunajambo ambalo makonda alishauriwa vibaya ni hili, swala la waalim kupanda magar buree ni unyanyasaji wa kijinsia, tena ni ubaguzi wa hali ya juu, na hii inataka kuchora pc kuwa waalim wanapata mshahara mdogo sana..
Hoja isingekuwa kuwasafirisha waalim bure ila wangetatua changamoto za waalm kwa kuboresha masilhi yao, na kuondoa changamoto zao, waalim hawana haja ya kutokulipa nauli,
Au makonda angekuja na hoja y usafiri wao kama puplic car au kuwakopesha vifaa vya usafr kwa mashart nafuu, haiingii akilin waalim kusafr buree watapata shida isiyokuwa na tija
Sina uhakika kama waalim watakubali, kwa mara ya kwanza katika uhai wangu wa jf naungana na g.mkoba..
Nina msimamo wangu juu ya Makonda, nikisikia tamko lakupinga ametoa kiongozi wa UKAWA au mwanaharakati mwingine nitatafakari mawazo yake ILA, Mkoba wewe ni Jipu, Mnyonyaji wa wa walimu, na tunatafakari jinsi ya kukutumbua. Kifupi hauna sifa wala haustahili kuongea kwa niaba ya Mwalimu. HAUNA TOFAUTI NA WALE VIONGOZI WANAOBAKA DEMOKRASIA. Unabahati ya sheria za mtandao. TENA WALIMU WANAHASIRA NA WEWE LAITI UNGELIJUA....Mwenyekiti wa chama cha walimu Tanzania G. Mkoba amesema haoni kama ni sahihi kwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni kuingia kwenye makubaliano na wenye mabasi ya daladala ya kuwasafirisha walimu bure bila kuwashirikisha walimu wenyewe, hivyo ameshauri kuwa ni vizuri mambo yanayowahusu waalimu yakawa yanawashirikisha walimu.
Chanzo: Clouds tv
Hiyo lift na allowance ni kwa walimu tu au na watumishi wote wa serikali??Walimu subirini muyaone manyanyaso na matusi ya makondakta wa daladala.
Anafika kituoni anasema hata wale walimu kitambulisho juu! Mnanyoosha saba anasema nachukua wawili tuu na bus lina nafasi. Linakuja lingine mikono juu, ingia watatu. Nani ataweza manyanyaso hayo?
Suluhisho ni kuwapa transport allowance au kuamuru magari ya serikali yawe yanasimama vituoni na kutoa lift
Kwa hiyo makonda awalipe mshahara mnono walimu na kuwalipa malimbikizo yao??Hivi ni kweli walimu wana shida na nauli ya kwenda kazini? Hapana walimu hawana shida ya nauli isipokuwa walimu wana shida ya mshahara mdogo,malimbikizo yao toka kipindi cha Kikwete,kutopanda vyeo na mazingira duni ya kazi
Hivyo hayo ndio baadhi ya matatizo ya msingi waliyo nayo walimu na sio nauli ya daladala
Iko vere simpo, hutaki kupanda bure, ingia kimya kimya kisha lipa, kelele za nini???Mwenyekiti wa chama cha walimu Tanzania G. Mkoba amesema haoni kama ni sahihi kwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni kuingia kwenye makubaliano na wenye mabasi ya daladala ya kuwasafirisha walimu bure bila kuwashirikisha walimu wenyewe, hivyo ameshauri kuwa ni vizuri mambo yanayowahusu waalimu yakawa yanawashirikisha walimu.
Chanzo: Clouds tv