CWT: NHC haitufai kwa lolote

CWT: NHC haitufai kwa lolote

SONGOKA

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
1,836
Reaction score
1,845
Habari nilizozipata kutoka kwa kiongozi mwandamizi wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) nikwamba mpaka sasa hakuna hata mwalimu mmoja aliyefanikiwa kuweza kukopa au kununua nyumba za NHC Tanzania nzima.

Walimu wanashangaa NHC kugeuka kuwa shirika lenye mlengo wa kibepari na sii la kuwahudumia watanzania wenye kipato cha chini na kati, na wamepanga kufikisha malalamiko yao officially kwa mkuu wa nchi

MY TAKE:
TUICO na TUCTA tunaomba mtupe mrejesho pia, NHC inatumika kwa manufaa ya wenye pesa nzito nzito.
 
Wao walie na TBA ndo inawahusu watumishi wawache NHC wadil na Vibopa
 
wanacho fanya NHC ni kujitajirisha.

Viongozi wote walio katika menejiment ya NHC WAMEKOPESHWA MAGARI MAPYA KABISA NA BADO WANATUMIA MAGARI YA KAMPUNI NA AMBAYO I MAPYA PIA !

VIONGOZI WA JUU KAZI YAO KUZUNGUKA TU SAFARI HAZIISHI NCHINI NA NJE WANATUMIA SANA PESA ZA SERIKALI BILA KUULIZWA !

KILA KIONGOZI WA NHC KTK MANAGEMENT TEAM AMESHAJENGA JUMBA LA KIFAHARI KTK MUDA MFUPI TU WALIOAKAA KAZINI.TUJIULIZE MARA HII PESA WAMETOA WAPI ?

TAKUKURU MKO WAPI HAWA JAMA WANA PESA NI BALAA.WANAZIPATA WAPI ?
 
TUCTA ni Janga kwa Wafanyakazi wa Tanzania... Bahati Mbaya sana, TUCTA is heavily regulated na TISS kwa Maslahi ya CCM ... Wafanyakazi mtaendelea kulipwa mishahara ya hadaa hadi CCM watoke Madarakani ...
Habari nilizozipata kutoka kwa kiongozi mwandamizi wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) nikwamba mpaka sasa hakuna hata mwalimu mmoja aliyefanikiwa kuweza kukopa au kununua nyumba za NHC Tanzania nzima.

Walimu wanashangaa NHC kugeuka kuwa shirika lenye mlengo wa kibepari na sii la kuwahudumia watanzania wenye kipato cha chini na kati, na wamepanga kufikisha malalamiko yao officially kwa mkuu wa nchi

MY TAKE:
TUICO na TUCTA tunaomba mtupe mrejesho pia, NHC inatumika kwa manufaa ya wenye pesa nzito nzito.
 
Habari nilizozipata kutoka kwa kiongozi mwandamizi wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) nikwamba mpaka sasa hakuna hata mwalimu mmoja aliyefanikiwa kuweza kukopa au kununua nyumba za NHC Tanzania nzima.

Walimu wanashangaa NHC kugeuka kuwa shirika lenye mlengo wa kibepari na sii la kuwahudumia watanzania wenye kipato cha chini na kati, na wamepanga kufikisha malalamiko yao officially kwa mkuu wa nchi

MY TAKE:
TUICO na TUCTA tunaomba mtupe mrejesho pia, NHC inatumika kwa manufaa ya wenye pesa nzito nzito.

Nyumba za NHC zinauzwa kuanzia milioni 39 na kuendelea, kulingana na ukubwa wa nyumba. Ukiongeza na riba ya benki(kumbuka NHC unawalipa cash kwa kukopa benki kwa kutumia dhamana ya nyumba uliyouziwa) nyumba ya milioni 39 unaweza kuinunua kwa milion 50 au zaidi.

Hizi nyumba kwa mtu wa kipato cha chini akizikimbilia anaumia bora kwa wale wenye pesa zao lakini hawana muda au wanaotaka kutakasa pesa haramu.
 
Bei ya kiwanja cha serikali haizidi 1.5 Mil lakini makampuni yananunua na kuuza 10 Mil. NHC inauzwa nyumba 50 Mil kwa mshahara upi? Nyumba ya 15 Mil wao wauza 50 Mil, je 50 Mil ni being rahisi kwa mtanzania.
 
NHC ni ya watu watatu tu, watu hawa ukipingana nao hata Uwaziri unaota mbawa. NHC, ATC, TPA NSSF ndio mashirika yanayotafunwa zaidi.
 
WEZI TU HAO, HAWANA LOLOTE, WAMEJENGA PALE LEVOLOSI ARUSHA NYUMBA ZA KUNUNUA MLI 90 mpaka leo hazipata watu huu ni mwaka wa 3 hakuna fedha inayoingia huku wanaweka makampuni ya ulinzi, usafi na huduma zingine za lile eneo kwa gharama cjui ya nani, hii nchi inaliwa kwa kivuli cha kuchapa kazi kumbe wizi mtupu, Safari za mafunzo nje ya nchi kila cku alafu ni kwa wakubwa tu watendaji hawapelekwi, sasa mapaka leo wanajifunza nn wakati wamejenga majengo watu wanashindwa gaharama za kununua na kupanga , ni kubwa sana , mfano pale LEVOLOSI ARUSHA Kupaishwa sh laki 3 kwa mwezi na bado uchangie elfu 30 ya maji na usafi jumla inakuwa Tsh 330,000/- kwa mwezi wakati appartment yenyewe room mbili tu, sasa unajiuliza hili ni shirika la UMMA au shirika la wahuni wachache wapiga pesa. BUNGE LA NCHI WATETEZI NA WAWAKILISHI WA WATANZANIA MKO WAPI NA MNAFANYA NN BUNGENI,
 
NHC ni ya watu watatu tu, watu hawa ukipingana nao hata Uwaziri unaota mbawa. NHC, ATC, TPA NSSF ndio mashirika yanayotafunwa zaidi.

mkuu hebu funguka hawa mapacha WATATU ni kina nani????
 
Habari nilizozipata kutoka kwa kiongozi mwandamizi wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) nikwamba mpaka sasa hakuna hata mwalimu mmoja aliyefanikiwa kuweza kukopa au kununua nyumba za NHC Tanzania nzima.

Walimu wanashangaa NHC kugeuka kuwa shirika lenye mlengo wa kibepari na sii la kuwahudumia watanzania wenye kipato cha chini na kati, na wamepanga kufikisha malalamiko yao officially kwa mkuu wa nchi

MY TAKE:
TUICO na TUCTA tunaomba mtupe mrejesho pia, NHC inatumika kwa manufaa ya wenye pesa nzito nzito.

Hili shirika lipo kwa maslahi ya magabachori, mie nilidhani kwamba kipaumbele cha nyumba hizo kingeelekezwa kujenga nyumba maeneo ambayo kuna uhaba wa nyumba za watumishi katika kila kona ya nchi na kuwapangisha au kuwakopesha watumishi hao, lakini kwakuwa watumishi hawana 10% ya kuwahonga vigogo basi nyumba zinalengeshwa kwa wahindi na mafisadi huku watumishi wakinyanyasika kwenye nyumba za watu binafsi kwa kulipa kodi kubwa na mbaya zaidi nyumba hizo ni za vigogo wa serikali
 
Habari nilizozipata kutoka kwa kiongozi mwandamizi wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) nikwamba mpaka sasa hakuna hata mwalimu mmoja aliyefanikiwa kuweza kukopa au kununua nyumba za NHC Tanzania nzima.

Walimu wanashangaa NHC kugeuka kuwa shirika lenye mlengo wa kibepari na sii la kuwahudumia watanzania wenye kipato cha chini na kati, na wamepanga kufikisha malalamiko yao officially kwa mkuu wa nchi

MY TAKE:
TUICO na TUCTA tunaomba mtupe mrejesho pia, NHC inatumika kwa manufaa ya wenye pesa nzito nzito.

Nchi yangu Tanzania nakupenda. tuna wasomi wa kutosha, lakini najiuliza hivi kweli usomi wetu unatusaidia. kuna relation kati ya umasikini na usomi, tunategemea kwenye wasomi level ya umasikini iwe chini. msomi ni lazima apange mambo yake hata miaka 100 ijayo. nalishangaa shilika la nyumba 10-50 km wananunua viwanja na kujenga vijumba na kuviuza. hebu tujiulize mfanyakazi wa miaka 20 ijayo ataishi wapi ina maana atatakiwa kusafiri more than 50 km kuja kufanya kazi. kwa nini wasijenje nyumba mijini na kuzipangasha kwa mujibu wa sheria ambapo tunawezasema mtu apange kwa gahrama ya 10% ya mshahara wake. mtakuwa mmeisaidia sana nchi, wafanyakazi na vizazi vijavyo. vilevile sina uhakika kama uchambuzi yakinifu unafanywa kwenye miradi ya NHC, tuwe waangalifu ni hatari sana kwa nchi na uchumi wetu. CEO ambaye siku zote yuko karibu na wanasiasa, anatumia muda mwingi kwenye media, mwisho wa siku ni siasa tu, expect no positive impact to our ecomomy, tusubiri maumivu.
 
mkuu hebu funguka hawa mapacha WATATU ni kina nani????

Kabla ya kufunguka jua kuwa Shilika hili si la UMMA tena Bali ni la KUUMA, kumbuka malamiko ya hapo awali ya kuongezewa mshahara mkurugenzi pamoja naposho nyingi kama vile anafanya kazi peke yake, alipokataa Prof. Anna Tibaijuka unaona yaliyomtokea, Pili nyumba nyingi zinazokaliwa na wahindi mjini hazijaongezewa kodi mda mrefu kwani wahindi wanajua njia zao za kuwafanya wasiongezewe kodi, lakini wapangaji wapya wakukutana na kadhia kali ya kupandishiwa kodi kubwa kwa vyumba vya biashara, sisi walala hoi uwezi kupata sehemu ya biashara ya bei nafuu, yaani NHC imekuwa shirika la kilanguzi, hata vipimo vyao vya kodi per square haviko sahihi wanakisia tu bei wanakupiga.
 
National Housing Corporation njooni hapa [MENTION]National Housing Corporation[/MENTION]
 
wanacho fanya NHC ni kujitajirisha.

Viongozi wote walio katika menejiment ya NHC WAMEKOPESHWA MAGARI MAPYA KABISA NA BADO WANATUMIA MAGARI YA KAMPUNI NA AMBAYO I MAPYA PIA !

VIONGOZI WA JUU KAZI YAO KUZUNGUKA TU SAFARI HAZIISHI NCHINI NA NJE WANATUMIA SANA PESA ZA SERIKALI BILA KUULIZWA !

KILA KIONGOZI WA NHC KTK MANAGEMENT TEAM AMESHAJENGA JUMBA LA KIFAHARI KTK MUDA MFUPI TU WALIOAKAA KAZINI.TUJIULIZE MARA HII PESA WAMETOA WAPI ?

TAKUKURU MKO WAPI HAWA JAMA WANA PESA NI BALAA.WANAZIPATA WAPI ?
Tusiwe wepesi kulaumu, wao ni top management wa shirika la nyumba wasiwe na nyumba tena za kifahari? chanzo chakuuza nyumba kwa bei aghali si wao. NHC wao hawana pesa mfukoni, wanakopa kwenye taasisi za kifedha, hizo pesa zina riba.
Na lenyewe lazima lijiendeshe kwa faida, tulisha zoea kulifanya shirika hili kama shamba la bibi unakaa hadi unajukuu humohumo kodi yenyewe unayolipa hata haifikii nusu ya kodi unayotoza kwenye ile nyumba yako.
Hawa CWT tulisha wazoea wahana lolote, wao wanawakata walimu kila mwezi wameenda kujenga vitegauchumi ambavyo havina tija kwa walimu, kwa nini wao wasiwekeze kwenye nyumba za bei nafuu ili walimu wakope au wanunue?
 
kusema kweli hapa wa kulaumiwa ni serikali , shirika linaendeshwa kibishara kwa sasa sio linapokea bil 500 alafu linaambiwa jenga nyumba , shirika linakopa mabilioni sasa unategemea lifanye mambo yaliyokuwa yanafanyika 30 years ago haliwezi as long as serikali haitoi fungu mwendo utakuwa ni kama hivi , kuhusu management , hawa wazee ni wapigaji , yaaani hamna kupindisha maneno , tenda zote za ujenzi wanajua wenyewe wanavyopiga , kuhusu hoja ya huo mshahara wa mil sijui 15/20 kwa mwezi sio ishu sana manake shirika lina Assets za Zaidi ya tril 2 , moja ya mashirika makubwa East Africa kwa Assets valuation sasa mnataka DG Alipwe mil 3 ? serikali iseme tu kuwa hili ni shirika la biashara ya nyumba , waweke mfumo kuthibiti wizi
 
Yaani sisi wapuuzi kweli! Shirika lilikuwa mufilisi tuliaamsha ili leweze kufanya majukumu yake kwanza kwa kufanya biashara ili liwe na afya nyinyi mnataka kukamua mpaka damu.

shirika hili tuliacha lifanye business for next 10 years ndio lianze kujenga makazi ya makabwela kama mimi kwa kweli watafaidika wengi sana.
 
wanacho fanya NHC ni kujitajirisha.

Viongozi wote walio katika menejiment ya NHC WAMEKOPESHWA MAGARI MAPYA KABISA NA BADO WANATUMIA MAGARI YA KAMPUNI NA AMBAYO I MAPYA PIA !

VIONGOZI WA JUU KAZI YAO KUZUNGUKA TU SAFARI HAZIISHI NCHINI NA NJE WANATUMIA SANA PESA ZA SERIKALI BILA KUULIZWA !

KILA KIONGOZI WA NHC KTK MANAGEMENT TEAM AMESHAJENGA JUMBA LA KIFAHARI KTK MUDA MFUPI TU WALIOAKAA KAZINI.TUJIULIZE MARA HII PESA WAMETOA WAPI ?

TAKUKURU MKO WAPI HAWA JAMA WANA PESA NI BALAA.WANAZIPATA WAPI ?
Huyu sasa kaja na yake hivi nani alisema viongozi wa serikali lazima wawe masikini, umechanganya mada ndugu ni better ukawashitaki hao nhc pccb ili tujue mbivu na mbichi
 
kwani CWT hawana uwezo wa kujenga nyumba zao na kuwauzia walimu kwa njia ya mikopo.1.7 bilion wanazotaka kuanzisha bank si wangetumia kujenga na kisha kuwauzia walimu hizo nyumba
 
Habari nilizozipata kutoka kwa kiongozi mwandamizi wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) nikwamba mpaka sasa hakuna hata mwalimu mmoja aliyefanikiwa kuweza kukopa au kununua nyumba za NHC Tanzania nzima.

Walimu wanashangaa NHC kugeuka kuwa shirika lenye mlengo wa kibepari na sii la kuwahudumia watanzania wenye kipato cha chini na kati, na wamepanga kufikisha malalamiko yao officially kwa mkuu wa nchi

MY TAKE:
TUICO na TUCTA tunaomba mtupe mrejesho pia, NHC inatumika kwa manufaa ya wenye pesa nzito nzito.
Mawazo mgando, let me take a break! Hi hivi ndugu nani alikuambia NHC ni shirika la kujenga nyumba za walimu tu, hebu nenda kasome sheria iliyoliunda inasemaje kisha ndo uje na hadithi. NHC ya sasa siyo ya mwalimu hii ya sasa haina ruzuku hata senti yajiendesha kibiashara haiwezi kugawa nYumba. Umemiss point rudia tena
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom