bongospecialist
New Member
- Nov 5, 2010
- 4
- 0
Heshima kwako Kizomanizo.
Mkuu asante sana umejaribu kutoa majibu ambayo wengi wamekwepa kwa makusudi.Kuna kipindi unafika unawashangaa watu hapa Jamvini habari wanazotaka ni kusifia CHADEMA tu ukikosoa utapachikwa majina ya ajabu ajabu.Mleta mada kaomba CV za wabunge wa CHADEMA kama unajua unatuambia kama hujui unakaa kimya.
Mkuu wangu CV ya Godbless Lema ni ya hovyo kuliko nilivyofikiri mwanzo.Jamaa alishindwa kufaulu mtihani wa form II kuingia form III.Ana cheti cha lugha ya kiingereza miezi 3 KIMAHAMA mkabala na Golden Rose.Mkuu mambo mengine labda ajiendeleze baada ya kuwa mheshimiwa kazi hii namwachia kamanda PakaJimmy anaweza kumshauri.
Mkuu ni kweli Lema amechaguliwa kwasababu watu wameichoka CCM si kwa ubora wa kujenga hoja hata kidogo.
Nasikitika sana kama kuna watanzania wanajiita wasomi hata hawajui maana ya CV wanafikiri elimu ndiyo Cv elimu ni sehemu tu ya Cv Kushindwa Form II haina maana huyu ni mtu asiyefaa katika jamii. Mchango wake kwenye jamii ndiyo kitu cha maana na ndicho cha kuangalia kwenye CV kuna watu maarufu duniani leo hii ambao wamefanya mambo makubwa sana katika jamii yetu na yenye maana sana na hata mengine yamewezesha mimi na wewe tuweze kuchangia mwawazo yetu na maoni mbalimbali leo hapa. Mfano Bill Gate aliwahi kushindwa sehemu fulani katika MCHAKATO wa elimu na aka( drop class). Hebu tuwapime watu kwa uwezo wao na mchango wao katika kuleta maendeleo katika jamii na si vinginevyo. Kuna watu wanajiita wamesoma sana wana GPA za nguvu, ni ma dokta, Professa na kadhalika. Lakini hawana maana yoyote katika jamii elimu yao ni sawa na zero kwani haina Impact yoyote kwenye jamii na pengine wamechangia kudidimiza jamii. Maoni yangu ni kwamba jambo lolote la maana ambalo hawa wamefanya au watafanya katika kubadili jamii maskini ya watanzania ndiyo kinatakiwa hapa na si vinginevyo lakini kama unataka kuandika porojo unaidanganya nafsi yako.
Sifa za kugombea ubunge Jamhuri ya muungano wa Tanzania hizi hapa;
Sifa za mgombea Ubunge
Je Godbles Lema hana hizo sifa???????? .
Awe raia wa Tanzania Awe na umri wa miaka 21 au zaidi Awe ni Mwanachama na ni Mgombea iliyependekezwa na Chama cha Siasa Awe hajatiwa hatiani na Mahakama yoyote kwa kosa la kukwepa kulipa kodi katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi Awe anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza
Lameck Airo mbunge wa Lorya ame fuzu hizo sifa ndo maana akapata tiketi ya CCM na hatimaye kuwa mbunge wa Jimbo hilo.
Heshima kwako Kizomanizo.
Mkuu asante sana umejaribu kutoa majibu ambayo wengi wamekwepa kwa makusudi.Kuna kipindi unafika unawashangaa watu hapa Jamvini habari wanazotaka ni kusifia CHADEMA tu ukikosoa utapachikwa majina ya ajabu ajabu.Mleta mada kaomba CV za wabunge wa CHADEMA kama unajua unatuambia kama hujui unakaa kimya.
Mkuu wangu CV ya Godbless Lema ni ya hovyo kuliko nilivyofikiri mwanzo.Jamaa alishindwa kufaulu mtihani wa form II kuingia form III.Ana cheti cha lugha ya kiingereza miezi 3 KIMAHAMA mkabala na Golden Rose.Mkuu mambo mengine labda ajiendeleze baada ya kuwa mheshimiwa kazi hii namwachia kamanda PakaJimmy anaweza kumshauri.
Mkuu ni kweli Lema amechaguliwa kwasababu watu wameichoka CCM si kwa ubora wa kujenga hoja hata kidogo.
Peoples Power, Nguvu ya Wananchi ni nguvu ya Umma. Wanajamvi yeyote mwenye CV za hawa wabunge wafuatao wapya wanaoingia mjengoni atuwekee hapa tuwajue walisomea nini, wapi, wameisaidaje jamii so far,etc. lengo tuwajue vizuri kabla hawajaanza makeke yao Bungeni.
1. Tundu Lissu
2. John Mnyika
3. Vincent Nyerere
4. Hezekiah Wenje
5. Proffessor Kahigi
6. Lema(Arusha Mjini)
7. Sugu Joseph Mbilinyi(Mbeya Mjini)
8. Samson Highness (Ilemela)
etc
Mimi naomba nichangie kwa hao ambao wanamponda Lema kwamba hajasoma.
Labda tuambiane ni vigezo gani vinatumika ili kusema mtu amesoma au hajasoma? Nafikiri most us will count number of years one has
in class. Hii dhana ndo inatufanya tunakuwa na viongozi wabovu katika nchi yetu. Baraza la mawaziri la TZ linaloishia lilikuwa na maprofessor
kati ya 6-0 na PhD,s holders 10-14 lakini tupime performance ya serikali kwa ujumla. Sisemi kwamba tunatakiwa kuwa na viongozi ambao
hawajasoma NO, ila pima uwezo wa kiongozi kwa hoja zake, anavyo jieleza na mambo ailiyofanya.
Mimi namjua Lema na nimeshakaa nae mara nyingi hapa Arusha. sijawahi kumuuliza elimu yake bali kwa kumsikiliza ni mtu mweye uwezo
mkubwa sana wa kujenga hoja, kujieleza kiufasaha na ana msimamo. Kama ningependa kum rate kielimu basi ningesema ana MASTERS
DEGREE TENA YA MIAKA YA NYUMA na siyo hizi za sasa hivi (VODA FASTA) mtu kapata first degree yake PASS na ana qualify kufanya Masters.
Kwahiyo kama amesoma kimahama au popote mimi napenda kukuambia Lema ana uwezo mkubwa pamoja na elimu yake ya kimahama.
Angalia nchi kubwa duniani zimeongozwa na akina nani na ZIKO WAPI.