CV ya Pascal Mayalla

Mkuu siku ukimuibukia nitag niunge juhudi
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Paskali unampa sifa ambazo hana...

Paskali ni muoga kwa baadhi ya mambo,hua anadanganya na kwavile ana lugha laini ya kisanii saniii hivi watu hua wanaamini..

Anajifanya kila kitu anajua.....

Napata shida sana na lugha yake ya kisaniii...

Halafu hapendi head-on collisions hata kidogo,maneno yake ni kuzunguka zunguka circles,hana straight up points to clear something..
 
wewe na paskali nani muoga?
ungekua sio muoga ungetumia jina lako halisi kama paskali

Kwahiyo kutumia anony ndio uoga?

Hiyo ni definition yako na una ruksa ya kuitoa!

Kwa miwani ninayotumia mimi,huo si uoga maana hata jina linaweza kua Pascal Mayalla na ni verified ila anaeandika kupitia account hiyo muda huo sio yeye vilevile....

Ishu sio identity,we are all internet characters no matter what name you use,hatujui wanazoziendesha hizo accounts ni wao kabisa at that particular time!

Mtu real ni yule unaemuona kwa macho yako in physical form huku offline....

Unafeli sana kuchukua internet life kama physical life wakati ni virtual life altogether!

You are such a waste!
 
Name : Pascal Mayalla

Tribe : Sukuma

Education : LLB, Mass comm

Occupation : Journalist, Lawyer

Location : Dsm

Ni Jamaa mmoja smart na msomi

Hajui kuchukia wala kumtukana yeyote

Kiboko ya Mohamed Said kwa kumuumbua katika uwongo wake Mara nyingi tu.
 
Pascal Mayalla amejaliwa vipaji vingi sana.Ipo siku tu nitamuibukia kwenye vile vipindi vyake vya saba saba.
Mkuu Tate Mkuu, kwanza ni kweli kabisa kuna watu wana vipaji lukuki, yaani multi talented, ila kutokana na kutegemea fani moja tuu, vipaji vyao vingine vinakuwa havionekani, mimi ni mtangazaji wa redio, yaani radio announcer, enzi nikiwa mtangazaji wa RTD, sikufahamika sana, kwasababu nilikuwa ni mtangazaji wa External Service, idhaa ya Kiingereza, matangazo yake wali ya beamed nchi za Kusini mwa Africa kusaidia ukombozi wa nchi za Kusini mwa Africa hivyo sii wengi wananijua kama mtangazaji mzuri tuu wa redio.

Nikiwa RTD pia nilikuwa a Radio DJ, na Music DJ.

Mimi ni mtangazaji wa TV Talk Show Host wa kipindi cha Kiti Moto.

Mimi ni AV producer, yaani sio mtangazaji tuu bali pia ni mtayarishaji wa vipindi, content producer, presenter na sasa distributor.

Mimi ni journalist nikiandika for print media na electronic media
kazi hii nimeifanya kwa miaka 30 mpaka nimestaafu.

Baada ya kustaafu ndipo sasa nimejigundua kumbe nina kipaji cha uongozi ambacho kilifunikwa na utangazaji, nilikigundua nilipo beeb uchaguzi wa ubunge Kawe, japo niliambulia kura moja tuu, kutoka kwa wajumbe, kuna kitu nikajifunza, sasa kumetokea fursa nyingine ya kukipima kipaji changu cha uongozi, nime ingia in full, na kiukweli nitalisaidia sana taifa langu hili katika hilo jambo langu.
Mungu Nisaidie.
Paskali.
 
Ndg wana JF. Wasalamu.
Hivi karibuni nimejaribu kupitia michango/thread zilizoletwa na mtajwa hapo juu.
Mkuu guzman_ , kwanza asante kunianzishia thread.
Kwa namna ya uandishi wake na mawazo yake imenilazimu kutaka kujua Pascal Mayala ni nani hasa?
Pascal Mayalla ni mwana JF mwenzenu mtu wa kawaida sana.
Kiwango chake cha elimu?
Kiwango changu rasmi cha elimu ni darasa la 7, ila baada ya hapo nikaanza kuungaunga mara usome hiki mara kile, nikaungaunga hadi nikawa mwandishi wa habari na mtangazaji, nikaendelea kujisomea kwa kujisomesha kwa elimu ya kuunga unga hadi kuhitimu shahada ya sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, UDSM, ambapo ilinichukua miaka 15 kukabidhiwa LL.B yangu na ikanichukua miaka 5 mingine kukubaliwa kuwa wakili.
professional yake ni nini?
Professional yangu ni Mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea na sasa ni Wakili wa kujitegemea kwa kujitolea kutetea haki kwa watu na uwezo wa kuajiri wakili.
Historia yake ya kiafya ikoje (Hasa ya kiakili)
Niliwahi pata ajali mbaya ya Piki Piki nikadhaniwa nimekufa kumbe nilizimia tuu nikafufukia baridi la mortuary, kwa muda niliozimia madaktari wakasema nitakuwa confined to a wheelchair!, nilikuja kusimama and here I'm.
?Na kama mtanzania au la! n.k
Sio tuu ni Mtanzania, bali ni Mtanzania original halisi na Mzalendo wa kweli wa taifa hili.
NB: Naamini hamna mtu anaweza kuwa na fikra kubwa kama huyu jamaa.
Asante
Kitendo cha kuleta mada ya mkuu wetu wa mkoa kuwa Raisi wa JMT baada ya JPM binafsi nimeona ni suala zuri ila nani kaleta mawazo hayo ndo nataka kujua profile yake.
Mimi naandikia watu watatu humu
  1. Kuna mada nawaandikia wananchi wa kawaida simple minds, ambao hawahitaji kufikiri chochote, wao interest zao ni kusikia tuu chochote, hizi ni mada kuwahusu watu, naziandika kwa ajili ya simple minds ambao wao interest zao ni habari za watu.
  2. Mimi kama Mwandishi wa habari, kuna mada naripoti kuhusu matukio mbalimbali, Kwa ajili ya ordinary minds ambao hu discuss events, kumetokea nini wapi na ikawaje.
  3. Na kuna mada naziandika kwa ajili ya great minds, hizi ni mada kuhusu ideas na wasomaji they need to think. Mada hizi huziandika kwa coded ili kuelewa nazungumzia nini ni lazima kwanza uwe na uwezo to read in between the lines, pili uwe na uwezo wa kuzibaini hizo codes na uncode the codes to connect the dots.
Ikitokea wewe ni simple mind ukakutana na mada ya great minds, utaishia chaka!. Hiki ndicho kilichokukuta wewe uliposoma bandiko hili Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!. Apunguze..., ukikutana na mada iliyokuzidi kimo, lazima utaishia kuingia chaka. Pole.

Ila pia kiukweli nimeisaidia sana jf kuwa transforms simple minds wengi kuwa great minds. Na wewe uliposoma mwanzo bandiko hilo ulikuwa simple mind, sasa lisome tena huku unatafakari utapata kitu kingine, akisoma ikashindwa kabisa kujua nazungumzia nini, then bandiko hilo sio saizi yako.
Karibu ujaribu, ukishidwa kabisa nitakufungulia baadhi ya codes.
P.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…