Curriculum Vitae kwa kiswahili ni nini?

KUN

JF-Expert Member
Oct 17, 2011
379
225
sio kila neno la kiingereza lina neno lake kwa kiswahili....sisi tuna maneno machache sana ya kiswahili chukua dictionary ya oxford 7th edition afu linganisha na kamusi zetu...ni tofauti kabisa.
 
HT

JF-Expert Member
Jul 29, 2011
1,897
0
Maelezo Binafsi ya Mtu Kama Ujuzi n.k (Source Tuki)
Kama ni kuandika katika Heading ni Wasifu kama ilivyosemwa.

My CV - Wasifu Wangu [Kitaalam|Kimasomo|Kimaisha]
 
Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,269
2,000
sio kila neno la kiingereza lina maana yake kwa kiswahili....sisi tuna maneno machache sana ya kiswahili chukua dictionary ya oxford 7th edition afu linganisha na kamusi zetu...ni tofauti kabisa.

Ni kweli ila bado hujanisaidia
 
Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,269
2,000
Hati Nafsi

Hii ni mpya...naamini Bakita wanaikubali..!

Maelezo Binafsi ya Mtu Kama Ujuzi n.k (Source Tuki)
Kama ni kuandika katika Heading ni Wasifu kama ilivyosemwa.

My CV - Wasifu Wangu [Kitaalam|Kimasomo|Kimaisha]

Hivi mtu anaweza kuandika wasifu wake mwenyewe au unaandikwa na mtu baki?

Nahisi kama hili la wasifu liko mbali kidogo na CV ambayo mtu mwenyewe anajiandikia.
 
HT

JF-Expert Member
Jul 29, 2011
1,897
0
Hivi mtu anaweza kuandika wasifu wake mwenyewe au unaandikwa na mtu baki?

Nahisi kama hili la wasifu liko mbali kidogo na CV ambayo mtu mwenyewe anajiandikia.
Ndiyo mfano Mchungaji Donnie McClurkin ameandika Wasifu wake kwa kirefu sana wa maisha.
Ukiangalia Biography na CV vyote vinakuwa translated wasifu. mmoja ni wa Maisha mwingine ni wa ujuzi.
Pengine CV inapaswa iwe Wasifu wa Ujuzi na Biography Wasifu wa maisha

Hata hivyo mimi sio nguli wa lugha, ni maoni yangu tu!
 
Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,269
2,000
Ndiyo mfano Mchungaji Donnie McClurkin ameandika Wasifu wake kwa kirefu sana wa maisha.
Ukiangalia Biography na CV vyote vinakuwa translated wasifu. mmoja ni wa Maisha mwingine ni wa ujuzi.
Pengine CV inapaswa iwe Wasifu wa Ujuzi na Biography Wasifu wa maisha

Hata hivyo mimi sio nguli wa lugha, ni maoni yangu tu!

Ahsante sana kwa ufafanuzi.

Naamini wataalamu wa lugha watakuwa na neno au maneno ambayo yanatabaisha vizuri hizi dhana.

Labda Gaijin na EMT wataweza kusaidia.
 
Last edited by a moderator:

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
53,272
2,000
CV ni Curriculum Vitae, literally "Maisha ya Mitaala/Usomi". Strictly speaking it should be more about academic achievement than career achievements/ history, this is why in the US "Curriculum Vitae" is used in academic settings and "resume" is what is known as "Curriculum Vitae" in Tanzania.

It is common to see University professors and Ph.D aspirants refer to their printed record of academic achievement as "Curriculum Vitae", while jobseekers without an extensive record in academia would refer to their job history as "resume".

See

The Difference Between a Curriculum Vitae (CV) and a Resume
 
gmosha48

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
2,392
2,000
Hii ni kwa mujibu wa juha mmoja tunaepigac nae kinywaji haa kitaa.

Cd- country director

Ce- Country editor

Cv- Country volunteer.
 
EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,481
2,000
Ahsante sana kwa ufafanuzi.

Naamini wataalamu wa lugha watakuwa na neno au maneno ambayo yanatabaisha vizuri hizi dhana.

Labda Gaijin na EMT wataweza kusaidia.

Kamusi ya Kiingereza - Kiswahili iliyoandikwa na R.A Snoxall na H.B. Mshindo inasema kuwa:

Curriculum Vitae ni maelezo binafsi ya kuhusu elimu na uzoefu katika kazi, n.k.

Hii ni tofauti na biography ambayo ni maandishi ya habari za maisha ya mtu.

Nyani Ngabu ataongezea.
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
87,061
2,000
Kamusi ya Kiingereza - Kiswahili iliyoandikwa na R.A Snoxall na H.B. Mshindo inasema kuwa:

Curriculum Vitae ni maelezo binafsi ya kuhusu elimu na uzoefu katika kazi, n.k.

Nyani Ngabu ataongezea.

Naam, uko sawa kabisa.

CV ni 'muhtasari (ufupisho wa maelezo) wa elimu, ujuzi, maarifa, na tajiriba ya/za kazi'.
 
Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,269
2,000
Kamusi ya Kiingereza - Kiswahili iliyoandikwa na R.A Snoxall na H.B. Mshindo inasema kuwa:

Curriculum Vitae ni maelezo binafsi ya kuhusu elimu na uzoefu katika kazi, n.k.

Hii ni tofauti na biography ambayo ni maandishi ya habari za maisha ya mtu.

Nyani Ngabu ataongezea.

Ahsante sana Mkuu EMT,

Hiyo ya maelezo binafsi nakubaliana nayo kwa kiwango kikubwa.

Ila nilipata tatizo nyingine wakati naweka vichwa vidogo vidogo (sub-heading) ambapo nilitaka kuwa na,
A) Personal particulars or biodata (hii ni sahii kwa kusema ni "taarifa binafsi"??)
B) Academic details (Elimu/taaluma)
C) Professional experience (Uzoefu wa Kazi)
D) Other information (Taarifa nyinginezo)
E) Referees (Wadhamini).

Naomba michango yenu kuhusu hili,
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom