Kwani dawa siku zote hupatikana vipi? sii hutanyika uchunguzi kwanza mgonjwa kufanyiwa vipimo, ukachukuliwa damu ikafahamika ugonjwa kisha unapewa dawa inayohusiana na Ugonjwa. Kinachofanyika leo ni kelele za mgonjwa wa wasiwasi tu ambaye hana maradhi hayo kama yangekuwepo asingekwenda kazini kama tunavyowaona kina Jussa, Maaalim Seif, Karume wote wanaitumikia serikali ya Jamhuri ya muungano. hakuna mgonjwa hapa ila wanatumia ugonjwa wa kitoto kililia mafua ili upikiwe chapati na chai ya hiriki..
Nchi zenye matatizo tuliwaona viongozi wao kina Ojukwu wa Biafra, John Garang wa South Sudan, Hami Awate wa Eritria ambao walikataa hata kuzitumikia serikali zao kwa sababu walitaka kujitenga na kero zilikuwa halali..Lakini ya Zanzibar ni wadudu tu walioko ktk kokwa la embe ambao kazi yao ni kutula taratibu hadi embe lifubae na kuanguka toka mtini.
Serikali tatu, sii dawa bali kutuliza maumivu na presha...Chadema wanaitetea hopja hii kwa maslahi ya bara na ndio maana CUF na Wazanzibar walipiga mahesabu wakagundua kwamba serikali tatu ingekula kwao wakajitoa na kuunda serikali ya mseto ndani ya mfumo uliopo wa muungano kinachobadilika ni kuvikana vyeo kama lilivyokuwa Azimio la Zanzibar.
Hawa wanaofanya chokochoko za muungano wangetakiwa kuwajibishwa lakini kutokana na serikali yetu kuwa dhaifu kiasi kwamba wanashindwa hata kuwawajibisha Mafisadi ndio maana tunaona swala hili ni zito sana na linatuelemea. Wapo watu wanaamini kabisa Ufisadi hauwezi kudhibitiwa, ati Ufidasi hauwezi kwisha upo hata Marekani?... hii mifano ya mwendawazimu wakati tumejaza magereza zetu vibaka ambao pia wezi hawa hawawezi kwisha.
Swala la kero za muungano ni swala la kisiasa na ulaji na linatumiwa ili baadhi ya viongozi wapate kuchaguliwa ktk uchaguzi mkuu wa Zanzibar maana ndivyo wananchi wanaaminishwa kwamba kuna tatizo ktk muungano wakati tatizo ni viongozi wenyewe. Dawa ya kero za muungano ni KATIBA MPYA. Katiba itakayo wabana viongozi wote na kuacha mamlaka hayo kwa wananchi wenyewe kiasi kwamba wakitaka kura za maoni lazima zifanyike, wakitaka kumwondoa kiongozi madarakani wanaweza wakati wowote. Kuondoa au kupunguza madaraka kwa viongozi wa juu, kurudisha miiko na maadili kwa viongozi ambao wameshindwa kutatua matatizo ya Watanzania ndio dawa ya kwanza.
Kuunda serikali tatu itakuja kuunda majimbo na mengine ambayo yote kwa ujumla wake ni ULAJI tu, maana Tanzania kwa eneo ni sawa na state moja ya Marekani au Province moja ya canada lakini budget yake ni chini ya hata mji mmoja wa Marekani ambao una watu wasiozidi millioni 10.
Chukua mfano wa Zanzibar kama jimbo au Nchi, na wameshindwa kama jimbo na wameshindwa pia kama nchi..unaweza kunambia wanashindwa vipi kujiendeleza.. viongozi wake hawna tofauti na wa bara hivyo tunachukua mfano gani ikiwa huu ndogo uliopo machooni mwetu hauna mafao..
- TATIZO ni mambo mawili ambayo ni UONGOZI BORA na Mfumo Mbaya wa Kiutawala (KATIBA) haya ndio dawa na kinga ya kero zote za muungano na umaskini ni kuwabana mbavu tu makupe, mirija na makabaila..