CUF yataka serikali tatu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF yataka serikali tatu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by norbit, Dec 30, 2010.

 1. norbit

  norbit JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2010
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 496
  Likes Received: 212
  Trophy Points: 60
  • Wateule wa Rais wathibitishwe na Bunge
  • Baraza lisiwe na mawaziri zaidi ya 15
  • Vyama viungane siku 21 kabla kampeni kwisha
  • Rais aunde tume huru kwa ushauri wa wadau

  Chama cha Wananchi (CUF), kimeweka hadharani mambo yaliyomo kwenye rasimu ya mapendekezo yake ya Katiba mpya; mojawapo likiwa ni Tangazo la kuwapo Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania, ambayo itaundwa na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

  Jambo lingine lililomo kwenye rasimu hiyo, linahusu uwepo wa Serikali ya Tanganyika na Zanzibar juu ya mambo yote yasiyo ya Shirikisho na kwamba, kiongozi mkuu wa serikali hizo, ataitwa "Gavana" na kila gavana, atachaguliwa kwa mujibu wa Katiba ya nchi anayotoka (yaani Tanganyika au Zanzibar).

  Kwenye rasimu hiyo, pia kuna katazo la kumshtaki rais anapokuwa madarakani na iwapo atakuwa nje ya madaraka anaweza kushtakiwa kwa makosa maalum.

  Pia vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu kwamba, vitaweza kuungana kuunda chama kimoja kwa ajili kushiriki uchaguzi siku 21 kabla ya tarehe iliyotangazwa na tume ya uchaguzi kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni bila vyama hivyo kupoteza usajili wao.

  Rasimu hiyo iitwayo: "Dhana ya rasimu sifuri ya mapendekezo ya wadau kuhusu Katiba mpya ya Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania" au "Rasimu ya mapendekezo ya Katiba ya Tanzania, ina sura 16, Ibara 131 na nyongeza tatu na iko katika kurasa 88.

  Iliwekwa hadharani na Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro, alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.

  Alisema rasimu hiyo ilianza kuandaliwa mwaka 2006 na wadau waliotokana na jopo lililoundwa na chama hicho lililowashirikisha watu zaidi ya 400 wa kada mbalimbali.

  Alisema hadi kufikia Julai, mwaka huu, walitumia Sh. milioni 138 kuandaa rasimu hiyo na kwamba, katika kuiandaa, walipata msaada wa Katiba zaidi ya 30 za nchi za barani Afrika, Amerika na Ulaya kwa kuchukua sampuli zake.

  Jambo lingine muhimu lililomo kwenye rasimu hiyo, ni uwapo wa tume huru ya uchaguzi ya shirikisho, ambayo wajumbe wake watateuliwa na Rais baada ya kupendekezwa kwake kutokana na mamlaka za wadau wanaohusika, ambapo mjumbe mmoja atatoka katika chama cha siasa chenye wabunge wa kuchaguliwa walau kutoka upande mmoja wa Shirikisho.

  Wajumbe wengine watatoka mashirika na taasisi zisizo za kiserikali zinazoshughulikia uongozi wa jamii, taasisi za kidini, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, watu wenye ulemavu, wanawake, vijana na wazee.

  Pia mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa tume, watachaguliwa na wajumbe wa tume husika kutoka miongoni mwao.

  Jambo lingine linahusu uwepo wa mabaraza mawili ya wawakilishi, moja la Tanganyika na lingine la Zanzibar, ambayo yatakuwa na mamlaka ya kutunga sheria kuhusu mambo yasiyo ya Shirikisho, kujadili, kusimamia na kudhibiti shughuli za Serikali za Tanganyika na Zanzibar.

  Kuhusu mgombea binafsi, rasimu hiyo inatamka kwamba, kila mwananchi aliyetimiza umri wa miaka 18 anayo haki ya kupiga au kupigiwa kura katika uchaguzi unaofanywa Tanzania na wananchi.

  Hata hivyo, inatamka kwamba, uchaguzi hautarudiwa iwapo mbunge aliyechaguliwa jimboni atafariki dunia, badala yake chama anachotoka, kitateua mwanachama wake mwingine mwenye sifa kurithi kiti hicho na kwamba, uchaguzi utahitajika kama atakayekufa atakuwa ni mbunge aliyegombea binafsi.

  Rasimu hiyo pia inatamka kwamba, kutakuwa na wizara 15 na rais hataunda wizara mpya nyingine isipokuwa kwa ushauri wa Bunge.

  Pia Waziri Mkuu, waziri, naibu waziri, balozi, Gavana wa Benki Kuu (BoT), Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), makamishna wa mamlaka zilizoundwa kwa mujibu wa sheria na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, itakuwa ni wajibu wa Bunge kuidhinisha uteuzi wao utakaofanywa na Rais.

  Vilevile inatamka kwamba, kutakuwa na Mkutano Mkuu wa Katiba, ambao wajumbe wake watachaguliwa na sekta mbalimbali za umma wa Watanzania kwa wawakilishi 10 kutoka kila chama cha siasa kilichosajiliwa na madhehebu makuu ya Wakaristo na Waislamu.

  Wawakilishi wengine 10 watakuwa wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya raia wa Tanzania, vyama vya wafanyakazi, vyama vya wakulima, vyama vya wanafunzi wa vyuo vikuu, vijana, wanawake, vyama vya waajiri, vyama vya wasiojiweza, vyama vya wafanyabiashara, Spika na wabunge wa shirikisho, Rais, Makamu wa Rais na Baraza la Mawaziri wa Shirikisho.

  Wengine ni majaji wa Mahakama Kuu ya Shirikisho, Tanganyika, Zanzibar na Mahakama ya Zanzibar, Gavana wa Tanganyika, Zanzibar na Mabaraza ya Mawaziri wa Tanganyika na Zanzibar, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Tanganyika na Zanzibar, wajumbe 10 wanaowakilisha wasanii na wajumbe 10 wanaowakilisha vyama vya michezo. Mkutano huo wa Katiba utakuwa na mamlaka ya kutunga Katiba.

  Jambo lingine ni Mahakama Kuu ya Shirikisho, ambayo itakuwa "Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania" itakuwa na mamlaka yasiyokuwa na mipaka ya kusikiliza mashauri ya jinai, daawa na upatanishi kwenye mambo ya Shirikisho, kutoa hukumu na amri zenye nguvu kisheria kuzidi mahakama nyinginezo zilizoko chini yake.

  Pia haitakuwa na mipaka ya kutafsiri Katiba ya Shirikisho na sheria za nchi na kufanya kila jambo linalohusu utoaji wa haki kwa mujibu wa mila za kisheria zinazotumika Tanzania, ambazo hufanywa na mahakama kuu na kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi pamoja na taratibu zake.

  Vilevile, Rais wa Mahakama ya Rufani, ambaye atatajwa kama "Rais wa Mahakama" na kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano, ambao hautahojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania.

  Jambo lilingine linahusu Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, ambayo itakuwa na mamlaka ya kuchunguza tabia na mwenendo wa kiongozi yeyote wa umma.

  Rasimu hiyo pia inatoa haki ya uraia kwa watu wote waliokuwa raia wa Tanganyika na Zanzibar kabla ya Aprili 26, 1964, waliozaliwa baada ya tarehe hiyo na wazazi wawili wa Kitanzania au mzazi mmoja wa Kitanzania na wenye uraia wan chi nyingine na wale watakaotaka kuasili.

  Akizungumzia kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema ya kukataa kuandikwa Katiba mpya, Mtatiro alisema: "Mwanasheria Mkuu hawezi kusema ukweli kwa sababu ananufaika na Katiba iliyopo."
   
 2. T

  Topical JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2010
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono wazo la Wizara zisizidi 15

  Naunga mkon wazo kudhibiti wateule wa Rais na tume huru ya uchaguzi

  Serikali tatu...mm! kwanini isiwe serikali moja.
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  BORA SERIKALI MOJA TU NCHINI KWETU

  Mhe Lipumba kama profesa wa uchumi alipashwa kutambua kwamba aina ya mabadiliko tunayoyataka ni yal ya kuleta ufanisi zaidi na gharama ndogo zaidi.

  Hivyo kupendekeza muundo wa serikali toka hizi mbili tulizonazo kwa sasa hadi serikali tatu ni kututakia janga la kutokua na maendeleo nchini mwetu isipokua ni kuzalisha zaidi NAFASI ZA KAZI KWA VIONGOZI kupata kula zaidi na wananchi ambao tumekua buzi lao kuendelea kuchunwa zaidi na zaidi hadi maziwa kukatika na damu kuanza kutiririka.

  CUF, japo uhuru mnao wa kupendekeza mnachokipenda, mimi naona tukichagua mfumo wa serikali MOJA nchi yetu itapiga hatua haraka zaidi kimaendeleo. Isitoshe, kuifufua TANGANYIKA sasa hivi kwa ulimwengu huu wa bishara za ushindani mkubwa duniani WATANGANYIKA itatuchukua miaka mingi mno for RE-BRANDING as a nation within a nation mpaka kuja kukubalika kimataifa.

  Cha msingi hapa; tutumie mfumo wa Ki-Marekani (Federal System) na maeneo mbali mbali nchini yapitiwe upya kisheria na kupewa hadhi ya kua STATES with GOVERNORS wa kuziongoza lakini Rais wa The Republic of United States of Tanzania (UST) [ambayo kiswahili chake kitakua ni Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwenye uhalisia zaidi] awe mmoja ili kuimarisha zaidi umoja wetu kitaifa.

  Nasema hivi kwa sababu baada ya mabadiliko yote kukamilika wananchi tutakapojiuliza swali 'HOW BETTER OFF ARE WE AFTER REVIEWING OUR GOVERNANCE SYSTEM' jibu hapa linatakiwa lisije likawa la kutafutiza tafutiza tu na watu kujiumauma.
   
 4. N

  Nonda JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Hapo red,
  Huu ndio mfumo wanaupendekeza. yaani iwepo state of Tanganyika na state of Zanzibar

  Brand name ya Tanzania haitaondoka, ndio hilo shirikisho.
  Au unasahau kuwa Muungano huu ni wa state of Tanganyika na State of Zanzibar?

  Nyerere angeacha usanii na kiini macho walipoanzisha huu muungano leo tusingezungumzia serikali moja. Huwezi kufuta taifa la mwenzako bila kupata migogoro.

  Pia kuwepo kwa Tanganyika na institutions zake kutaondoa mazingaombwe ya muungano tulionao. Au tunapenda changa la macho liendelee?
   
 5. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #5
  Dec 30, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  ndiyo maana kuna haja ya debate on new katiba!
   
 6. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Federal system hiyo inatakiwa ipanuliwe zaidi kuliko huko wali. Hatupashwi kufuata moja kwa moja ule ule muunda wa wakati ule wa mwaka wa 1961 nchini mwetu.

  Ukweli unatokana na mambo mengi sana ambapo ni sharti TUWE VERY REALISTIC kuvisimamia ipasavyo kama vile:

  1. Wakati wa Muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika Wazanzibari walikuo 582 wakati Wa-Tanganyika walikua zaidi ya milioni 18. Leo hii Wazanzibari wakaribia milioni 2.5 wakati Watanganika tumezidi milioni 39.

  Sasa kwa kuwa rasilmali ardhi siku zote haiongezeki, Wa-Tanzania Zanzibar walio wengi sasa Visiwani kumekia tu jina ila makazi yao rasmi na ya kudumu kwa sasa ni Mwanza, Dar Arusha na kwingineko. Siku hizi mara watembeleapo Visiwani ni kusahahi tu maramoja na kurudi. Mfano mzuri ni Mzee Jumbe alihamia Kigamboni tangi miaka hiyo. Leo hii ukiwaambia watoto wake mathala kwamba Muungano umevunjwa na kwamba sheria inawataka kurudi visiwa kamwe hawatakuelewa.

  Kwa mantiki hiyo hapo juu, yeyote anayezungumzia Muundo wa utawala wa nchi yetu ni sharti akatandike chini mambo yote ya msingi, kuyafanyi uchambuzi wa kina bila kuleta SIASA WALA ITIKADI MLE NDANI ndipo ujenge hoja kwa nini unafikiri unavyofikiri juu ya jambo hili

  Hivyo ndi maana nikapendekeza swala la FEDERAL SYSTEM ambayo kidogo ina mjumuiko tofauti kidogo na ule wa Wa-Tanzania wenzangu wa chama cha CUF (hata hvyo nawapongeza sana kuona haja ya kuimarisha umoja wetu kitaifa). Kwa kuzingatia ukweli kwamba Wa-Tanzania Visiwani sasa hivi wametapakaa karibu katika kila kona ya Tanzania Bara kiasi cha kutoweza kuwahamisha kwa sababu yoyote ile basi ni bora Tanzania tukaanza FEDERAL SYSTEM chini ya SERIKALI MOJA TU.

  Mikoa yote ya sasa yakageuzwa STATES with semi autonomous Governors na kule Visiwani tukawa na Unguja State na Pemba State na kwamba ndani ya kila State tukawa Counties ambazo zina vikao vyao huko huko. Na kwa kujipanga upya huko kukawa na Bunge za aina mbili kitaifa.

  Wazee tukijipanga hivi bila kuleta siasa za ajabu ajabu nakuambia the END RESULT ITAKUA IN UMOJA WA KITAIFA ULIOIMARIKA ZAIDI, taifa ambalo watu wake tuko happy na bila Waunguja wala Wapemba kuhofia tena KUMEZWA.

  Think over this taratibu.
   
 7. C

  CHE GUEVARA2 Member

  #7
  Dec 31, 2010
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wacha kuongea longolongo wewe na ndoto zako za kingwendu hizo..........Zanzibar itabakia kuwa nchi huru na dola yake kamili kama hapo awali ilivyokuwa ikiitwa JAMHURU YA WATU WA ZANZIBAR na walipata uhuru wao kihalali na kuwa na kiti chao ndani ya United Nation!!!!!
  Hakuwa Adui yeyote yule anaeweza kulivunja Taifa la Zanzibar alishindwa mzee Julius Nyerere sasa nani mwengine anaeweza kulivunja Taifa la Zanzibari na mataifa yote ulimwenguni wanaitambua kama Zanzibar ilikuwa ni nchi huru na dola yake!!!!!
  Ameshindwa Muengereza kulivunja taifa la wa Scotishna mpaka hii leo Scotland ni nchi kamili na dola yake huru...waliungana na wa british miaka 100 iliyopita ili kuufanya United Kingdom lakini hadi hii leo wako na nchi yao huru!!! iweje Wazanzibar walivyokuwa wakaidi na siasa za mvutano:A S-alert1:
   
 8. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #8
  Jul 10, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  208238_10150146352486176_721596175_6946057_2281263_n.jpg Sunday, 10 July 2011 09:10
  Leon Bahati, Dodoma
  MTAZAMO tofauti miongoni mwa wabunge umeendelea kuwa chachu ya kutaka kuvunjwa kwa muungano wa Tanzania.Hali hii imejionyesha wazi wiki hii katika mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma baada ya wabunge kuvutana kuhusu hatima yake, huku baadhi yao wakitaka uvunjwe na kuundwa upya na wengine kuutetea.Chanzo cha mvutano huo ni kufutia baadhi ya wabunge kutoka Zanzibar kuubeza na kuonyesha wazi kuwa Tanzania bara inanufaika zaidi kuliko visiwani.

  Hoja hii si tu kwamba iliwakoroga wabunge wa bara, bali pia wananchi walioisikia wamekuwa wakihoji sababu za wabunge hao kuubeza muungano kana kwamba hauwasaidii.

  Kauli tata kuhusu muungano ambazo kwa ujumla zinadhoofisha uhusiano baina ya pande hizo mbili, ulianza muda mrefu hasa baada ya nchi kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya saisa na unaendelea kukua kadiri muda unavyosonga mbele huku Serikali ikifanya jitihada za kuunusuru.


  Katika mvutano ulioibika bungeni wiki hii, wabunge wa Chadema na baadhi wa Chama cha Wananchi (CUF), walioonekana dhahiri kutaka muundo wa sasa wa Muungano huo uvunjwe na kuundwa mwingine wenye serikali tatu; Tanganyika, Zanzibar na Serikali ya Muungano.

  Hata hivyo, mfumo huo umekuwa ukipingwa kila mara kwa vile ni sawa na kumwondole madaraka na nguvu Rais wa shirikisho kwa vile hatakuwa na uwezo kuingilia mambo ya ndani ya serikali ya mbili zitakaozoundwa.

  Hata hivyo, wakati wabunge hao wakitetea hoja hiyo, wengine kutoka Chama tawala CCM, na baadhi ya mawaziri akiwamo Samuel Sitta wa Afrika Mashairiki, walisimama kudete kuutetea.

  Hoja za wabunge
  Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, alishutumu tabia ya viongozi waliopo madarakani kuficha ukweli juu ya suala zima la muungano akiweka bayana kuwa sasa ni wakati mwafaka Watanzania wakajadili hatima ya Muungano huo.

  Akitumia vitabu vya watu mashuhuri kama vile Rais wa Pili wa Zanzibar, Aboud Jumbe na Profesa Issa Shivji, Lisu
  alisema matatizo na kero nyingi zinatokana na baadhi ya mambo kutowekwa wazi.

  Alitaja baadhi ya mambo aliyosema siri kuwa ni juu ya Mapinduzi ya Zanzibar na lengo hasa lililolazimu uwepo wa muungano huo.

  Mambo mengine alisema ni kuingizwa kinyemela kwenye katika ya Tanzania vipengele kuanzia cha 11 hadi 22.

  Halima Mdee wa Kawe, alisema kero za muungano zimekuwa hazitatuliwi kutokana na waziri mwenye mamlaka ya muungano kupuuzwa na viongozi wenye mamlaka ya juu katika kuamua kusu suala hilo.

  Aliwataja viongozi hao ambao alidai hawana muda wa kutulia ili kutafuta ufumbuzi wa kero hizo kutokana na kuwa na kazi nyingi kuwa ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar.

  Alilalamika kuwa kutokana na hali hiyo ni kero sita tu zimetatuliwa, huku saba ambazo ni za msingi, zikiendelea kupigwa danadana.

  Miongoni mwa kero hizo sugu, alizitaja kuwa ni suala la mafuta, ushiriki wa Afrika Mashariki na suala sahihi za waanzilishi wa Muungano huo.

  "Suala la kodi mbili ni kiini macho na kwamba wananchi wengi wamekuwa wakiathirika kutokana na tatizo hilo," alieza Mdee ambaye alipendekeza Katiba ijayo kuwa na mwanga wa kutatua kero za muungano.

  Mohamed Amour Chomboh (Magomeni) alitamba kuwa yeye ni miongoni mwa watu wachache walioshuhudia Mapinduzi ya Zanzibar yalivyofanyika na anatambua ni muhimu kuenziwa.

  Alisema anaona kuna umuhimu wa muungano huo kuendelea kudumu lakini, akaasa kuwa kero zake zimekuwa ni tishio kubwa hasa kwa maslahi ya Zanzibar.

  Alilalamikia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwa ndio moja ya kero ambazo zinaweza kusababisha Wazanzibari waje juu na hata kutaka kuvunja Muungano.

  Alisema Zanzibar inategemea zaidi bishara kwa ajili ya kuimarisha uchumi wake na kwamba TRA ndiyo imekuwa ikisababisha biashara kudorora visiwani humo.

  Waziri atwishwa mzigo
  Jaddi Sumail Jaddi (Mkwajuni-CCM) alisema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Hassan Suluhu ,ambaye ni Mzanzibar alikabidhiwa nafasi hiyo kama mtego wa kumbebesha lawama za kero za Muungano ambazo zinalalamikiwa na Wazanzibar.

  "Ndugu yangu Samia ni mchawi aliyepewa mtoto amlee akimnyonga, alamumiwe yeye," alisema Jaddi.
  Sitta alisema huo ni upotoshaji na kwamba alipewa kazi hiyo kwa vile Serikali inaamini kwamba ana uwezo wa kuifanya kazi hiyo.

  Yalikuwepo malalamiko kwamba Wazanzibar wanaoajiriwa Bara ni wachache, lakini Sitta alipinga akitoa mfano wa wizara yake ina maofisa wakuu wa idara 12 na kati ya hao, wanne ni Wazanzibari.

  Sitta awatuliza
  Munkali wa wabunge hao ni kama ulizimwa na
  Sitta ambaye alifanikiwa kubadili kabisa hali ya hewa iliyokuwa inaashirikia kuwa wabunge wengi wanataka Mungano huo uvunjwe.

  Akichangia mjadala huo Sitta alisema siku ambayo Watanzania wataamua kuwa na serikali tatu za muungano, itakuwa ndiyo tiketi ya kuuvunja muungano huo.

  "Kuunda tena Tanganyika ni kutengeneza mbia mwingine atakayekuwa anashindana na Zanzibar," alisema Sitta.

  Alifafanua kuwa hali hiyo itajenga mazingira ya mvutano kwa serikali ya Tanganyika na Zanzibar wa kila mmoja kupigania maslahi yake na Serikali ya Muungano haitakuwa na nguvu kwa sababu uwepo wake utategemea pande hizo mbili.

  Alitoa mfano akisema linaweza kujitokeza suala la kuchangia uendeshaji wa Serikali ya Muungano na hapo yanaweza kujitokeza malalamiko kwamba pande zote zigharimie sawa kwa sawa na hapa Zanzibar ndiyo itakayonyanyasika.

  Sitta ambaye alikuwa Spika katika Bunge lililopita alionya akisema kama ni mpango wa kuunda serikali tatu ni bora waridhie kabisa muungano usiwepo na serikali zote zijitegemee.

  Alitaka ieleweke kwamba wakati inaonekana kuwa Wazanzibar ndio wanaoonekana kulalamika sana wakati huu kwamba wananyimwa maslahi yao lakini ukweli wapo Watanzania Bara ambao nao wanalalamika vivyo hivyo ila nguvu hiyo inapungua kutokana na kuwepo serikali mbili.

  Amtetea Nyerere
  Kuhusu Baba wa Taifa kuwa dikteta, Sitta alisema kuwa huo ni upuuzi kwa sababu yapo matendo mengi ambayo yanaonyesha hakuwa mlafi wa madaraka na badala yake alipenda haki kwa wananchi wake na bara la Afrika kwa Ujumla.

  Alitoa mfano kuwa kama angekuwa dikteta angeweza kuamua kufuta kabisa uwepo wa serikali ya Zanzibar.
  "Lakini alikubali iendelee kuwepo serikali ya Zanzibar ndani ya Muungano," alisema Sitta ambaye pia ni mbunge wa Urambo Mashariki.

  Katika kuelezea kuwa Karume hakuwa mtu wa kuburuzwa alisema, Tanzania ilipoishiwa akiba ya fedha za kigeni na kwenda kuiomba serikali ya Zanzibar iwapatie kwa sababu wao walikuwa nazo nyingi kutokana na mauzo ya karafuu, alikataa.

  Kuhusu suala la picha ya siku ya Muungano kuonekana Mwalimu Nyerere peke yake akichanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar, Sitta alisema ni suala tu la heshima ambalo alipewa kutokana na wadhifa wake wa Rais wa Muungano.

  Alifafanua kuwa siku hiyo waliteuliwa watu wawili, mwanauma na Mwanamke, kutoka pande zote kushiriki katika kufanikisha tukio hilo lililoandika historia ya Tanzania.

  Hoja nyingine aliyopangua ni ile ya wabunge wengi kueleza kuwa katiba ilibadilishwa ili Rais wa Zanzibar asiwe tene Makamu wa Kwanza wa Rais tofauti na makubaliano ya waasisi wa muungano kwa hofu ya CCM kwamba Rais wa visiwani anaweza kutoka chama cha upinzani.

  Sitta alisema ukweli ni kwamba mabadiliko hayo yalitokea baada ya kuona kwamba nafasi hiyo ya pili itaonekana kuwa ni ya Wazanzibari tu, kwa vile serikali ya Zanzibar daima itaongozwa na mzanzibar.

  Zanzibar na OIC
  Kuhusu suala la kutaka Zanzibar iruhusiwe ijiunge na Jumuia ya Nchi za Kiislamu Duniani (OIC) kwa vile Tanzania imeamua kutofanya hivyo, Sitta alisema tatizo ni kwamba kanuni haziruhusu.

  Alisema kwamba OIC ilikataa kufanya hivyo kwa vile sheria zao ni kujenga ushirikiano na serikali ile inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa.

  Kuhusu kipengele cha kwanza hadi 11 viliundwa kwa makubaliano ya pande zote lakini baadaye kifungu cha 12 hadi 22 vikaingizwa kinyemela, Sitta alisema, sio kweli.


  Kwa mujibu wa Sitta vipengele hivyo vilitokana na kuvunjika kwa Jumuia ya Afrika Mashariki 1977 ambapo baadhi ya mambo mengi yaliyokuwa yanasimamiwa na ushirikiano huo yalibaki bila usimamizi.

  Alitaja miongoni kuwa ni Shirika la Posta, reli, bandari na ndege ambapo Tanzania Bara ilibidi iyabebe baada ya rais wa Zanzibar kuridhia.

  Hata hivyo alisema Tanzania bara ilibeba jukumu hilo kwa gharamna zake bila kuishirikisha Zanzibar hiyo ikawa ni nafuu kwa Wazanzibar kwa sababu faida zake zinaenda pande zote za Muungano.

  Kama hiyo haitoshi, Sitta alisema rais wa Zanzibar aliiomba Bara ianzishe pia elimu ya juu kwa sababu isingeweza kufanya hivyo kutokana na uwezo wa kifedha.

  Akipinga malalamiko kwamba Zanzibar haina uwakilishi kwenye Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC), Sitta alisema katika vikao vyote vya majadiliano visiwa hivyo vimekuwa na uwakilishi.

  Isitoshe akasema kuwa katika kuthamini Zanzbar, EAC inajiandaa kuwekza katika miradi mitatu visiwani humo ambayo ni ujenzi wa kiwanja cha ndege cha kimataifa Pemba, ujenzi wa Bandari ya Maruhubi na chelezo ya kusafirisha mizigo na magari Zanzibar, Mombasa na Dar es Salaam.
   
 9. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #9
  Jul 10, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  @ Wabunge wetu kutoka Zanzibar
  Sina budin ila kuwapongeza Wabunge wote walioanzisha jeke jeke hili la Kutaka Serikali Tatu au Muungano Uvunjwe. Tunawapongeza na tunataka hizi kelele ziendelee, wala msimsikilize Sita wala saba. hao watanganyika wanatetea Nchi yao na maendeleo ya Tanganyika ambayo inatumia badget kubwa sana ya Serikali ya Muungano ambayo kuwepo kwake haipo. bali nio Tanganyika kutumia koti la Muungano.
  @Sitta
  Yote anayoyasema ni sababu za uwongo zilizokua hazina uzito wala muelkekeo, hapo chini nitanukuu kipengele kimoja kimoja alichoeleza Sitta na nitavifafanua kwakutumia Mifano ya nchi nyengine zilizoungana.
  Nanukuu maneno ya Samuel Sitta.
  "…Akichangia mjadala huo Sitta alisema siku ambayo Watanzania wataamua kuwa na serikali tatu za muungano, itakuwa ndiyo tiketi ya kuuvunja muungano huo.
  "Kuunda tena Tanganyika ni kutengeneza mbia mwingine atakayekuwa anashindana na Zanzibar," alisema Sitta.
  #. Kipengele hichi hapa hatutaki Ubia wala ushindani kwani Muungano sio Biashara baina ya Tanganyika kuinyonya Zanzibar wala Zanzibar kuitegemea Tanganyika. Bali Nikuunda Udugu na Usala wa Nchi zetu mbili ambazo zitakuwa na thamani ya Utaifa wake, historia na silka zao. Hapa ndipo tutakua na majivuno na kulinda mipaka yetu . Kwa upande wa Tanganyika kumekuwa na wimbi la wageni kutoka Kenya, Uganda, Malawi, Burundi, zambia na hata Congo.
  Kuwepo kwa Serikali ya Tanganyika kila mkoa watakua responsible wakulinda mipaka yao kwakusaidiwa na hii serikali ya Muungano itakayokua katikati. Na kwa upande wa Zanzibar Wazanzibari watatakiwa kufanya hivo. Ikiwa JWT litakua la Muungano hakuna haja ya Majeshi wote na askari wenye asili ya Kizanzibari kuhamishwa. wanatakiwa wabaki zanzibar na walinde mipaka yao. Kuundwa kwa serikali TATU ndio njia pekee yakuimarisha udugu na kuheshimu Historia zetu na mial zetu.
  Mfano :
  UK wanafanya hivo Walles, Scotlands na Northen Island. Wanaserikali zao na mambo yao wanaamuliwa kwa Devolve government zao. Kama ni Compitistion ya Bishara kila mmoja ana haki yakuimarisha uchum,i wake kwayale mambo yasio ya Muungano.
  Muungano wa Scandanevia nao uko hivo hivo Danmark ni nchi yenye population ya watu Million 5 tu na mbona haijamezwa na Norwa au Sweeden? Kila mtu anapasi yake na wanamashirika ambayo yanaunganisha ile Scandanevia na kila mmoja anfaidika.
  Kuhusu kuchangia serikali ya Muungano nakusema itatakiwa kila mmoja achangie sawa sawa. Yes Lakini hjapa mambo yanayoshikiliwa na Muungano hayatokua mengi sana kama yalivo sasa hivi na Raisi wa Muungano hana haja yakuwa MFALME kama alivo sasa. Kwahiyo hapo tutafungua milango ya Biashara baina yetu na Tanganyika na kila raiya atakua naipatia nchi yake GDP. Mfano Mzanzibari akifanya kazi Tanganyika katika kazi iliokua ya Muungano au sio ya Muungano inabidi alipe kodi ya GDP ile ya Tanganyika. Na Mtanganyika atatakiwa kufanya hivo2.
  Wazalendo Jiulizeni hivi sasa ni Wakenya wangapi wanopmiliki Hoteli na Maskuli Zanzibar na wala hawalipi Kodi kama inavbotakiwa kwamba wao ni Wageni?
  WAzalendo jiulizeni ni Watanganyika Wangapi wana vilabu vya Pombe na wanafanya Biashara bila yakulipa kodi. Mfano mdogo ni uchafuzi wa Mji Mkongwe na Vinyago mbona ikifika jioni hawasafishi na badala yake ni Baraza la Mji wa zanzibar ndio wanaosafisha pale Ngome Kongwe. Nani anelipa kodi ya Baraza la Mji wa zanzibar sio Mkenya wala Mtanganyika ni Mzanzibari Mlala hoi.
  # Kipengele chengine Sitta alichotetea ni hiki.
  "…Alifafanua kuwa hali hiyo itajenga mazingira ya mvutano kwa serikali ya Tanganyika na Zanzibar wa kila mmoja kupigania maslahi yake na Serikali ya Muungano haitakuwa na nguvu kwa sababu uwepo wake utategemea pande hizo mbili."
  Hili la Serikali ya Muungano kutokua haina nguvu hivi ndivo tunavotaka kwani Serikali ya Muungano inatakiwa ishulikie mambo machache tu na sio kujibebesha Mzigo na kuwanyanyasa Watu. Hivi sasa Raisi amekuwa akienziwa kama Firauni au Mfalme hakuna sheria yoyote inayombana hata kama wataiba kura au kula Rushwa Raisdi anlindwa. Tutakapokua na Serikali TATU Tanganyika naamini kwa timu ya Wasomi Vijana kutoka CHADEMA wataweza kuiendesha Nchi yao ya Tanganyika na tukawa na Serikali ya Muungano katikati isiokua na madaraka makubwa.
  Wazanzibari Sitta anasema haya kwasababu anajua Serikali ya Tanganyika ipo na haijafa kama tunavodai . Bali inatumia mwamvuli wa Muungano kuendesha mambo yake na Kuikandamiza Zanzibar. Wakati Umefika Watanganyika wengi Wasomi hawataki Muungano huu uliopo na Wazanzibari ni hivo hivo. Muungano wa Nyerere na Sitta umepitwa na wakati ni lazima Wananchi wea pande zote mbili wasikilizwe. wazanzibari hatuko tayari kuona kwamba Zanzibar inafyonzwa na Serikali ya Tanganyika kwa koti la Muungano.
  "…Alitoa mfano akisema linaweza kujitokeza suala la kuchangia uendeshaji wa Serikali ya Muungano na hapo yanaweza kujitokeza malalamiko kwamba pande zote zigharimie sawa kwa sawa na hapa Zanzibar ndiyo itakayonyanyasika."
  Kuhusu kuchangia the Government of United Kingdom ina badget yake ndogo ya Muungano huo na inakwenda bila yamatatizo as long as each country they would have their own Devolve Government & its own parliament. Bunge lilioko sasa sio la haki kwani lnaupendeleo wa Serikali ya Tanganyika.
  Mfano nikutoa ruzuku kwa Makanisa. Mbona misikiti haina ruzuku inayotengwa na Serikali au kusimamiwa na Serikali? Iweje kundi fulani la watu wapewe support ya kila aina na kundi jengine lifanywe watoto wa Kambo.
  Sitta Muungano umefikia ukingoni na ukijitia kuulazimisha utakuja kukosa mtoto na maji ya moto.
   
 10. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Chadema wataka SERIKALI TATU viongozi wa ccm Pinda na sitta wachanganyikiwa bungeni View attachment 33967


  Juzi bungeni mbunge mmoja wa chadema Lissu alilitikisa sana bunge kuhoji muungano,baadhi ya wabunge kuunga mkono serikali tatu na kuwe na serikali ya shirikisho,sitta alikerwa sana na hili na kuhofia kuwa pindipo tanganyika itarudi zanzbar itapata mbia wake na serikali ya muungano itakuwa haina nguvu hata rais wa muungano pia.

  Hii hoja naona ni dhaifu kwa sababu nchi zote duniani zimekuwa na ushindani katika suala la development na democracy,sasa hpa kwetu viongozi wetu kama Pinda na Sitta wanaogopa hili,kwa nini ?

  Pia Pinda amesema kuwa hatopendezewa pia kuwepo serikali tatu,na amesisitiza kuwepo na serikali mbili ya muungano na serikali ya zanzibar na alisisitiza kuwa wananchi waitambue zanzbar kama mshiriki wa muungano na inatambulika kama ni nchi katika jamuhuri ya muungano,sasa suali ni kwamba huyu Mizongo pinda yeye si ndie aliwahi kutamka kuwa zanzibar sio nchi ?Au leo kasahau ?

  Naona viongozi wa muungano tanganyika/tanzania wakati huu katika mchakato huu wa katiba wamechanganyikiwa,wabunge wa pando zote mbili wanahoji juu ya siri ya muungano na kutaka kuwepo na mfumo wa serikali tatu ili kuondoa kero za muungano.

  Wazanzibar wame stick pale pale kuwa serikali tatu au kuvunja muungano, HATA BADO VIONGOZI NAONA WATAPATA STROCK.
   
 11. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #11
  Dec 22, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  December 10, 2011Posted by zanzibardaima in Politics. Makala hii ya Ahmed Rajab[​IMG]
  Baadhi ya Wazanzibari waliojitokeza mapema mwaka huu kupinga Muungano hadharani. Kwa wao, chaguo la kwanza ni kutokuwa na Muungano, la pili ndio serikali tatu, hawataki kuuona wa serikali mbili wa sasa wala kuusikia wa serikali moja

   
 12. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #12
  Dec 22, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  December 10, 2011

  Posted by zanzibardaima in Politics.
  Makala hii ya Ahmed Rajab

  [​IMG]
  Baadhi ya Wazanzibari waliojitokeza mapema mwaka huu kupinga Muungano hadharani. Kwa wao, chaguo la kwanza ni kutokuwa na Muungano, la pili ndio serikali tatu, hawataki kuuona wa serikali mbili wa sasa wala kuusikia wa serikali moja

  Kwa vile Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba umepitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, muswada huo utatekelezwa mara tu utapomalizika mchakato wa kuufanya uwe sheria kamili. Muswada huo ambao ni muhimu sana kwa watu wa Tanganyika na wa Zanzibar kwa vile utaamua mustakabali wa nchi zao mbili, utatekelezwa kwa mujibu wa ratiba au jedwali itayowekwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


  Kati ya taasisi zote zitazoundwa katika utekelezwaji wa mchakato wa kuiandika upya Katiba mpya ya Muungano, iliyo na umuhimu mkubwa ni ile tume ya wajumbe 30 itakayokuwa na idadi sawa ya wawakilishi kutoka Tanganyika na Zanzibar.

  Hii ndiyo taasisi itayoongoza kupanga na kusimamia huo mchakato mzima. Hali kadhalika itatoa mapendekezo itayokuwanayo juu ya misingi ya mizingo au vigezo na miongozo itayotangazwa na Rais wa Muungano baada ya kushauriana na Rais wa Zanzibar na pia kupata ridhaa yake.


  Miongoni mwa majukumu muhimu sana ya tume au kamisheni hiyo itakuwa ni kazi ya kuuongoza mchakato wa kukusanya maoni ya wananchi katika ngazi za chini kabisa za taifa hili. Huko Zanzibar kazi hiyo itafanyika katika ngazi ya shehia ambapo Wazanzibari watatakiwa watoe maoni yao kuhusu mwelekeo ujao wa nchi yao na pia kuhusu Muungano na Tanganyika.


  Kwa mfano, wale watakaohudhuria mikutano itakayofanywa kwenye shehia zao huko Zanzibar au wataopeleka taarifa zao kwa maandishi kwenye kamisheni au kwa wao wenyewe kuhudhuria mbele ya kamisheni watakuwa na uwezo wa kutoa maoni yao kwa uhuru kabisa bila ya hofu.


  Hali ya mambo haitokuwa tena kama zamani ambapo kaka mkubwa alikuwa akiongoza, akiangalia na hatimaye akijiamulia kuhusu ya sasa na yajayo ya Jamhuri ya Muungano. Kwa kufanya hivyo, kaka mkubwa alikuwa akiamua kuhusu mustakabali wa Tanganyika na ule wa Zanzibar, nchi huru zilizoungana mwaka 1964.


  Vifungu vya muswada huu vinavyotaka pawepo na uwakilishi ulio sawa na ushiriki ulio sawa katika kufikia uamuzi katika mchakato huu vinaitambua ile kanuni ya kimsingi ya uhuru na mamlaka ya nchi hizo mbili pamoja na usawa wao. Utambuzi huo ni juu ya msingi wa kanuni za sheria za kimataifa pamoja na sheria za taifa hili.


  Ninasema hivi kwa sababu Hati za Muungano ni mkataba wa kimataifa. Nathubutu pia kuongeza kwamba Hati hizo za Muungano ndizo nyaraka zilizo muhimu kushinda zote zilizotajwa kuhusika na historia ya utungwaji wa Katiba nchini Tanzania.


  Tuwe wakweli pia na tukumbuke kwamba utungwaji wa Katiba nchini humu umeihusisha zaidi Tanganyika. Historia inakanushwa kwa kupuuzwa kama haipo ile Katiba ya Uhuru wa Zanzibar ya mwaka 1963, iliyopatikana baada ya mashauriano huko Lancaster House mjini London kati ya vyama; Zanzibar Nationalist Party na Afro-Shirazi Party.


  Hali kadhalika, siku ya uhuru wa Zanzibar — Desemba 10, mwaka 1963 — baada ya miaka 70 ya ukoloni wa Uingereza haitambuliwi ingawa siku ya uhuru wa Tanganyika inaadhimishwa na kusherehekewa kuwa ni Sikukuu ya Kitaifa ya Tanzania.


  Katika kuizingatia ripoti yake kamisheni inapaswa kuyatia maanani “maoni yanayolingana na yanayokinzana katika sehemu zote mbili za Jamhuri ya Muungano” (yaani Tanganyika na Zanzibar) kuhusu mustakabali wa Muungano. Itapoangalia dhana nzima ya Muungano ama muundo wake itaona kwamba kuna ukinzani mkubwa kati ya wanachodai Wazanzibari na msimamo rasmi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.


  Kwa bahati mbaya ni taabu kuutaja msimamo wa Watanganyika kuhusu Muungano, na iwapo wanapendelea waendelee nao au wauvunje. Ni taabu kwa sababu inavyoonyesha ni kwamba msimamo rasmi na wa wengi huko Bara katika muda wote huu wa miaka 47 ya Muungano ni kuwa Zanzibar ni mzigo kwa Tanganyika.


  Tusisahau kwamba hali hiyo ilikuwa na ukweli katika kipindi kifupi sana cha historia ya Visiwani pale ilipokuwa kawaida kwa wanadamu kuwatesa wanadamu wenzao, pale wananchi walipokuwa wakinyimwa uhuru wao wa kimsingi na pale nchi hiyo ilipokuwa ikiongozwa na mtu mmoja. Kwa hakika, yaliyokuwa yakitokea Zanzibar kabla ya mwaka 1972 yameutia dosari uungwana na utu wa Mwalimu Julius Nyerere na pia yameitia dosari Tanzania.


  Kamisheni yenye jukumu la kuichunguza na kuirekebisha Katiba imepewa mamlaka makubwa na lazima pachukuliwe hadhari wanapoteuliwa wajumbe wake na uongozi wake. Ni muhimu kwamba iwe huru na isifungamane na Serikali. Pia itambue kwamba itakabiliwa na changamoto nyingi kabla ya kuwasilisha Rasimu ya Katiba kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.


  Atapoipata Rasimu hiyo, Rais ataunda Bunge la Katiba kwa masharti yaliyomo kwenye Muswada wa Mabadiliko ya Katiba. Zanzibar itakuwa na asilimia 30 ya wajumbe kwenye Bunge hilo. Muhimu ni kwamba wajumbe wa Tanganyika na wale wa Zanzibar watapiga kura mbalimbali si kwa pamoja. Na kila upande utahitaji upate ridhaa ya wingi wa theluthi mbili ya wajumbe wake ili rasimu hiyo ya Katiba iweze kufikishwa kwa wananchi watoe uamuzi wao kwenye kura ya maoni.


  Kwa Zanzibar hiyo kura ya maoni itasimamiwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na rasimu ya Katiba itapita endapo Wazanzibari wengi wataikubali.


  Panaweza pakazuka mgogoro wa kisiasa ikiwa, kwa mfano, upande mmoja utaikataa hiyo rasimu ya Katiba mpya. Mgogoro huo utaweza kutanzuliwa kwa vile Katiba ya kale (yaani hii ya sasa) ya mwaka 1977, itaendelea kufanya kazi. Hatua hiyo itakuwa ni ya suluhisho la kisheria tu kwani matatizo ya kisiasa kuhusu mustakbali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yatabidi yatanzuliwe kwa njia ya kirafiki kati ya Tanganyika na Zanzibar, tukikumbuka kwamba katika demokrasia ni matakwa ya watu yaliyo juu na yenye kutawala.


  Inapaswa pia wakubwa wakumbuke ya kuwa kinyume cha miaka ya nyuma watu hawana tena hofu visiwani Zanzibar. Vilevile kinyume cha miaka ya nyuma vyama vya kisiasa vyenye matawi yao Zanzibar haviwezi tena kuwafukuza wenzao wa Visiwani au kuwatisha. Wala wale wenye kutokubaliana na msimamo rasmi wa kisiasa au wa kiitikadi hawafikiriwi tena kuwa ni wahaini wa Taifa la Tanzania.


  Hivyo inatia moyo kuona kwamba Wazanzibari kwa mara ya kwanza katika historia yao ndani ya Muungano na Tanganyika, wamepewa haki yao ya kuwa washirika sawa. Pongezi ni kwa Wazanzibari wote na hasa viongozi wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, na wale wenye kuhusika na mambo ya kikatiba na kisheria ambao kwa mara ya kwanza wametoa mapendekezo yanayolinda maslahi ya nchi yao.


  Kuna hofu Zanzibar kuhusu namna kura ya maoni itavyoendeshwa na jinsi orodha ya kudumu ya wapigaji kura itavyotumiwa. Pia kuna manung’uniko mengi kuhusu kutolewa kwa vitambulisho vya ukaazi. Hofu iliyopo ni kwamba wasio Wazanzibari huenda pia wakashiriki kwenye kura ya maoni ijapokuwa sheria inasema wazi kwamba kutakuwa na kura mbili za maoni: moja kwa Watanganyika na nyingine kwa Wazanzibari.


  Msimu wa kampeni umekwishaanza na kuna wengi Visiwani ambao wamekwishafikiria masharti magumu kuhusu Muungano na muundo wake wa baadaye na iwapo uendelee kama ulivyo sasa au la. Hili linapingwa na Wazanzibari wengi lakini inavyoonyesha ni kwamba viongozi wa Tanganyika wangependelea uendelee ulivyo, na pengine, hata baadaye, kuitimiza ndoto yao ya kuwa na serikali moja tu kwa sehemu zote mbili za Muungano, yaani Tanganyika na Zanzibar.

  _________________________________________________________________________________________________________

   
 13. T

  Topical JF-Expert Member

  #13
  Dec 22, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Sawa kabisa, nimategemeo yangu kuwa maamuzi ya wananchi yataheshimwa at the end

  Kama ni serikali tatu well and good kama kuvunja muungano well and good
   
 14. gambachovu

  gambachovu JF-Expert Member

  #14
  Jan 15, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,865
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  mkuu,kuna option nyingine ya muungano kama United States... So kwa kuwa muungano hautakiwi uvunjike,so bora huu,au wa serikali tatu..
   
 15. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #15
  Jan 15, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,775
  Likes Received: 6,108
  Trophy Points: 280
  ...
  Katika kongamano hilo lililofanyika Ijumaa iliyopita katika ukumbi wa Diamond Jubilee, imeelezwa kuwa kama Watanzania wanaona kuna haja ya kuwa na katiba mpya, basi kwa Watanzania Waislamu haja hiyo ni maramia zaidi, kwani katiba iliyopo, ndani ya miaka 50 imekuwa ni kikwazo katika kupata haki zao za msingi. Kwa maana hiyo Waislamu wametakiwa kutumia fursa ya kutoa maoni yao katika tume ya kukusanya maoni ya kuundwa katiba mpya ili masuala ya Kiislamu ambayo yanalalamikiwa kwa muda wa nusu karne yaingizwe katika katiba hiyo.

  Akizungumza katika Kongamano hilo, Sheikh Suleiman Kilemile alisema, sasa umefika wakati fursaya kutoa mapendekezo yapi yanafaa kuingizwa katika Katiba mpya na yepi hayafai kuingiza imepatikana, hivyo akawataka Waislamu kutumia fursa hiyo aliyoilinganisha nadhahabu. “Ili udhalili na unyongekwa Waislamu uondoke, ni lazima Waislamu mtoe maoni yenu yafanyiwe kazina yaingizwe katika Katiba mpya. Sisi ni Watanzania ambao tunashiriki katika harakati zote za kinchi ikiwamo kulipa kodi nakutekeleza haki zote za kiraia. Sasa ni jambo la ajabu kuwa nasi tuna mahitaji yetu kisha yanafumbiwa macho kwa kigezo katiba hairuhusu” Alisema Sheikh Kilemile. Kilemile aliitaka Tume ya Serikali ya kukusanya maoni itakapo anza kazi yake izingatie maoni ya Waislamu, vinginevyo tatizo litaendelea na Katiba hiyo itakuwa bado ni mbovu.

  Alisema, ili Katiba iwe kamili na kuepusha mayowe na malalamiko ni vyema yakaingizwa mapendekezo ya Waislamu na ya watu wote mmoja mmoja na yale ambayo yatajumuishwa kupitia Jukwaa la Waislamu la Kuratibu Mabadiliko ya Katiba. Sheikh Kilemile aliwataka Waislamu kutoa maoni ya uhakika, maoni ambayo haswa ni kero na ni matatizo ya Waislamu, hivyo aliwataka kuorodhesha matatizo halisi ya Waislamu na Uislamu humu nchini ili hapo baadae yaweze kupatiwa ufumbuzi kupitia muongozo wa katiba.

  Alisema, kwa upande wa Uislamu wenyewe wapo watu wanaodhani kuwa Uislamu ni dini ambayo inatenganisha kati ya maishana roho, ilihali Uislamu ni dini na roho. Akifafanua hayo kupitia Qur an, 110-Al imran, Sheikh Kilemile alisema, Mwenyezi Mungu amewataja Waislamukuwa ni umma ulio bora kwa sababu wana kitabu (mwongozo) hivyo alisemakupitia humo maadili ya Uislamu yanakidhi haja kwa binaadamu yoyote yule.

  Aidha, alisema nusu karne iliyopita imepita kwa matatizo mengi kwa Waislamu na histori ipo wazi na kikwazo kikubwani katiba iliyopo sasa, hivyo basi aliwasihi Waislamu kuwa makini kutumia fursahii na kuifanya nusu y akarne inayokuja iwe nzuri kwao na vizazi vijavyo.

  Naye Amir wa Baraza Kuu la Jumiya na Taasisiza Kiislamu, Sheikh Mussa Kundecha, akieleze kazi kubwa ya Jukwaa hilo mbele ya Waislamu alisema, kazi kubwa ya kwanza n ikuelimisha Waislamu dhana ya Katiba na nini haja ya Muislamu kuwa katika Katiba. Alisema, Muislamu anatakiwa kufahamu pindi anapozungumzia Katiba anazungumza kitu gani na pale atakapotakiwa kutoa maoni yake aseme manenoya namna gani. “Waislamu kama jamii ya Watanzania yapo mambo yao muhimu ambayo yanatakiwa kuhakikisha yameingia na kukubalika katika katiba kwa sababu ndiyo yatakayo tuhakikishia mustakabali wa umma wa Kiislamu, kwa muda wote katiba hiyo itakapokuwa inafanya kazi.” Alisema Amir Kundecha.

  Sheikh Kundecha, alisema endapo maoni ya Waislamu hayakuingizwa katika Katiba mpya ama kwa bahati mbaya au kwa makusudi, ni wazi Katiba hiyo itakuwa haijawa halali kwa Watanzania.

  Kwa upande wake Maalim Ally Bassaleh, ambaye pia Makamu Mweyekiti wa Jopo la Jukwaa hilo, akiongea katika kongamano hilo alisema, Katiba ndiyo muongozo wa msingi kuweza kuongoza wananchi katika nchi. Akifafanua zaidi, alisema Katiba hiyo pia ndio mkataba baina ya viongozina wananchi, hivyo alisema, Waislamu ni muhimu sana kushiriki kutoa maoni yao wakizingatia kuwa ni sehemuya jamii ya Watanzania.
   
 16. k

  kipinduka Senior Member

  #16
  Jan 15, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni vzr lkn mna hakika yatafanyiwa kaz mawazo yenu,kwan viongoz weng wa kiislamu ni vigeugeu vlevle waache ku2miwa na vyama vya siasa ktk kufanya maamuz ya waislam
   
 17. M

  Mkira JF-Expert Member

  #17
  Jan 15, 2012
  Joined: May 10, 2006
  Messages: 425
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35


  Mie NINAWASHAURI WATANGANYAIKA KWA WINGI WETU NI AMA SERIKALI MOJA YENYE MAJIMBO YAKIWA NA MAGAVANA WAO NA RAISI WA NCHI MMOJA KAMA MAREKANI AU MUUNGANO UVUNJIKE. SERKAILI YA ZANZIBAR LIWE JIMBO TUMECHOKA KUBEBEMBELEZA HAO AMBOA NDIO FIRST BENEFICIARIES NA FIRST COMPLAINERS. NITWASHAANGAA SANA WATANGANYIKA KUKUBALI KUBULUZWA KWANI MUUNGANO NI WA NINI HASA?
   
 18. w

  wail Member

  #18
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  watanganyika mukiwa hamutaki muungano wazanzibar ndio watafurahi zaidi kwasababu asilimia kubwa ukiwauliza hawautaki
   
 19. g

  giggs Member

  #19
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  nani kakwambia anataka serikali tatu!!! mbili matatizo kila siku kero za muungano, hapa tunahitaji serikali moja..... kama hakuna basi tatu impossible...
   
 20. logbes

  logbes Member

  #20
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kumbuka Muungano lazima/muhimu/nashauri uwepo ila sababu zipi unafikiri za muhimu katika kutetea hoja ya serikali moja au tatu. mbili ndo hizi zilizozaa sintofahamu mpaka leo kwa hiyo haifai.
   
Loading...