..yaani Maalim Seif amiliki mashamba makubwa makubwa pamoja na majumba huku Tanganyika, lakini Prof.Lipumba hana ruhusu ya kumiliki ardhi Zanzibar hata kiduchu?
..una maana gani unaposema kuifuta Zanzibar?
..mimi nadhani mnajenga mazingira ya hofu tu.
..kama kungekuwa hakuna sheria inayoruhusu wa-Znz kumiliki ardhi Tgk basi hakuna ambaye angepiga kelele.
..wa-Znz wanaishi kila mahali kama ulivyoeleza ktk post yako. lakini hakuna nchi yoyote ile iliyopokea wa-Zanzibar wengi kama Tanganyika.
..haiwezekani wa-Znz kwa maelfu mhamie huku Tanganyika, wakati huo huo mkisema hamuwataki wa-Tanganyika ktk ardhi yenu.
cc gombesugu
umekuwa zombi kiasi hicho, hebu tuoneshe wapi Maalim Seif anamiliki ardhi yenu ya Tanganyika...?
Kisha Wazanzibar hatuna udugu na watu mafedhuli, makatili, watwana wa Mrima, kama ni ndoa tunaishia BagaMoyo mbali tunafika Tanga ama Kondoa hao ndio ndugu zetu sisi...!!
..utwana, ufedhuli, na ukatili, upo katika kauli na matendo ya mhusika.
..tabia hizo hazina mahusiano yoyote yale na asili ya mtu, au siyo monopoly ya watu wa eneo fulani.
..dunia yetu imebadilika sana. hatuko katika zama zile za kusema watu wa eneo fulani hawafai, au watu wa eneo fulani ni bora kuliko wengine.
..Huku Tanganyika tumekaribisha wa-Zanzibari zaidi ya laki 3. Wazanzibari hao wanafanya shughuli zao kama wa-Tanganyika bila kubugudhiwa kwa namna yoyote ile.
cc gombesugu
takashi,Naona unachanganya mambo, haki ya kuishi katika inchi ya kigeni na haki ya kumiliki ardhi katika nchi ya kigeni ni vitu viwili tofauti... Maelfu ya wa tngk wanaishi Zanzibar, vile vile maelfu ya wa znz wanaishi tngk...Linapokuja suala la kumiliki ardhi hapo ndio tunatofautiyana.Kwa mfano , Tanzania iwe na uhusiano mzuri na china au India halafu kuwe na makubaliano ya kila raia wa upande mmoja awe na haki ya kumiliki ardhi upande mwengine , sasa hapa nani ataathirika ?
Hata Zanzibar pia Watanganyika wamejaa kila chochoro kwanzia mjini tens stone town mjini wenye sura ya Zanzibar hadi wamejazana wala hawabughudhiwi na mtu, ukienda mashamba utawakuta tena habari hawana, sasa shida ikowapi?
..shida iko kwenye sheria iliyopitishwa na baraza la wawakilishi.
..sheria hiyo haikuzingatia mahusiano ya kindugu baina ya wa-Tanganyika na wa-Zanzibari.
..sheria hiyo inawabagua wa-Tanganyika kwa kuwazuia kumiliki ardhi Zanzibar.
Tatizo lenu Watanganyika hamutaki kuelewa na hii yote nadhani mnajiona kama kwamba Zanzibar ni mali yenu, ila bado tunasema ARDHI sio suala la Muungano, hivyo Zanzibar inapaswa kusimamia ardhi yake, kwa upande wa Tanganyika kwa vile mumeizika hivyo mumehalalisha kila kitu kiwe cha Muungano, hilo kwetu halituhusu ni jukumu lenu kuirejesha Tanganyika yenu iwasimamie mambo yasiyo ya Muungano kwa upande wenu, ila mukilalama kuhusu hili mutatuanya tuelewe kwamba dhamira yenu ilee ya kuimeza Zanzibar, hebu twendeni kwa misingi ya sheria tusihemkwe kwa utashi wetu,
uamuzi bado ila ukifika hali itaonekana tu
Mkuu, mimi kwa kifupi nauchukia huu muungano na huwa nasema wazi siku zote bila kufichatakashi,
..ninachopendekeza mimi ni kwamba wa-Tanganyika waruhusiwe kumiliki ardhi Zanzibar.
..mapendekezo hayo yanatokana na ukweli kwamba wa-Zanzibari wanaruhusiwa kumiliki ardhi huku Tanganyika.
..tuwe na sheria sawa ya kumiliki ardhi. baada ya hapo umiliki wa ardhi utakuwa determined na nguvu za soko[supply & demand].
. gombesugu ametoa mfano wa maeneo ya Marangu na Machame ambako kuna ardhi ndogo. Pamoja na ukweli huo serikali yetu haijapitisha sheria ya kubagua wa-Tanganyika wasio wazawa wa maeneo[marangu,machame] hayo kuhamia huko na kumiliko ardhi huko.
..wa-Tanganyika na wa-Zanzibari wana mahusiano ya kindugu kwa karne kadhaa sasa. Haipendezi mahusiano hayo kuanza kutiwa mushkel ya sheria za kibaguzi kama hii iliyopitishwa na baraza la wawakilishi.
NB:
..Balozi Seif Idi anapigana vikumbo na walalahoi huku Tgk kupata viwanja kule Kigamboni, lakini Prof.Ana Tibaijuka waziri wa ardhi huku Tanganyika hana haki ya kumiliki ardhi Zanzibar.
..Dr.Mohamed Seif Khatib ameuziwa nyumba za serikali ya Tanganyika na waziri John Pombe Magufuli. Nyumba zile hazikuwa na uhusiano wowote na muungano, wizara ya ujenzi si ya muungano. Lakini huyu Pombe Magufuli hana haki ya kumiliki ardhi Zanzibar.
Foum Jnr, W. J. Malecela, Chris Lukosi, Kibunango, Nguruvi3
Kwa kuwa suala la ardhi si la muungano basi hata Wazanzibari walioko bara wasiruhusiwe kumiliki ardhi bara. Wapemba waliojazana bara watambue kwamba wao ni wapangaji tu. Wakamiliki ardhi kwao na si bara!
..shida iko kwenye sheria iliyopitishwa na baraza la wawakilishi.
..sheria hiyo haikuzingatia mahusiano ya kindugu baina ya wa-Tanganyika na wa-Zanzibari.
..sheria hiyo inawabagua wa-Tanganyika kwa kuwazuia kumiliki ardhi Zanzibar.
ya tanzania bara mnawapa wazungu alafu mchukue ya zanzibar ya nini? waachieni ardhi yao
..ndugu yangu, usitetee ubaguzi kwa kisingizio kwamba Tanganyika haipo.
..hata serikali ya Tanganyika ikirejeshwe sitarajii, na sitaunga mkono, kupitishwa kwa sheria yoyote ile ya kuwabagua wa-Zanzibari.
..kuhusu Zanzibar "kumezwa" huko nako ni kuwatia hofu wananchi.
Kutokana na uhaba wa ardhi Kilimanjaro, wakazi wa huko wanahamia maeneo ya mikoa mingine kama Handeni, Korogwe, Arusha, kiteto, Mkuranga.takashi,
..ninachopendekeza mimi ni kwamba wa-Tanganyika waruhusiwe kumiliki ardhi Zanzibar.
..mapendekezo hayo yanatokana na ukweli kwamba wa-Zanzibari wanaruhusiwa kumiliki ardhi huku Tanganyika.
..tuwe na sheria sawa ya kumiliki ardhi. baada ya hapo umiliki wa ardhi utakuwa determined na nguvu za soko[supply & demand].
. gombesugu ametoa mfano wa maeneo ya Marangu na Machame ambako kuna ardhi ndogo. Pamoja na ukweli huo serikali yetu haijapitisha sheria ya kubagua wa-Tanganyika wasio wazawa wa maeneo[marangu,machame] hayo kuhamia huko na kumiliko ardhi huko.
..wa-Tanganyika na wa-Zanzibari wana mahusiano ya kindugu kwa karne kadhaa sasa. Haipendezi mahusiano hayo kuanza kutiwa mushkel ya sheria za kibaguzi kama hii iliyopitishwa na baraza la wawakilishi.
NB:
..Balozi Seif Idi anapigana vikumbo na walalahoi huku Tgk kupata viwanja kule Kigamboni, lakini Prof.Ana Tibaijuka waziri wa ardhi huku Tanganyika hana haki ya kumiliki ardhi Zanzibar.
..Dr.Mohamed Seif Khatib ameuziwa nyumba za serikali ya Tanganyika na waziri John Pombe Magufuli. Nyumba zile hazikuwa na uhusiano wowote na muungano, wizara ya ujenzi si ya muungano. Lakini huyu Pombe Magufuli hana haki ya kumiliki ardhi Zanzibar.
Foum Jnr, W. J. Malecela, Chris Lukosi, Kibunango, Nguruvi3
Kutokana na uhaba wa ardhi Kilimanjaro, wakazi wa huko wanahamia maeneo ya mikoa mingine kama Handeni, Korogwe, Arusha, kiteto, Mkuranga.
Huko wanapewa ardhi bila matatizo. Na hakuna mwananchi kutoka mkoa mwingine aliyenyimwa ardhi Kilimanajaro. Ukienda Wilaya ya Same kule gonja utawakuta akina Chacha wanamiliki ardhi. Ukienda Rombo Hai utawakuta akina Molel, akina Mhina wanamiiliki ardhi n.k. Ukitaka kununua nyumba Moshi ni kisu chako tu, hakuna sheria inakuzuia
Hawa wznz wanasema hilo si jambo la muungano. Vipi mbona elimu ya juu n.k. si mambo yua muungano lakini bado wanataka wapewe tena wakidai utadhani ni haki yao. Wanadai hela za elimu ya juu licha ya kupewa nafasi 1000 bila mkopo na kwa upendeleo.
Mimi nadhani wenye matatizo hapa ni Tanganyika, kama ingelikuwepo msumeno ungekata mbele na nyuma.
Sheria za znz zinatumika Tanganyika. Hakuna sababu ya kupigizana kelele ni kuweka sheria tu za kuwabana mambo yanaisha. Sasa hivi hakuna Tanganyika wanakuja na mgongo wa Tanzania.
Lipo katika yale ya mkataba wa 1964Unatetea Muungano hadi unachoka ki-akili,
Nani alosema Elimu ya Juu sio suala la Muungano..? kama hujui uliza kwanza usikurupuke....!!!