CUF yachemka maandamano kumpinga Hamad jimboni Wawi

CUF yachemka maandamano kumpinga Hamad jimboni Wawi

Nilshasema hayo yote tumeshakubali, sasa tatizo nini? Nyinyi wenye guvu, wasomi, wajuwaji na sifa zote mmepata nini kwa kifo cha watu wawili kule Arusha? Mbona Magamba wanaendelea kupeta hata mnaomba kwenda kunywa juisi na mkuu wa Kaya kama mnavyomwita? Hebu tupe faida mnayopata nyinyi ambayo sisi Wazanzibari hatuipati as far as amani ya nchi ilivyo?

Ukiona katika watu waliokasirika kupatikana kwa muafaka ni chadema zaidi; sijui ni kwanini?

Kama wanaona CUF wamekosa, mbona roho zinawauma sana? something fishy
 
Mods piga ban wapemba wanatuchafulia kiswahili. NYENGINE ndio kitu gani, sema NYINGINE '*-'.xy'z zako we. Maalim akisema 'sawa sawaaaa!' misukule inaitikia 'sawaaaaa!!!' Mtaongozwa na Maalim mpk astaafu kuishi. Inaonekana ni yeye tu ndio mwenye akili kati ya wapemba wote

Ukiona mbwa anaugumilia maumivu jua jiwe/mawe limepata kisawa sawa! Umewekewa 'gear' (Lugha) ndogo tu, na ambayo ni 'size' yako na umeanza kupeleka mashitaka kwa modes, jee wanaume wa shoka wakija na makombora ya uhakika si utahama hata hapa mjengoni? Hii Lugha Wazanzibari ni yetu mali yetu na ndio maana tunaifinyanga tupendavyo na wala hakuna mjinga yeyote wa kutuudhi; labda aje na chuki zake binafsi. Nyinyi wengine munadandia treni kwa nyuma tu! Zanzibar Daimaaa Mbeleee! I swear by the God am proud to be Zanzibariiiiii.
 
Usolijua ni kama usiku wa kiza kinene.

Maalim Seif si tu katibu mkuu wa CUF taifa bali pia ni makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Je Hamad rashid ni nani?

maalim ameunguruma kwa nguvu zote manzese na ving'ora kibao , je Hamad rashid kaunguruma wapi? au habari maelezo?

Alichokifanya makamo wako huyo wa rais ndio kaburi la CUF. Roho yake mbaya inafanya asipate ushindi tena huko visiwani.
 
Ukiona katika watu waliokasirika kupatikana kwa muafaka ni chadema zaidi; sijui ni kwanini?

Kama wanaona CUF wamekosa, mbona roho zinawauma sana? something fishy

Tunasubiri picha za maandamano ya kumpinga HR. Isijekuwa mnapiga porojo tu hapa kumbe hamkupata mtu wa kuandamana.
 
Ukiona katika watu waliokasirika kupatikana kwa muafaka ni chadema zaidi; sijui ni kwanini?

Kama wanaona CUF wamekosa, mbona roho zinawauma sana? something fishy

Hatujakasirika bali tumesikitika kwa maalim kuwauza wapemba wenzake kwa kupewa umakamo wa raisi ceremonial, kazi yake imekuwa ni kufungua na kufunga makongamano, warsha na vitu vya namna hiyo.

Maalim kawasaidia na washirika wake wachache kama sita saba hivi nao wamepata uwaziri sasa wanakula bata na kutekeleza sera za ccm huku wanachama wengine wakiendelea kusota.

Kinachosikitisha zaidi ni kwamba nafasi nyengine zote zilizosalia zimeendelea kuhodhiwa na ccm. Sasa huo muafaka gani wa kipuuzi unaojali maslahi ya upande mmoja na kuwatenga wengine? Na kiongozi yeyote anayekubali kitu kama hicho hana kingine zaidi ya uroho wa madaraka na ubinafsi.
 
Jee ulimsapoti wakati wa Kambi ya Upinzani rasmi kule Bungeni? Una uhuru wa kumsapoti lakini kama unaona ni mzuri mchukue kwenye chama chako badala ya kutaka abaki CUF ambako atabishana nawe katika kugombea Upinzani rasmi.
Naamini hukujua kilichokua kinaendelea Dodoma kipindi kile cha hiyo ishu ya kambi bungeni...........jeushajiulizani kwa nn cdm hadi leo hawajajiunga na vyama vingine vya upinzani ktk kambi Yao? It was not about personal interest, ukiwa mwanachama wa chama fulani lazima ulinde na kutetea sera za chamachako.......vinginevyo kubali kufa kifo cha mende. Alichofanya Hamad akiwa kama kiongozi ilikua sahihi kwa faida ya chama. Hvyo sioni ubaya kwa Hilo.
 
kwani akiwa jembe ndo afanye atakavyo? kanuni na taratibu za watu walio makini hazijali ujembe wa mtu bali uzingatiifu wa sheria, kanuni na taratibu. Bila Kanuni na taratibu kila mpuuzi atafanya anaovyoona inafaa
 
Una uhakikia na unachokisema au unafuata polojo za hamadi kwenye vyombo vya habari na mjengoni Dom tu? Uliza ujibiwe. Hana chochote cha maana alichokifanya wawi na hata 2010 alitemwa kwenye maoni akabebwa na Maalifu Seif-kumbe habebeki akaanza kumkwaruza mbebejai. POLE YAKE
 
Utetezi siyo kupinga kila kitu. Penye ukweli hata kama katenda wazimu au adui yako jifunze kupongeza. Seif hana sababu ya kubeza yanayofanyika sasa Zenji. Kila mwenye macho anaona ati
 
Kumbe inasemekana nalidhani una uhakikia na unachokisema? Tusibni kwa sababu tu ya ushabiki wa kisiasa na mapenzi yetu kwa mtu hata kama bomu
 
Hatujakasirika bali tumesikitika kwa maalim kuwauza wapemba wenzake kwa kupewa umakamo wa raisi ceremonial, kazi yake imekuwa ni kufungua na kufunga makongamano, warsha na vitu vya namna hiyo.

Maalim kawasaidia na washirika wake wachache kama sita saba hivi nao wamepata uwaziri sasa wanakula bata na kutekeleza sera za ccm huku wanachama wengine wakiendelea kusota.

Kinachosikitisha zaidi ni kwamba nafasi nyengine zote zilizosalia zimeendelea kuhodhiwa na ccm. Sasa huo muafaka gani wa kipuuzi unaojali maslahi ya upande mmoja na kuwatenga wengine? Na kiongozi yeyote anayekubali kitu kama hicho hana kingine zaidi ya uroho wa madaraka na ubinafsi.

Mimi akili za watu wa CDM sizielewi kabisaaa! Kwani Slaa angeshinda nyinyi woote mngekuwa mawaziri? Mbona una wivu na wale mawaziri wa Cuf walio kwenye SUK? Halafu lengo la Chama cha siasa ni kutumikia wananchi, sasa CUF angalau wana nafasi ya kuwapa wananchi maendeleo ya kweli kuliko wangekuwa opposition kule ZNZ. Ushahidi ona wslivyofanikiwa kuongeza bei ya karafuu kwa zaid ya 700%. Tuliwahi kusikia hapa CDM wakidai muafaka wao Tanganyika baada ya uchaguzi unadhani wangepewa uwaziri wakina Mbowe wangekataa? Juzi kuitwa ikulu tu kujadili katiba walikimbilia kama inzi kwenye kidinda, wakaambulia juice tu! Aibu CDM mchukueni HR halafu tuone atawafikisha wapi!
 
quote_icon.png
By Priory of Zion
Naona sasa itabidi tuanze kuambiana ukweli! Watanzania tuna kawaida ya kusema mema tu ya marehemu na muda mwingine tunatia chumvi nyingi! Pengine ni njia ya 'kumlaghai' Mungu ili amhurumie! Lakini la Regia kwa hili nadhani linatumiwa na CDM kama mtaji wa kisiasa kujipatia umaarufu! Huku Kondoa niliko hilo jina ndio kwanza wanalisikia! Ukiondoa mchango wake kwenye chama chake kama upo, au kujipendekeza kwake kwa kundi la Mbowe,na kuleta PICHA za mikutano ya CDM hapa JF ; Mimi sioni MCHANGO WAKE kitaifa! Hata bungeni sikuwahi kumsikia akuzungumza lolote la maana!
 
Mimi akili za watu wa CDM sizielewi kabisaaa! Kwani Slaa angeshinda nyinyi woote mngekuwa mawaziri? Mbona una wivu na wale mawaziri wa Cuf walio kwenye SUK? Halafu lengo la Chama cha siasa ni kutumikia wananchi, sasa CUF angalau wana nafasi ya kuwapa wananchi maendeleo ya kweli kuliko wangekuwa opposition kule ZNZ. Ushahidi ona wslivyofanikiwa kuongeza bei ya karafuu kwa zaid ya 700%. Tuliwahi kusikia hapa CDM wakidai muafaka wao Tanganyika baada ya uchaguzi unadhani wangepewa uwaziri wakina Mbowe wangekataa? Juzi kuitwa ikulu tu kujadili katiba walikimbilia kama inzi kwenye kidinda, wakaambulia juice tu! Aibu CDM mchukueni HR halafu tuone atawafikisha wapi!

Unaelewa maana ya serikali wewe au unaropoka tu. Serikali ni kuanzia raisi hadi sheha.

Sasa inapotokea mmeingia muafaka wa kuwasaidieni wachache kuingia serikalini na kuwaacha wengi nje huo ni ubinafsi na kutokuwa na mtazamo wa kitaifa. Huwezi kuwatumikia wananchi kwa kutumia sera za mtu mwingine halafu ujinasibu kwamba unaelewa unachokifanya.

As long mmekubali kuitumikia ccm na kutekeleza sera zake hapo ndipo mnaonyesha kuolewa, kama ungekuwa muafaka wa kweli na SUK lazima mngegawana nafasi mwanzo mwisho. Hamkujifunza kwa jirani zetu hapo ODM na PNU walikuwa wanakwenda pasu kwa pasu katika nafasi zote za uteuzi.
 
Hivi yule Waziri wa Uchukuzi wa Zanzibar anaetoka chama cha Cuf atajiuzulu lini kutokana na ile ajali ya meli pale Nungwi kuuwa wapemba wengi na kupunguza kura nyingi za CUF?
Kumbuka Zanzibar ukipata kura 2000 tu tayari umeukwaa ubunge/ uwakilishi.
 
Hivi kwanini wana CHADEMA na CCM (John Tendwa na Werema) kipindi hichi wanampenda sana Hamad Rashid na kufika hadi kumtetea kama ambavyo inaonekana hapa Jamii Forum, wachangiaji wengi hua wanamtetea na ama kumkweza Hamad Rashid huku wakimponda Maalim na Bingwa wa Siasa Afrika! Jee watu hawa (CCM+CHADEMA) wana mapenzi ya dhati juu ya Hamad Rashid au kwa Vile 'Wafanya biashara wa kisiasa' hawa wanamgombania dalali huyu ili mtaji wao wa kisiasa utononeke na hatimae ifikapo 2015 waje kujipatia pesa zaidi halafu wajifiche kwenye speaker za magari ya music!
Dear mpemba!!!!!!! i swear siku HAMAD RASHID AKIPOKELEWA NA SLAA CDM MIMI nahamia NCCR
HAMAD RASHID ni mpuuzi sana, mpenda madaraka, ndumila kuwili, mchumia tumbo.
nafuu mara mia kufanya kazi na Seif kuliko rashid

Note: Naunga mkono kutimuliwa kwa HR ila pia CUF lazima ikubali imeporomika na kuipeleka juu ni rahisi sana kama itawatumia wabunge wake vizuri. Kwa nini mpaka leo waziri wa usafirishaji zenji hawajibishwi???????
 
Hivi yule Waziri wa Uchukuzi wa Zanzibar anaetoka chama cha Cuf atajiuzulu lini kutokana na ile ajali ya meli pale Nungwi kuuwa wapemba wengi na kupunguza kura nyingi za CUF?
Kumbuka Zanzibar ukipata kura 2000 tu tayari umeukwaa ubunge/ uwakilishi.
kwa kumwacha huyu waziri aendelee CUF wamefanya kosa kubwa kwani kiutendaji hawatofautiani na ccm.
Lazima waziri angebeba collective responsibility kwa kujiuzuli hapo wanainchi tungeona CUF are realistic na sii kuoneana aibu ya kuwajibishana
 
Hivi yule Waziri wa Uchukuzi wa Zanzibar anaetoka chama cha Cuf atajiuzulu lini kutokana na ile ajali ya meli pale Nungwi kuuwa wapemba wengi na kupunguza kura nyingi za CUF?
Kumbuka Zanzibar ukipata kura 2000 tu tayari umeukwaa ubunge/ uwakilishi.[/
masuala Kama haya ya kutowajibika ndio siku zote yanaturudisha nyuma ktk maendeleo. Kwa kuwa cuf IMO kiccm ccm zaidi kwa sera zileee zakulindana ndio sababu Kama chama wameshindwa kumwajibisha Waziri Huyu hata baada ya kutotanguliza maslahi ya wananchi mbele.
Kwa hiyo usitegemee mabadiliko yeyote ya kimaendeleo kupitia SUK znz.
 
Unaelewa maana ya serikali wewe au unaropoka tu. Serikali ni kuanzia raisi hadi sheha.

Sasa inapotokea mmeingia muafaka wa kuwasaidieni wachache kuingia serikalini na kuwaacha wengi nje huo ni ubinafsi na kutokuwa na mtazamo wa kitaifa. Huwezi kuwatumikia wananchi kwa kutumia sera za mtu mwingine halafu ujinasibu kwamba unaelewa unachokifanya.

As long mmekubali kuitumikia ccm na kutekeleza sera zake hapo ndipo mnaonyesha kuolewa, kama ungekuwa muafaka wa kweli na SUK lazima mngegawana nafasi mwanzo mwisho. Hamkujifunza kwa jirani zetu hapo ODM na PNU walikuwa wanakwenda pasu kwa pasu katika nafasi zote za uteuzi.

Mwita maranya,

Naomba ufahamu kuwa nia na dhumuni ya chama chochote cha siasa duniani ni kuchukua madaraka ya kuongoza nchi lakin ikiwa na nia ya kuleta maendeleo kwa jamii husika.

Vile vile unatakiwa kujua kuwa kila Chama kina katiba yake ambayo siku zote inaendana na mila, desturi na sirka za jamii husika. Sasa unapozungumzia Kenya na Zanzibar ni vitu viwili tofauti kabisa kuanzia mila ,desturi na hata sirka za sehemu hizo ingawa dhumuni linabaki pale pale kuleta ustawi wa jamii na kukuza uchumi lakin vipaumbele ni tofauti kabisa kulingana na mazingira na mila na desturi.

Kwa mazingira ya Znz na siasa za Znz kilichofanyika ni kitu muhimu sana kwani wengi tunakitazama katika kuleta ustawi wa jamii na kukuza uchumi wa wananchi wa visiwani. Napenda kukujuza kuwa kasi ya kukua kwa uchumi wa Znz imepanda kutoka 3.4% tokea 2000 - 2005 na 6.3% mwaka 2005- 2010. Lakin kwa mwaka mmoja wa SUK uchumi umeongezeka kwa 37% kitu ambacho ndio wananchi wanataka.

Kumbuka kuwa wananchi siku zote wanataka kukuwa kwa uchumi wao na kuleta faraja na ustawi wa jamii na sio malumbano.

Kwa WaZnz na wachumi wote duniani nafikiri watakubaliana na mimi kuwa siku zote jamii inataka kuona inaendelea kiuchumi na sio kisiasa. kukuwa kwa uchumi kunaleta faraja kwa jamii.

Sasa kwa mazingira ya muafaka wa Kenya ilibidi iwe hivyo na kwa mazingira ya Znz naona wapo sawia kabisa. Kumbuka haiwezekani wote kuingia serikalini lakin lazima kuwe na wale wengine pembeni wa kuona na kutoa mawazo yao kwa ajili ya mustakabali bora wa jamii hususan kukuza uchumi.

Kumbuka bottom line ya kila kitu ni kukuza uchumi na si vinginevyo.
 
Imekula kwenu usijifanye umeridhika. Kilichopo hapo ni kuwa mmemsindikiza Maalim Sharifu Ikulu mkidhani na nyie mtaingia, sasa ameamua kuibomoa CUF huku mnamshangilia. Serikali gani yenye viongozi 400 lkn ni mmoja tu ndio anafanywa boshen kuwazuga na nyie kwa upemba wenu mnaitkia sawaaaa.

Kweli maalim kiboko yenu

Pilipili yaliwa shamba nyie inawawashia nini?

Au sababu Hamad Rashid Pandikizi lenu ndani ya CUF Limefukuzwa? Kwani msiwe wa wazi mchukueni basi kama mnamuona dhahabu kwenu na sio kuleta chokochoko.

Lakin nashangaa Znz shwari kabisaaaaa hakuna maneno. Kwanini Bara wanaleta chokochoko. au Hamad Rashid alikuwa anawapa nini?

Tutajua mengi ya hamad baada ya kutimuliwa kwani wote waliokuwa wananufaika naye watapiga kelele na ndio hizi tunazisikia.

Back
Top Bottom