Tulishinikizwa kumfukuza MHE. HAMAD Rashid - Mzee Machano (Makamu Mwenyekiti Taifa-CUF) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tulishinikizwa kumfukuza MHE. HAMAD Rashid - Mzee Machano (Makamu Mwenyekiti Taifa-CUF)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by hasan124, Mar 20, 2012.

 1. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Katika ule muendelezo wa Kuweweseka na jinamizi la kumfukuza Mhe. HAMAD Rashid Mohamed, Mbunge wa Wawi kupitia CUF, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Mzee Machano ameibuka na kusema kwamba walishinikizwa na Katibu Mkuu akishirikiana na Kaimu wake kumfukuza MHE. HAMAD.

  Habari hizi za ndani zimedai kwamba makubaliano hayakuwa kufukuza Bali ni kutoa onyo tu, ila hali ilikuja kubadilika ghafla kabla kikao hicho hakijaanza pale Masons Hotel mjini Zanzibar, ambapo shinikizo Hilo la Katibu na Mpambe wake Jusa kuwazidi wajumbe waliohudhuria kikao hicho cha tar.04-01-2012. Shinikizo ambalo ndilo lililopelekea hata kura za kuwafukuza MHE. HAMAD na wenzake kuwa ni za kunyanyua MKONO juu na kuhesabiwa wakihofu endapo watapiga kura za Siri lengo lisingetimia.

  Habari hizi za ndani zimekuja siku chache baada ya Mwenyekiti wa Chama Taifa Prof. I. Lipumba kupokewa kwa gharama Kubwa ambazo zingeiwezesha CCM B kuingia kwenye uchaguzi huko Arumeru, Jambo hili linalotafsiriwa na wajuzi wa mambo kuwa ni moja kati ya Matumizi mabaya ya raslimali watu na fedha kwani mapokezi hayawezi kuipa ushindi hata wa udiwani CUF almaarufu Kama CCM B bali imejikuta ikipata gharama zaidi za kuuguza majeruhi waliopata ajili katika mapokezi HAYO.

  Inapotokea chama cha siasa chenye miaka ishirini toka kusajiliwa, ni sehemu ya serikali katika upande mmoja wa Nchi, kinapata ruzuku na michango ya wabunge wake zaidi ya thelathini ambao huchanga zaidi ya shilingi million moja kwa mwezi kila mmoja lakini kinashindwa kushiriki uchaguzi mdogo kwa kisingizio chochote, hapo ni kuonyesha mwisho wa chama chenyewe.

  Kwa maoni yangu CUF wanatakiwa watambue kwamba Uhai wa Chama haupimwi kwa Maandamano au Mapokezi Bali Matokeo ya Uchaguzi, na ni vyema watu wajue aliyepokelewa ni Profesa Lipumba sio CUF kwa kuthibitisha hili asafiri kiongozi mwingine halafu waandae HAYO mapokezi tuone.

  Source: Rest in peace.

   
 2. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,135
  Likes Received: 6,630
  Trophy Points: 280
  ngoja waje wachambuzi mkuu.
   
 3. Dullo

  Dullo JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 24, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haya tumekusikia, asante kwa kutujuza!!
   
 4. kakakuona40

  kakakuona40 JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Habari za kutengeneza utazijua tu, wala huhitaji kuwa na div IV kuzitambua! hata mimi mwenye zero nimegundua hilo, kuna utata kwa uliyoyaandika na kuchanganya maudhui.
   
 5. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Rip cuf
   
 6. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Utabaki na zero Yako hivyo hivyo, hizi ni nyeti za ndani na hao unaowajua wanajua huu ndio ukweli. Hakurupuki MTU hapa.
   
 7. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Onyesha huo utata uko wapi, usikimbilie kuwenda viwango vya form 4 kama kigezo ili watu wajifanye wameugundua huo utata kwa kuogopa wataonekana hawajafika hiyo form four yako.

  Hii Habari ina utata gani? au amegusa interests zako? au na wewe ulinyanyua mikono nini?
   
 8. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hamadi Rashidi ni bora upumzike sasa tumekuchoka! Umejaribu kuiua CUF umedondokea pua vibaya! Wananchi wamekupa jibu siku ile tar 11/03/2012! Wewe endeleza ADC au kapige mzinga kwa PINDA! Siku rip CUF haina mvuto! Watu wameona ukweli!
   
 9. m

  mkigoma JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 1,182
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hamad na Vibaraka wake KUSHINEYI
   
 10. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Igunga mlitumia million 300, Mapokezi ya Prof. Million almost 300, imekaa vipi hii?! Kumbe ndio maana hamkutaka kusimamisha mgombea Arumeru kisa kampeni hii ya prof. Mkidhani ndio muokozi wenu? Poleni sana kwani kachelewa timing imekataa.
  "Izraeli na Roho ya CUF"
   
 11. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #11
  Mar 20, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,785
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  CUF ina matatizo lakini simuoni HR kama kweli alianzisha mapambano kwa nia ya kukisaidia chama chake bali ili nae ale!!
   
 12. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #12
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Binafsi naamini Kama Suala ni kula HAMAD Rashid ana neema Siku nyingi tu, na wao CUF wanajua Hilo, naamini aliamua kulianzisha baada ya kuona ouzo usiovumilika, msafi yeyote hawezi kuishi sehemu chafu na Ndicho alichofanya HAMAD Rashid. Hasa ukitazama sababu alizotoa mfano: chama kujikita zaidi Zanzibar na kuitosa bara.
   
 13. kakakuona40

  kakakuona40 JF-Expert Member

  #13
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hakuna ushahidi wowote uliouonyesha kuwa mwekekiti amethibitisha hayo madai yako, pia suala la kutoshiriki uchaguzi huo ni uamuzi sahihi kwa siasa inaendana na uchunguzi na tathmin ya kina, huwezi kutumia mamilion ya pesa wakati bado chama hakijajijenga vya kutosha katika eneo husika, ukubali ukatae vyama vya upinzani havona ushawishi katika maeneo mengi ya nchi isipokuwa ni baadhi tu ya eneo, mi naikili hoja ya kuimalisha kile ulichonacho wakati ukitafuta kingine ni bora sana.
  Acha propaganda za kitoto
  Na ndio maana tatzania hatuendelei kwa taarifa za kutunga
  shame on u
   
 14. w

  woyowoyo Senior Member

  #14
  Mar 20, 2012
  Joined: Jul 24, 2011
  Messages: 173
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyu Hamad Rashid alipokuwa kiongozi wa chama alijenga chama wapi? zaidi ni kugombea vyeo ndani ya CUF, kamfanyia fitna wilfred Rwakatare ili asishinde ubunge Bukoba mjini 2005 alikuwa anajua Lwakatare angeshinda ubunge yeye asingepata nafasi ya kuongoza kambi ya upinzani bungeni kwa kuwa Lwakatare alikuwa Naibu katibu mkuu.
   
 15. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #15
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wale waleeeee!! Kwani fukuza fukuza ndani y CUF imeanzia wapi? Kama sio sultani na ubinafsi wake.
   
Loading...