CUF waitaka ZEC kuondoa jina la Maalim Seif kwenye karatasi za kura

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Chama kikuu cha upinzani Zanzibar CUF, kimeitaka Tume ya Uchaguzi visiwani humo ZEC kuondoa na kutotumia karatasi za kupigia kura zenye kuonesha jina la mgombea wake wa urais pamoja na baraza la wawakilishi kwa lengo la kugomea uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika Machi 20 visiwani humo.

Chanzo: DW Swahili
 
Wamewaeleza tu kwa mdomo au officially kwa barua? Tume haitokaa ijarubu kufanya hivyo asilani.
 
Hata nembo hawaruhusiwi kuitumia maana chama kimesajiliwa kwa mujibu wa sheria .na kama jecha atanga'ngania uccm wake akatumia atafunguliwa mashtaka ya kutumia nembo ya chama bila ridhaa
 
ZEC na serekali yake haijalishwi na marekani na jumuia ya ulaya na hawamuogopi yoyote awe marekani au ulaya hahwatwlishwi hawana ubavu ccm iko imara wanajiweza wana vikosi vya smz na mazombe kwahiyo washike abadu zao marekani na vibaraka wao
 
Hivi kwa nini hao ZEC wasimuapishe tu huyo ' Gbagbo' wao wa Zenji aendelee kushika madaraka hayo ya Urais, ambayo hataki kabisa kuyaachia ingawa wazanzibari wamemkataa kwenye sanduku la kura tarehe 25/10/2015?

Hivi si bora tu hizo bilioni 7 walizopanga kutumia kwenye huo uchaguzi wa marejeo wakazitumia kwenye shughuli zingine za maendeleo kama vile ujenzi wa barabara, kuliko hii kitu wanayotaka kuifanya ya kwenda kuzifuja kwenye huo wanaouita uchaguzi wa marejeo, wakati katika hali halisi weshamuandaa Shein wao kumwapisha tarehe 21/03/2016?
 
ZEC na serekali yake haijalishwi na marekani na jumuia ya ulaya na hawamuogopi yoyote awe marekani au ulaya hahwatwlishwi hawana ubavu ccm iko imara wanajiweza wana vikosi vya smz na mazombe kwahiyo washike abadu zao marekani na vibaraka wao
umeishia darasa la ngapi wewe jinga?!!
 
Back
Top Bottom